Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Title
Now showing 1 - 20 of 320
Results Per Page
Sort Options
Item Athari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzo(University of Dar es Salaam, 2014) Malindi, BakitaUtafiti huu unahusu Athari za matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo, uliofanyika katika mkoa wa Mara manispaa ya Musoma katika kata za Mwisenge, Iringo, Mkendo, Nyakato na Kamnyonge. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 40 ambapo wanawake walikuwa 20 na wanaume walikuwa 20, vilevile kila kata ilitoa watafitiwa 8. Utafiti huu ulilenga kwanza kubaini matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Pili, kubainisha makundi ya jamii yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa kuzingatia jinsi, umri na kiwango cha elimu. Tatu, kueleza sababu za kutumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo.Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha wazi kuwa kuna baadhi ya matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Matamshi hayo ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo hutokana na matumizi ya mara kwa mara ya lugha ya Kikwaya, kutopata elimu na kutumia lugha mbili au zaidi katika eneo moja. Utafiti huu pia umedhihirisha makundi ya jamii ya watafitiwa yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo. Makundi hayo mtafiti ameyagawa katika sehemu mbili, yaani kuna makundi ya watafitiwa wanaotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa wingi, na kuna makundi ya watafitiwa wasiotumia sana matamshi ya Kikwaya. Makundi yanayotumia sana matamshi ya Kikwaya ni wazee (72%), wakulima (74%), wasiosoma (72%), wanawake (70%) na wafanyabiashara (60%). Hali kadhalika makundi ya watafitiwa yasiyotumia sana matamshi ya Kikwaya ni vijana (39%),waliosoma shule (48%), wanaume (52%) na wafanyakazi (45%).Item Athari ya mhariri katika mswada: uchunguzi wa machapisho teule ya kifasihi ya Kiswahili(University of Dar es Salaam, 2017) Pacho, Peter JacoboUtafiti huu umelenga kuchunguza Athari ya Mhariri katika Miswada ya Kifasihi ya Kiswahili. Hii inatokana na kuwapo kwa malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya waandishi juu ya namna wahariri wanavyohariri miswada yao. Malalamiko hayo husababisha kuwapo kwa mgongano baina ya wahariri na waandishi. Hoja ya msingi katika utafiti huu ni kuwa mhariri ni kiungo muhimu sana katika tasnia ya uchapishaji licha ya kuwapo kwa dosari ndogondogo zinazojitokeza kwa wahariri wasiokuwa makini. Mtafiti ameongozwa na malengo mahususi, yaani kubaini sifa za mhariri wa miswada ya kifasihi ya Kiswahili, kufafanua majukumu ya mhariri wa miswada ya kifasihi ya Kiswahili na jinsi anavyozingatia majukumu yake na kubainisha athari za mhariri katika miswada ya kifasihi ya Kiswahili. Katika ukusanyaji wa data za uwandani na maktabani katika wilaya za Kinondoni, Ubungo na Ilala, mtafiti ametumia mbinu za mahojiano na uchambuzi na uchanganuzi wa matini teule. Kwa kutumia Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji, Nadharia ya Uhariri na baadhi ya Kanuni za Uhariri zimeweza kubainika athari chanya na athari hasi za mhariri. Athari chanya ni kuboresha lugha ya mwandishi; kuboresha msuko wa hadithi na kuboresha maudhui ya kitabu. Kwa upande mwingine athari hasi ni kubadili jina na umbo la kitabu; kucheleweshwa kwa miswada; athari za kidhana na kimaana; kubadili sauti ya mwandishi na kukosekana kwa ushikamani, uthabiti na muwala. Licha ya kuwapo kwa malalamiko mengi ya waandishi juu ya namna wahariri wanavyohariri kazi zao, na kuonesha kuwa kwa sehemu kubwa wahariri wanaharibu miswada yao. Mtafiti amegundua kuwa mengi ya malalamiko hayo siyo ya msingi, na yanatokana na waandishi wengi kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na taaluma ya uchapishaji, hususan kipengele cha uhariri.Item Athari ya utendaji simulizi katika mabadiliko ya ushairi andishi wa kiswahili uchunguzi wa diwani za e. Kezilahabi - dhifa na karibu ndani(University of Dar es Salaam, 2015) Ally, LailaUtafiti huu umechunguza athari ya utendaji simulizi katika mabadiliko ya ushairi andishi wa Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka diwani za E. Kezilahabi za Dhifa (2008) na Karibu Ndani (1988). Aidha, ili kuweza kuona namna mabadiliko na miundo mipya ya ushairi wa Kiswahili ilivyozuka, matumizi ya mbinu za fasihi simulizi, ambazo zo katika utafiti huu tumeziita vipengele vya utendaji simulizi yamechunguzwa. