Athari za ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa
No Thumbnail Available
Date
2012
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu Athari za Ukopaji wa Msamiati wa Kiswahili katika Lugha ya Kinyakyusa. Utafiti umefanyika nyanda za juu Kusini katika mkoa wa Mbeya wilayani Kyela katika kata nne za Kyela Mjini, Ikolo, Bujonde na Kajunjumele. Utafiti umehusisha mbinu kuu mbili za ukusanyaji wa data. Mbinu hizo ni usaili na ushuhudiaji. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa umeathiri msamiati wa lugha ya Kinyakyusa kifonolojia, kileksika, kimofolojia na kisemantiki. Ukopaji wa msamiati unatokana na sababu tofautitofauti: fahari na hadhi inayoambatana na lugha chanzi, kutaja vitu na dhana mpya ambavyo hapo awali havikuwapo katika lugha pokezi, kupanua maana za maneno na kuondoa utata. Aidha, maneno ya mkopo huenda sambamba na michakato ya uingizaji katika lugha pokezi kama vile ubadilishaji wa sauti, usilimishaji wa sauti, uchopekaji wa konsonanti na irabu na uingizaji wa nomino katika ngeli za majina. Pia, utafiti ulibaini athari za ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa, nazo ni: athari za kifonolojia, kileksika, kimofolojia na kisemantiki. Ukopaji wa msamiati mpya kutoka lugha ya Kiswahili katika Kinyakyusa umesababisha uongezekaji wa sauti mpya. Hivyo basi, ipo haja ya kuchunguza idadi ya sauti hizo katika lugha ya Kinyakyusa.
Description
Keywords
Nyakyusa language, Swahili language
Citation
Katuma, R (2012) Athari za ukopaji wa msamiati wa Kiswahili katika Kinyakyusa, Tasinifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Kinapatikana http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)