Athari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzo

Date

2014

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu unahusu Athari za matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo, uliofanyika katika mkoa wa Mara manispaa ya Musoma katika kata za Mwisenge, Iringo, Mkendo, Nyakato na Kamnyonge. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 40 ambapo wanawake walikuwa 20 na wanaume walikuwa 20, vilevile kila kata ilitoa watafitiwa 8. Utafiti huu ulilenga kwanza kubaini matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Pili, kubainisha makundi ya jamii yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa kuzingatia jinsi, umri na kiwango cha elimu. Tatu, kueleza sababu za kutumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo.Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha wazi kuwa kuna baadhi ya matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Matamshi hayo ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo hutokana na matumizi ya mara kwa mara ya lugha ya Kikwaya, kutopata elimu na kutumia lugha mbili au zaidi katika eneo moja. Utafiti huu pia umedhihirisha makundi ya jamii ya watafitiwa yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo. Makundi hayo mtafiti ameyagawa katika sehemu mbili, yaani kuna makundi ya watafitiwa wanaotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa wingi, na kuna makundi ya watafitiwa wasiotumia sana matamshi ya Kikwaya. Makundi yanayotumia sana matamshi ya Kikwaya ni wazee (72%), wakulima (74%), wasiosoma (72%), wanawake (70%) na wafanyabiashara (60%). Hali kadhalika makundi ya watafitiwa yasiyotumia sana matamshi ya Kikwaya ni vijana (39%),waliosoma shule (48%), wanaume (52%) na wafanyakazi (45%).

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8295.4.M34)

Keywords

Mara, Tanzania (Region), Language, Bantu languages, Swahili language, Kwaya language

Citation

Malindi, B (2014) Athari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzo,Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.