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za maktabani pamoja na uwandani. Mbinu za maktabani zilihusisha usomaji wa diwani mbili za Kezilahabi, Dhifa na Karibu Ndani kwa lengo la kubaini mbinu mbalimbali za utendaji simulizi alizotumia mtunzi katika mashairi yake. Kwa upande mwingine, mtafiti alitumia mbinu za utafiti wa uwandani kwa kuwahoji wadau mbalimbali wa taaluma ya ushairi wa Kiswahili kuhusiana na ujitokezaji wa vipengele vya utendaji simulizi katika Dhifa na Karibu Ndani, dhima za vipengele hivyo pamoja na athari zake katika mabadiliko ya ushairi andishi wa Kiswahili. Uchambuzi wa data za utafiti huu ulifanyika kwa kutumia misingi ya nadharia ya naratolojia pamoja na nadharia ya fomula simulizi. Misingi ya nadharia ya naratolojia iliyotumika katika utafiti huu imedondolewa kutoka katika kiunzi cha nadharia ya naratolojia kama kilivyoasisiwa na kuendelezwa na Bal (1997), Genette (1988) na Monika (2009). Nadharia hii imesaidia kujadili masuala yanayohusiana na matumizi ya vipengele vya utendaji simulizi. Masuala hayo ni pamoja na usimulizi, nafsi za usimulizi na njeo za usimulizi. Kwa upande mwingine, mjadala wa athari ya utendaji simulizi katika mabadiliko ya ushairi andishi wa Kiswahili uliongozwa na nadharia ya fomula simulizi kama ilivyoelezwa na Parry (1971) na Lord (1981). Kutokana na uchunguzi uliofanyika katika utafiti huu imedhihirika kuwa diwani za Karibu Ndani na Dhifa zimesheheni matumizi ya mbinu mbalimbali za utendaji simulizi. Mbinu hizo ni pamoja na matumizi ya visasili, mbinu za usimuliaji, ujazilizaji wa usimulizi katika wakati uliopo, ujao na uliopita, matumizi ya miundo ya fasihi simulizi, taswira, matumizi ya tashibiha, matumizi ya mbinu ya ukiushi pamoja na takriri. Vilevile mtokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa matumizi ya vipengele vya utendaji simulizi yameathiri ushairi andishi wa Kiswahili kifani na kimaudhui. Kusheheni kwa vipengele vya utendaji simulizi katika ushairi andishi wa Kiswahili - Dhifa na Karibu Ndani kunaimarisha hoja zinazoshadidia kuwa ushairi wa Kiswahili umetokana na fasihi simulizi ya Kiafrika.Item Athari za kifonolojia na kimofolojia za Kiswahili cha mwambao wa ziwa Tanganyika Katika Kiswahili sanifu(University of Dar es Salaam, 2016) Isindikiro, JosephUtafiti huu umechunguza sifa na athari za kifonolojia na kimofolojia za Kiswahili cha Mwambao wa ziwa Tanganyika katika Kiswahili sanifu ili kubaini hali ya kiisimu ya Kiswahili sanifu katika eneo ambalo ni makutano ya watumiaji wa Kiswahili kutoka Tanzania, Kongo, Burundi na Zambia wakiwa na lugha zao za makabila pia. Utafiti huu umetumia data kutoka uwandani na maktabani. Data ya uwandani, imekusanywa katika kata za mwambao wa ziwa Tanganyika, wilayani Nkasi kwa kutumia mbinu za ushuhudiaji, hojaji, usaili na utungaji wa insha. Kata hizo zimeteuliwa kutokana na uhusiano mkubwa wa kibiashara na kijamii baina ya watumiaji wa Kiswahili sanifu kutoka Tanzania, Kiswahili cha Kongo, Kiswahili cha Zambia na Kiswahili cha Burundi. Data ya maktabani imetumika kufafanua na kushadidia hoja na data ya uwandani katika ilivyofafanua vipengele mbalimbali. Data imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kiidadi. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Mwachano na Makutano na Nadhariatete ya Ndugu na Ndugu wa Mbali iliyoasisiwa na Massamba (2007). Nadharia hii imeonekana kulandana na hali halisi ya Kiswahili kinachotumiwa eneo la utafiti. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa Kiswahili sanifu katika mwambao wa ziwa Tanganyika kimepata athari katika vipengele vya fonolojia na mofolojia kutokana na makutano ya watumiaji wake na watumiaji kutoka maeneo mengine ya utafiti huu. Aidha, uthari hizo zimesababisha baadhi ya maumbo katika msamiati wa Kiswahili sanifu kuathirika na kuonekana kuwa msamiati mpya katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Utafiti unapendekeza kufanyika kwa utafiti mwingine kama huu utakaojikita katika kuchunguza mchango wa KMZT katika msamiati wa Kiswahili sanifu. Aidha, unaweza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu vipengele vya kiisimu kinachotajwa na baadhi ya wanaisimu kuwa Kiswahili sanifu cha Kongo.Item Athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya kisiha(University of Dar es Salaam, 2017) Kileo, Joan GodwinLengo la utafiti huu ni kuchunguza athari za Kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha. Utafiti huu una malengo mahususi matatu ambayo ni: kubainisha maneno ya lugha ya Kiswahili yaliyomo katika lugha ya Kisiha, kueleza athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha, na kufafanua sababu za athari za kimofofonolojia za lugha ya Kiswahili katika lugha ya Kisiha. Chanzo cha data kilichotumika katika utafiti huu ni uwandani. Data zilikusanywa kwa njia ya mahojiano, hojaji na ushuhudiaji kutoka kwa wazee wenye rika la kati ya miaka 50-85 na wanafunzi wa kati ya miaka 10-14 katika wilaya ya Siha. Data zilizopatikana katika utafiti huu zilichambuliwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles (1982). Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa lugha ya Kisiha imeathiriwa na lugha ya Kiswahili hasa katika kipengele cha mofolojia. Aidha, athari za kifonolojia zimejitokeza katika kipengele cha sauti za Kiswahili zilizotumiwa na watoa taarifa wakati walipokuwa wanazungumza Kisiha. Athari hizo ni matumizi ya sauti [z] badala ya sauti [s], sauti [m] badala ya sauti [n], sauti [ch] badala ya sauti [sh] pamoja na udondoshaji wa sauti [h] ya Kisiha. Fauka ya hayo, utafiti huu umeweka bayana sababu za athari za kimofofonolojia za Kiswahili katika lugha ya Kisiha, ambapo miongoni mwa sababu hizo ni elimu, biashara, pamoja na upanuzi wa matumizi ya Kiswahili vijijni. Mwisho ni muhtasari wa utafiti, matokeo ya utafiti, mchango wa utafiti pamoja na mapendekezo ya tafiti fuatishi ambapo imependekezwa kuwa tafiti zifanyike katika vipengele ambavyo havikushughulikiwa, kama vile sintaksia na semantiki. Aidha, kuna haja ya kufanya tafiti kuhusu mbinu na mikakati ya kuchochea matumizi ya lugha ya Kisiha katika muktadha huu wa kutamalaki kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kudumisha lugha ya Kisiha.Item Athari za kiswahili katika msamiati wa kiwanji(University of Dar es Salaam, 2014) Lusanjala, Sharon UmotiUtafiti huu umeshughulikia Athari za Kiswahili katika Msamiati wa Kiwanji. Utafiti huu umefanyika wilayani Makete, Mkoa wa Njombe nchini Tanzania. Ili kufikia malengo yake, mbinu na njia mbalimbali za utafiti zikiwa ni pamoja na mbinu ya maktabani na uwandani zimetumika. Na njia zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni mahojiano pamoja na ushuhudiaji. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles na Byrne (1982), ambayo inaeleza kuwa lugha zinazokaribiana kimaeneo zinaweza kuathiriana. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kuna athari mbalimbali za Kiswahili katika msamiati wa Kiwanji ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya msamiati wa Kiswahili katika Kiwanji, athari ya uchanganyaji lugha, upotoshaji wa matamshi sahihi ya msamiati wa Kiwanji, msamiati asilia wa Kiwanji kupotea, na msamiati wa Kiwanji kupungua matumizi. Vilevile, sababu zilizobainika ambazo huchangia athari hizi ni pamoja na mwingiliano wa kimatumizi wa Kiswahili na Kiwanji, baadhi ya maeneo kutozungumza Kiwanji, pia fahari ya kutumia Kiswahili kuliko Kiwanji, uhaba wa msamiati wa Kiwanji, na shughuli za kijamii na kibiashara. Mapendekezo yaliyotolewa ili kupunguza athari hizi ni pamoja na kuandaa makongamano na warsha mbalimbali za kuelimisha kuhusu umuhimu wa lugha za asili kama Kiwanji. Pia lugha ya Kiwanji ifanyiwe tafiti zaidi, ili iweze kuandikiwa kwa lengo la kusomwa na watu mbalimbali pamoja na kuitunza, kukipa Kiwanji dhima mbalimbali katika jamii, na kudumisha uhalisia wa lugha hiyo kwa kuzienzi mila na desturi.Item Athari za maendeleo ya Sayansi na teknolojia katika nyimbo za michezo ya watoto: mifano kutoka katika Mkoa wa Dar es Salaam(University of Dar es Salaam, 2011) Urassa, Costansia CosntantiniUtafiti huu unabainisha athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia katika fasihi ya watoto hususani nyimbo za michezo ya watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam .Watoto wa Mkoa huo wanachukuliwa kama kiwakilishi tu cha watoto wakitanzania popote walipo mijini na vijijini nchini Tanzania ili kufanikisha kupata data za utafiti huu, mtafi ti alitcmbelea rnaeneo yal iyoteul iwa katika Mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya zote talu yaani, Wilaya ya Temeke, Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Kinondoni, ambayo kwa kiasi fulani yanah usika na maendeleo ya sa) ansi na teknolojia. Mbinu zilizotumika katika kupata data za utafiti huu ni mbinu ya mahojiano/ usaili, mbinu ya hojaji na mbinu ya ushiriki Katika utafiti huu, nadharia ya Sosholojia ilifanikisha uchambuzi sahih wa data za utafiti. Hivyo mtafiti alifanikiwa kubainisha athari Chanya ambazo ni kurahisisha kuenea kwa nyimbo za watoto kutoka eneo moja kwenda nyingine kukuza vipaji vya watoro. kukuza ajira, kuleta umoja miongoni mwa watoto, kutunza kumbukumbu, kuungan isha vizazi mbalimbali na jamii na kukuza ubunifu miongoni mwa watoto. Athari Hasi ni kupoteza utendaji, k.utobadil ika kwa kazi ya sanaa ku lingana na wakati na malezi ya watoto. Hivyo malengo ya utafiti huu yamefikiwa na maswali yamejibiwa kama yalivyokusudiwa. Utafiti huu ulibaini pia kwamba kuna Fulani zilizofanyika na wanazuoni mbalimbali ili kuendeleza Fasihi ya Watoto hususani michezo ya watoto wadogo, na hasa ile inayoambatana na nyimbo. Hata hivyo tafiti zilizofanyiwa kuhusu nyimbo za michezo ya watoto bado hazitoshelezi.Item athari za matamshi ya msamiati wa Kiswahili sanifu katika kimakunduchi(The university of Dar es Salaam, 2012) Khamis, MaryamSuala la kuathiriana kwa lugha limejadiliwa na wataalamu wengi. Hata hivyo hakuna utafiti uliofanywa juu ya athari za matamshi ya Kiswahili sanifu katika lahaja ya Kimakunduchi. Utafiti huu ulinuiliwa kuchunguza athari za matamshi ya Kiswahili sanifu katika Kimakunduchi. Sura ya kwanza inaeleza kuhusu lahaja inayotafitiwa kuwa ni Kimakunduchi na inazungumzwa Unguja katika Mkoa wa Kusini na Wilaya ya Kusini katika kijiji cha Makunduchi. Tatizo kubwa katika uchunguzi ilikuwa upande wa matamshi hususani katika sauti ikiwemo ubadilikaji uchopekeji na udondoshaji. Madhumuni ya uchunguzi huu ni kuchunguza athari za