Changamoto za ufafanuzi wa maana za nomino za pekee katika kamusi za kiswahili: uchambuzi wa majina ya siku za wiki
Loading...
Date
2020
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza changamoto za ufafanuzi wa maana za Nomino za Pekee kwenye majina ya siku za wild katika kamusi za Kiswahili. Majina ya siku za wild yaliyokuwa yakichunguzwa kwenye utafiti huu ni Ijumaa, Jumapili, Alhamisi,Jumanne, Jumamosi, Jumatatu na Jumatano. Lengo kuu la utafiti huu liligawanywa katika malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha maana za majina ya siku za wild, kupambanua changamoto za kimaana kwenye majina hayo pamoja na kudabiri sababuza kuwapo kwa maana tofautitofauti na changamoto hizo za kimaana. Data zilikusanywa kutoka manispaa mbili za jiji la Dar es Salaam, ambazo ni Kinondoni na Ubungo. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni uchambuzi wa matini, hojaji pamoja na usaili.Nadharia Sababishi ya Urejelezi ya Kripke (2013) ndiyo iliyotumika katika uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Sambamba na nadharia hiyo, uchanganuzi wa data ulitumia mikabala miwili; mkabala wa kitaamuli na mkabala wa kiidadi. Aidha, mikabala yote hiiilitumia mbinu ya uchanganuzi mada wa data. Data za utafiti huu zilionesha kuwa, tofauti na Alhamisi na Ijumaa yaliyotoholewa kutoka lugha ya Kiarabu, majina mengine ya siku za wild katika lugha ya Kiswahili kwa asili yalitokana na muunganiko wa nenola Kiarabu `juma' lenye maana ya `wiki' katika lugha ya Kiswahili na nambakadinali za Kibantu, mosi, pili, tatu hadi tano ndipo tukawa na majina ya Jumamosi, Jumapili hadi Jumatano (Kihore, 1997). Hata hivyo ilibainika kuwa, licha ya mpishano wa kimaanauliopo miongoni mwa kamusi teule za Kiswahili na miongoni mwa wazungumzaji wake, maana za majina ya siku za wild zilizoko kwenye kamusi zilionekana kupishana na maana zilizotolewa na watumiaji wa lugha hiyo. Msingi wa maelezo haya ulitokana na malengo ya utafiti ambayo yalibainisha kuwa katika lugha ya Kiswahili, majina ya siku za wild yamefasiliwa kwa maana zisizopungua tatu. Hii ina maana kwamba, kila jina la siku ya wild lina fasili tofauti zisizopungua tatu. Aidha, ilibainika kuwa, changamoto za kimaana kwenye majina ya siku za wiki zinatokana na mpishano wa fafanuzi za majina hayo kwenye machapisho ya kamusi pamoja na fasili za watumiaji wenyewe wa lugha ya Kiswahili. Sababu za kuwapo kwa half hii zimekuwa ni uhesabuji wa siku za wiki kwa mtazamo wa kidini, uhesabuji wa siku wa wiki kiserikali, kufasili maana za majina ya siku bila kuzingatia kanuni za kiisimu na ukosefu wa istilahi maalumu za kuyaita majina ya siku za wild katika lugha ya Kiswahili. Sababu zingine mbalimbali zilitolewa na watoataarifa. Sababu hizo zilikuwa ni mwingiliano wa tamaduni za kigeni katika jamii ya Waswahili, uigaji wa mpangilio wa siku za wiki za mataifa mengine duniani, athari za mfumo wa kalenda wa nchi za Magharibi katika Kiswahili pamoja na kuwapo kwa taratibu kubalifu za kikalenda kutoka nchi zilizoendelea. Kutokana na mkanganyiko wa kimaana unaoukiliwa na sababu hizo, utafiti huu umependekeza mtazamo unaofaa kutumika katika kuzifasili NP hususani majina ya siku za wiki katika lugha ya Kiswahili.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8701.T34N924)
Keywords
Swahili language, Noun, Dictionaries, Tanzania
Citation
Nzala, Mayolwa John (2020) Changamoto za ufafanuzi wa maana za nomino za pekee katika kamusi za kiswahili: uchambuzi wa majina ya siku za wiki,Tasnifu ya Shahada ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam