Changamoto katika kutafsiri dhana za kiutamaduni mifano kutoka kitabu cha mwana mdogo wa mfalme
No Thumbnail Available
Date
2013
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Tafsiri ni njia mojawapo ya mawasiliano inayohusisha lugha zaidi ya moja. Kwa kuwa kila
lugha ina utamaduni wake, tafsiri pia inahusisha tamaduni zaidi ya moja. Utafiti huu
umechunguza changamoto zilizojitokeza katika kutafsiri dhana za kiutamaduni kupitia
methali, misemo na istilahi mbalimbali kutoka lugha ya Kifaransa kwenda lugha ya
Kiswahili, lugha ambazo zina tofauti kubwa za kiutamaduni. Utafiti huu ni utafiti usio wa
kitakwimu uliofanyika maktabani. Data zimekusanywa na kuchanganuliwa kwa njia ya
maelezo kwa kutumia nadharia ya mawasiliano ya Ukubalifu (Relevence Theory)
iliyoanzishwa na Sperber na Wilson mwaka 1986. Utafiti huu umegundua kuwa changamoto za kutafsiri methali, misemo na istilahi
mbalimbali zinatokana na sababu nyingi. Miongoni mwa sababu hizo ni ugumu wa kupata
visawe kutokana na tofauti za mila na desturi baina ya lugha chanzi na lugha lengwa, tofauti
za kimazingira na tofauti za miundo ya tungo. Mfasiri ametumia mbinu kadhaa ili
kukabiliana na changamoto hizo. Mbinu zilizotumika ni pamoja na kutumia maelezo ya
ufafanuzi, kutohoa maneno, kuongeza vipengele ili kutia uzito katika matini lengwa na
kutumia maneno yenye ufanano wa maana au matumizi katika lugha lengwa.
Tunaamini kuwa changamoto na mbinu zilizotumika katika kukabiliana na changamoto hizo
ambazo tumezijadili katika utafiti huu zitakuwa msaada kwa wafasiri na watafiti wa uwanja
wa taaluma ya tafsiri katika kuboresha kazi zao.
Description
Keywords
Swahili language, Mwana Mdogo wa Mfalme
Citation
Mkinga, S (2013) Changamoto katika kutafsiri dhana za kiutamaduni mifano kutoka kitabu cha mwana mdogo wa mfalme, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)