matamshi ya Kiswahili sanifu katika Kimakunduchi na sababu za kutokea kwa athari hizo. Mada hii imechaguliwa kwa sababu, watafiti wameangalia vipengele hivyo vya matamshi lakini wamevifananisha na kuvitofautisha kutoka lahaja moja na nyingine. Hivyo kutokana na upeo wa mtafiti hakuna utafiti uliofanywa kuhusu mada hii. Utafiti huu utakuwa na manufaa kwa watafiti wa lugha kiisimu, walimu na wanafunzi wa Kimakunduchi wanaojifunza Kiswahili sanifu. Sura ya pili ya utafti inashughulikia mapitio na machapisho mbalimbali yanayochukuzana na mada. Sura ya tatu inashughulikia mbinu za utafiti na ukusanyaji wa data. Aidha malengo ya utafiti yalifikiwa na kukidhiwa haja maridhawa. Zana za utafiti zilitumika katika kukusanyia na kuchambulia data. Aidha utafiti ulitumia mbinu za uwandani na maktabani. Data ilikusanywa kwa njia ya mahojiano, hojaji na ushuhudiaji. Mbali na mbinu hizi, utafiti uliongozwa na nadharia ya Muachano na Makutano ambayo inadai kuwa; Jamii lugha moja inapoingiliana na jamiilugha nyingine, lugha za wanajamii hawa huathirika na kuanza kutokea athari katika vipengele kadhaa vya kiisimu vya lugha hiyo na hatimaye kuwa lugha moja.Sura ya nne, inawasilisha matokeo ya utafiti. Kutokanana na utafiti huu imebainika kuwa; lahaja ya Kimakunduchi imeathiriwa na Kiswahili sanifu katika vipengele vya matamshi ya maneno yake, kwa kubadilisha sauti, matumizi ya maneno ya Kiswahili sanifu badala ya Kimakunduchi na michakato mingine ya kifonolojia kama vile; udondoshaji na uchopekaji wa sauti na kutokana na athari hizo, hatimaye msamiati huo hutamkwa sawa na Kiswahili sanifu. Sanjari na hayo, utafiti huu umeweka bayana sababu za kuathiriwa Kimakunduchi, ambapo miongoni mwake ni pamoja na muingiliano wa wanajamii tofauti tofauti kutokana na sababu za kiuchumi na kijamii, kuenea kwa vyombo vya habari, Serikali kusisitiza matumizi ya Kiswahili sanifu badala ya lahaja ya Kimakunduchi, mtazamo hasi juu ya matumizi ya lahaja hii na ukaribu wa kijiografia kutoka Mjini Unguja na Makunduchi. Sura ya tano inatoa matokeo ya utafiti, hitimisho pamoja na mapendekezo kwa ajili ya kuboresha utafiti unaohusu kuathiriana kwa lugha na isimu kwa jumla.Item Athari za mtindo katika kuibua maudhui: mifano kutoka bembelezi za Pemba(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2013) Ali, Saumu IddiUtafiti huu unachunguza namna mtindo unavyoibua maudhui kwa kutumia mifano kutoka bembelezi za Pemba. Baada ya kuona kuwa wataalamu wengi wamesema bembelezi humhusu mama na malalamiko yake tu na wala hazimuhusu mtoto anayeimbiwa. Kutokana na maudhui mazito yanayojitokeza katika nyimbo hizo kama vile ndoa ukewenza, mapenzi na kadhalika. Utafiti huu ulilenga kubaini ni mbinu zipi zitumikazo kusawiriwa maudhui hayo na wakati huo huo mtoto akafarijika akanyamaza na akapata usingizi. Mbinu zitumikazo kama vile sauti ya upole, yenye kusihi na viitikio vyake ambavyo hurudiwarudiwa kwa mahadhi ndio humlaghai mtoto akanyamaza kulia na hata akajisikia kulala. Ili kufanikisha hayo mtafiti alitumia mbinu ya kupitia machapisho mbalimbali na kwenda uwandani kupata nyimbo, vyanzo vya nyimbo na maana zake. Baada ya kupata data mtafiti alichanganua na kufanya mjadala kwa kuhusisha na nadharia ya Uchambuzi wa Matini na Mwingiliano Matini. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa bembelezi asili yake haikuwa na makusudi hayo bali kina mama walizipata kutoka katika ngoma mbalimbali na walikuja kuzitumia katika matumizi yao yakiwamo haya ya kubembelezea watoto ambapo ziliongezwa, kupunguzwa na hata kubadilika kulingana na tukio, eneo na mambo yaliyozuka katika jamii. Baada ya kuhakiki sampuli ya nyimbo imebainika kuwa bembelezi husawiri kina mama, baba na watoto pia, sio kama ilivyozoeleka ni kwa ajili ya kina mama tu kutoa dukuduku lao au kwa ajili ya watoto tu ili walale au wanyamaze kulia. Ingawa hizo baadhi zinazowahusu watoto sio katika umri huo walio nao bali mpaka wakuwe wakubwa. Ingawa utafiti huu umechunguza kipengele cha mtindo katika kuibua maudhui na hadhira lengwa bado kuna maeneo yanahitaji utafiti wa kina. Maeneo hayo ni ishara na picha, falsafa katika bembelezi na fasihi simulizi kwa ujumla wake katika kisiwa cha Pemba.Item Athari za ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2012) Katuma, RehemaUtafiti huu unahusu Athari za Ukopaji wa Msamiati wa Kiswahili katika Lugha ya Kinyakyusa. Utafiti umefanyika nyanda za juu Kusini katika mkoa wa Mbeya wilayani Kyela katika kata nne za Kyela Mjini, Ikolo, Bujonde na Kajunjumele. Utafiti umehusisha mbinu kuu mbili za ukusanyaji wa data. Mbinu hizo ni usaili na ushuhudiaji. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa umeathiri msamiati wa lugha ya Kinyakyusa kifonolojia, kileksika, kimofolojia na kisemantiki. Ukopaji wa msamiati unatokana na sababu tofautitofauti: fahari na hadhi inayoambatana na lugha chanzi, kutaja vitu na dhana mpya ambavyo hapo awali havikuwapo katika lugha pokezi, kupanua maana za maneno na kuondoa utata. Aidha, maneno ya mkopo huenda sambamba na michakato ya uingizaji katika lugha pokezi kama vile ubadilishaji wa sauti, usilimishaji wa sauti, uchopekaji wa konsonanti na irabu na uingizaji wa nomino katika ngeli za majina. Pia, utafiti ulibaini athari za ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa, nazo ni: athari za kifonolojia, kileksika, kimofolojia na kisemantiki. Ukopaji wa msamiati mpya kutoka lugha ya Kiswahili katika Kinyakyusa umesababisha uongezekaji wa sauti mpya. Hivyo basi, ipo haja ya kuchunguza idadi ya sauti hizo katika lugha ya Kinyakyusa.Item Athari za ukristo katika ngoma za kijadi za kabila la Wandali(University of Dar es Salaam, 2016) Masebo, Jubeck AlinineUtafiti huu una bainisha athari za Ukristo kwa ngoma za kijadi za kabila la Wandali. Wananchi wa kata yakafulena ikingawa na chukuliwa kama kiwakilishi tu cha Wandali popote walipo katika tarafa ya Undali wilaya ya Ileje. Ilikufanikisha kupata data za utafiti huu, mtafiti alitembelea maeneo yaliyoteuliwa katika kata ya kafulena Ikinga ambayo kwa kiasi Fulani yanahusika na ngoma ya Ling; omana dhehebu la Moravian. Mbinu zilizotumika katika kupata data za utafiti huu ni mbinu ya mahojiano/ usaili, mbinu ya kushuhudia na mbinu ya ushiriki. Katika utafiti huu, nadharia ya Sosholojia ilifanikisha uchambuzi sahihi wa data za utafiti. Hivyo mtafiti alifanikiwa kubainisha athari hasi za Ukristo kwa maendeleo ya ngoma za kijadi za kabila la Wandali kwani dhehebu la Moravian linazipiga vita na kuwakata za waumini wake kucheza ngoma hizo. Utafiti huu ulilenga kutafiti “Athari za Ukristo katika ngoma za kijadi za kabila la Wandali” huku ukijiuliza maswali kuwa: Ukristo umeathiri vipi ngoma za kijadi za kabila la Wandali? Utafiti huu ulibaini kwamba kuna matatizo mengine licha ya Ukristo yanayo kwamisha maendeleo ya ngoma za kijadi za kabila la Wandali.Matatizo hayo ni serikali ‘kutokuzijali’ ngoma za kijadi za kabila la Wandali na kuziona kama kazi ya keni kuwaburudisha wageni wao wanapotembelea vijijini, migogoro ya ndani kwandani ya vikundi vya ngoma. Migogoro hiyo mingi ni ya kimadaraka na sababu ya mwisho inayo changia kufifia na kufa kwa ngoma za kijadi za kabila la Wandali ni kuhama na kusafiri kwa vijana wengi kutoka sehemu ya Undali kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya makazi na biashara.Item Athari za ukristo katika ngoma za kijadi za kabila la Wandali(University of Dar es Salaam, 2016) Masebo, Jubeck AlinineUtafiti huu una bainisha athari za Ukristo kwa ngoma za kijadi za kabila la Wandali. Wananchi wa kata yakafulena ikingawa na chukuliwa kama kiwakilishi tu cha Wandali popote walipo katika tarafa ya Undali wilaya ya Ileje. Ilikufanikisha kupata data za utafiti huu, mtafiti alitembelea maeneo yaliyoteuliwa katika kata ya kafulena Ikinga ambayo kwa kiasi Fulani yanahusika na ngoma ya Ling; omana dhehebu la Moravian. Mbinu zilizotumika katika kupata data za utafiti huu ni mbinu ya mahojiano/ usaili, mbinu ya kushuhudia na mbinu ya ushiriki. Katika utafiti huu, nadharia ya Sosholojia ilifanikisha uchambuzi sahihi wa data za utafiti. Hivyo mtafiti alifanikiwa kubainisha athari hasi za Ukristo kwa maendeleo ya ngoma za kijadi za kabila la Wandali kwani dhehebu la Moravian linazipiga vita na kuwakata za waumini wake kucheza ngoma hizo. Utafiti huu ulilenga kutafiti “Athari za Ukristo katika ngoma za kijadi za kabila la Wandali” huku ukijiuliza maswali kuwa: Ukristo umeathiri vipi ngoma za kijadi za kabila la Wandali? Utafiti huu ulibaini kwamba kuna matatizo mengine licha ya Ukristo yanayo kwamisha maendeleo ya ngoma za kijadi za kabila la Wandali.Matatizo hayo ni serikali ‘kutokuzijali’ ngoma za kijadi za kabila la Wandali na kuziona kama kazi ya keni kuwaburudisha wageni wao wanapotembelea vijijini, migogoro ya ndani kwandani ya vikundi vya ngoma. Migogoro hiyo mingi ni ya kimadaraka na sababu ya mwisho inayo changia kufifia na kufa kwa ngoma za kijadi za kabila la Wandali ni kuhama na kusafiri kwa vijana wengi kutoka sehemu ya Undali kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya makazi na biashara.Item Atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira: uchanguzi wa ngano teule kutoka jamii ya wagogo(University of Dar es Salaam, 2019) Citungo, Mercy AbelUtafiti huu umechunguza atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji dhamira kwa kutumia ngano teule kutoka jamii ya Wagog. Data zilikusanywa tangu Mei mpaka Juni 2018 katika mkoa wa Dodoma, wilaya ya Mpwapwa katika vijiji vya Inzomvu, Tambi, Mboli na. Mlrmbule. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza athari ya vipashio vya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira.ili kutekeleza lengo hili, utafiti umeongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni kubainisha vipashio vya kisanaa vinavyojenga muundo wa ngano za jamii ya Wagogo, kuainisha miundo ya ngano za Wagogo kulungana na vipashio vya kisanaa vilivyobainishwa na kuchanganua athari vipashio vya kimuundo katika uwasilishaji wa dhamira. Kimsingi, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushiriki, mahojiano na majadala wa vikundi lengwa. Data ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ua Umuundo kama ilivyoasisiwa na Ferdnand de Saussure. Nadharia hii imejikita katika msingi mkuu unaoeleza kuwa kitu chochote kitaleta maana endapo kitakuwa na muunganiko wenye sehemu mbalimbali zenye uhusiano ili kukamilisha maana iliyokusudiwa. Utafiti huu umebaini kuwa kimuundo ngano za jamii ya Wagogo hujengwa na vipashio mbalimbali vya kisanaa hususan mianzo na miisho ya kifomula, wahisika na msuko wa matukio. Aidha, tumeibaini miundo mbalimbali ya ngano kama vile, muundo sahili, duara, rejeshi na changamano. Miundo hii katika ngano ndiyo huibua dhamira mbalimbali kulingana na aina ya muundo uliojitokeza. Halikadhalika, utafiti huu umebaini kuwa msuko wa matukio husaidia kutambulisha wahusika, mgogoro na ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira. Kutokana na matokeo hayo, utafiti huu umependekeza kuwa ipo haja ya kafasiri ngano za makabila mbalimbali katika lugha ya Kiswahili ili zisipotee. Hii inatokana na ukweli kwamba kutokana na maendeleo ya sayansi na technolojia, ngano katika jamii nyingi zina hatari ya kupotea kabisa. Aidha, mtafiti anapendekeza kufanyika kwa tafiti nyinginezo ili kufanya ulinganishi na kubainisha vipashio vya kisanaa vinavyopatikana katika ngano za jamii nyingine ili kuweza kubaini kama kuna kufanana au kutofautiana kwa vipashio hivyo.Item Breaking cultural barriers of HIV/AIDS intransigence through theatre: an examination of theatre-against-AIDS interventions in Kenya(University of Dar es Salaam, 2010) Mwita, MahiriIn the beginning of the 21st century, HIV-AIDS prevention programs declared that ‘almost everyone in Kenya knows about AIDS and how deadly it is’. However, emerging statistics continued to report rising rates of infection, presenting a new challenge that this universal awareness was not translating into decline in the spread of the disease. This intransigence has been blamed on cultural stigma that inhibits people’s openness to be associated with AIDS and its services. In the search for innovative preventions to target this stigma, theatre-against-AIDS programs have been mainstreamed into many intervention programs in Kenya. However, little academic research is available on the quality and efficacy of these programs. This research studied the process of performing the theatre-against-AIDS interventions, the stigma they target, and the immediate and long-term efficacy of the programs. The study employed an ethnographic methodology comprising of memoing, participant observation, interviews, focus-group discussions, and theme-coding as its main methods of data collection and analysis. This study established that the theatre-against-AIDS programs are successful in mobilizing people into community-based forums in which they discuss various themes on the AIDS problems. Specific achievements include enabling forums that suggest local solutions to the AIDS issues and participants of these outreaches taking the action of going to VCT centres for HIV testing. Its main challenges include lack of socio-political and economic support structures to sustain the momentum created through the outreaches.Item Changamoto katika kutafsiri dhana za kiutamaduni mifano kutoka kitabu cha mwana mdogo wa mfalme(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2013) Mkinga, SilvesterTafsiri ni njia mojawapo ya mawasiliano inayohusisha lugha zaidi ya moja. Kwa kuwa kila lugha ina utamaduni wake, tafsiri pia inahusisha tamaduni zaidi ya moja. Utafiti huu umechunguza changamoto zilizojitokeza katika kutafsiri dhana za kiutamaduni kupitia methali, misemo na istilahi mbalimbali kutoka lugha ya Kifaransa kwenda lugha ya Kiswahili, lugha ambazo zina tofauti kubwa za kiutamaduni. Utafiti huu ni utafiti usio wa kitakwimu uliofanyika maktabani. Data zimekusanywa na kuchanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa kutumia nadharia ya mawasiliano ya Ukubalifu (Relevence Theory) iliyoanzishwa na Sperber na Wilson mwaka 1986. Utafiti huu umegundua kuwa changamoto za kutafsiri methali, misemo na istilahi mbalimbali zinatokana na sababu nyingi. Miongoni mwa sababu hizo ni ugumu wa kupata visawe kutokana na tofauti za mila na desturi baina ya lugha chanzi na lugha lengwa, tofauti za kimazingira na tofauti za miundo ya tungo. Mfasiri ametumia mbinu kadhaa ili kukabiliana na changamoto hizo. Mbinu zilizotumika ni pamoja na kutumia maelezo ya ufafanuzi, kutohoa maneno, kuongeza vipengele ili kutia uzito katika matini lengwa na kutumia maneno yenye ufanano wa maana au matumizi katika lugha lengwa. Tunaamini kuwa changamoto na mbinu zilizotumika katika kukabiliana na changamoto hizo ambazo tumezijadili katika utafiti huu zitakuwa msaada kwa wafasiri na watafiti wa uwanja wa taaluma ya tafsiri katika kuboresha kazi zao.Item Changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya kiswahili nchini Tanzania.(University of Dar es Salaam, 2018) Kilapilo, VianeyMatumizi ya katuni-mnato-bubu katika kufikisha ujumbe kwa jamii yanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaana katika kusimbua ujumbe. Lengo la utafiti lilikuwa ni kuchunguza changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania. Ili kukamilisha utafiti huu, data ilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Mbinu ya uchambuzi matini ilitumika kwa kuwa iliwezesha kukusanywa kwa katuni. Mbinu ya mahojiano ilitumika uwandani na kuwezesha kupatikana kwa data kutoka kwa watoa data asilia. Aidha, nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Nadharia ya Alama ya Piece ya mwaka (1904). Misingi yake iliwezesha kubaini changamoto za kimaana zinazotokana na kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya Kiswahili. Pia sababu za kutokea kwa changamoto hizo zimebainika na kujadiliwa katika ripoti hii ya utafiti. Kimsingi utafiti umebaini kuwa katuni zina maana na zinabeba ujumbe. Pia, utafiti umebaini kuwa, kuna changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni. Baadhi ya changamoto hizo ni: kuwapo kwa mkanganyiko wa kimaana, kushindwa kuhusisha matukio katika safu za katuni, kushindwa kusimbua alama ili kujenga maana, na kupotoshwa kwa ujumbe uliokusudiwa na nyingine zilizojadiliwa. Changamoto hizo zinasababishwa na uzoefu wa kimaisha, mtazamo wa mtu au jamii, mila na desturi za jamii, eneo la kijiografia, itikadi zilizopo katika jamii na nyingine zilizojadiliwa. Mwisho, mtafiti anatoa mapendekezo kuwa kuna haja ya kufanya tafiti nyingine kubaini changamoto za kimaana zinazojitokeza katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato za aina nyingine na mambo mengine mbalimbali yanayohusu katuni kwa ujumla.Item Changamoto za kutumia kamusi katika ujifunzaji na ufundishaji kiswahili kwa wasioona: Mifano kutoka shule za msingi na Sekondari mkoa ni Iringa, Tanzania(University of Dar es Salaam, 2016) Amon, JoyceUtafiti huu umelenga kuchunguza, na kufafanua changamoto za matumizi ya kamusi katika ujifunzaji na ufundishaji wa Kiswahili kwa wasioona. Utafiti huu unachungu za zaidi na mnawanafunzi wasioona wanavyoweza kutumia kamusi katika maana za maneno na matumizi yake, tahaji na alama zinazotumika katika kamusi. Katika utafiti huu tumetumia hojaji pamoja na dodoso kupata data kutoka uwandani, ambapo watoa taarifa 40 kutoka shule ya Msingi Mwaya na shule ya sekondari Lugalo walishirikishwa. Nadharia iliyotuongoza katika uchanganuzi wa data ni Nadharia ya Mwenendo wakiam shina mwitiko ambayo msingi wake mkuu ni jinsi za na mbinu zinavyoweza kuhamasisha tabia ya kujifunza lugha ya animotisha ndiyo kiini cha kujifunza na kufundisha. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa, hakuna kamusi zilizo katika maandishi ya nukta nundu zinazo wawezesha wanafunzi wasioona kuweza kujifunza maana za maneno na matumizi ya kisarufi katika kamusi za Kiswahili sanifu. Hali hii inasababisa kushindwa kujifunza matumizi ya kamusiza Kiswahili kwaufanisi. Kwahiyo, ilikupunguza changamoto hizo ni vema wadau wa uchapishaji wakamusi za Kiswahili sanifu kuandaa kamusi zenye maandishi ya nukta nundu. Aidha, utafiti huu unatoa mchango mkubwa katika taaluma ya Leksikolojia katika kujua umuhimu wakutengeneza kamusiya Kiswahili Sanifu kwa kutumia maandishi ya nukta nundu na kutambua ukubwa wasoko la kamusi hizo kwa watumiaji wake.Item Changamoto za ufafanuzi wa maana za nomino za pekee katika kamusi za kiswahili: uchambuzi wa majina ya siku za wiki(University of Dar es Salaam, 2020) Nzala, Mayolwa JohnUtafiti huu ulilenga kuchunguza changamoto za ufafanuzi wa maana za Nomino za Pekee kwenye majina ya siku za wild katika kamusi za Kiswahili. Majina ya siku za wild yaliyokuwa yakichunguzwa kwenye utafiti huu ni Ijumaa, Jumapili, Alhamisi,Jumanne, Jumamosi, Jumatatu na Jumatano. Lengo kuu la utafiti huu liligawanywa katika malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha maana za majina ya siku za wild, kupambanua changamoto za kimaana kwenye majina hayo pamoja na kudabiri sababuza kuwapo kwa maana tofautitofauti na changamoto hizo za kimaana. Data zilikusanywa kutoka manispaa mbili za jiji la Dar es Salaam, ambazo ni Kinondoni na Ubungo. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni uchambuzi wa matini, hojaji pamoja na usaili.Nadharia Sababishi ya Urejelezi ya Kripke (2013) ndiyo iliyotumika katika uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Sambamba na nadharia hiyo, uchanganuzi wa data ulitumia mikabala miwili; mkabala wa kitaamuli na mkabala wa kiidadi. Aidha, mikabala yote hiiilitumia mbinu ya uchanganuzi mada wa data. Data za utafiti huu zilionesha kuwa, tofauti na Alhamisi na Ijumaa yaliyotoholewa kutoka lugha ya Kiarabu, majina mengine ya siku za wild katika lugha ya Kiswahili kwa asili yalitokana na muunganiko wa nenola Kiarabu `juma' lenye maana ya `wiki' katika lugha ya Kiswahili na nambakadinali za Kibantu, mosi, pili, tatu hadi tano ndipo tukawa na majina ya Jumamosi, Jumapili hadi Jumatano (Kihore, 1997). Hata hivyo ilibainika kuwa, licha ya mpishano wa kimaanauliopo miongoni mwa kamusi teule za Kiswahili na miongoni mwa wazungumzaji wake, maana za majina ya siku za wild zilizoko kwenye kamusi zilionekana kupishana na maana zilizotolewa na watumiaji wa lugha hiyo. Msingi wa maelezo haya ulitokana na malengo ya utafiti ambayo yalibainisha kuwa katika lugha ya Kiswahili, majina ya siku za wild yamefasiliwa kwa maana zisizopungua tatu. Hii ina maana kwamba, kila jina la siku ya wild lina fasili tofauti zisizopungua tatu. Aidha, ilibainika kuwa, changamoto za kimaana kwenye majina ya siku za wiki zinatokana na mpishano wa fafanuzi za majina hayo kwenye machapisho ya kamusi pamoja na fasili za watumiaji wenyewe wa lugha ya Kiswahili. Sababu za kuwapo kwa half hii zimekuwa ni uhesabuji wa siku za wiki kwa mtazamo wa kidini, uhesabuji wa siku wa wiki kiserikali, kufasili maana za majina ya siku bila kuzingatia kanuni za kiisimu na ukosefu wa istilahi maalumu za kuyaita majina ya siku za wild katika lugha ya Kiswahili. Sababu zingine mbalimbali zilitolewa na watoataarifa. Sababu hizo zilikuwa ni mwingiliano wa tamaduni za kigeni katika jamii ya Waswahili, uigaji wa mpangilio wa siku za wiki za mataifa mengine duniani, athari za mfumo wa kalenda wa nchi za Magharibi katika Kiswahili pamoja na kuwapo kwa taratibu kubalifu za kikalenda kutoka nchi zilizoendelea. Kutokana na mkanganyiko wa kimaana unaoukiliwa na sababu hizo, utafiti huu umependekeza mtazamo unaofaa kutumika katika kuzifasili NP hususani majina ya siku za wiki katika lugha ya Kiswahili.Item Changamoto zinazowakabili wanafunzi wa sekondari wanapotafsiri kutoka kiingereza hadi Kiswahili(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2017) Ninsiima, BettyUtafiti huu kuhusu Changamoto zinazowakabili wanafunzi wa sekondari nchini Uganda wanapotafsirimatinikutokaKiingerezahadiKiswahiliunakusudiwakupunguzachangamotozakutafsirimatinikutokaKiingerezahadiKiswahili. Utafitiulikuwanamalengomawiliyafuatayo: Kwanza, kubainisha changamoto zinazowakabili wanafunzi wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Lengo la pili lilikuwa kuchunguza chanzo cha changamoto zinazowakabili wanafunzi wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Kutokana na uchunguzi watoa tarifa walitoa mapendekezo na mikakati ya kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili, ambalo ni lengo la tatu. Katika utafiti huu, mtafiti alitumia hojaji na mahojiano kukusanya data aliyotumia kujibu maswali yake ya utafiti. Ufafanuziwa data na matokeo ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kiidadi. Nadharia ya Ulinganifu Matini ndio iliyotumika katika utafitihuu. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kwamba kuna changamoto nyingi katika kutafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili kwa wanafunzi wasekondari. Uchunguzi unaonyesha kwamba kuna changamoto ya kukosa msamiati wa kutumia wakati wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili, ukosefu wa vitabu vya kutosha vya kutumia, athari za lugha mama na kadhalika. Mikakati mingi ilipendekezwa kupunguza changamoto hizi. Mapendekezo ya Wanafunzi: vitabu vinavyofaavya Kiswahili viwekwe kwenye maktaba, walimu wa Kiswahili wasahihishe kazi zao kila wakati ili waweze kuwarekebisha wanaposhindwa, Kiswahili kama Kiingereza kifundishwe kuanzia shule za msingi, nawanafunzi wanaofaulu kutunukiwa. Walimu pia walipendekeza yafuatayo: kuwepo sera nzuri zinazoeleweka na kuianzisha lugha hii ya Kiswahili katika shule na vipimo viwekwe ili wanafunzi wapunguze utumiaji wa lugha za mitaani na zakienyeji, wapate kozi za kukuza lugha, vipindi vya Kiswahili darasani viongezwe, serikali iwaajiri walimu wa Kiswahili wakutosha na kutoaf edha za kununua vitabu vinavyofaa na vifaa vingine vya kujifunza na kufundishia lugha ya Kiswahili, kunahitajika programu za ufundishaji wa walimu wa Kiswahili ambazo zitawachangamsha na kuleta nguvu mpya na kutengeneza upya mielekeo mipya katika ujifunzaji na utafsiri wa matini za Kiingereza kwenda Kiswahili kwa jumla. Pia, walimuwa Kiswahili wanapaswa kupanua mbinu za kufundisha na kuchangamsha masomo yao ili yapendeze kwa wanafunzi wao. Majukumu ya Serikali: inastahili kuifanya Kiswahili lugha rasmi ya pili ya nchi ili kila Mganda aongee lugha hii jambo ambalo litawasaidia wanafunzi kupanua msamiati katika lugha. Wizara ya Elimu ikuze na kuweka katika mtalaa wa nchi silabasi ya kuanzisha na kufundisha Kiswahili kuanzia shule za msingi.Item Chanzo na suluhisho la matatizo ya uandishi wa Kiswahili katika sekondari za Tanzania : mifano kutoka kidato cha tano katika mkoa wa Dar es Salaam(University of Dar es Slaam, 2011) Ndossi, Ndeni AsseryChanzo na suluhisho la matatizo ya uandishi wa Kiswahili katika sekondari za Tanzania : mifano kutoka kidato cha tano katika mkoa wa Dar es Salaam