Atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira: uchanguzi wa ngano teule kutoka jamii ya wagogo

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji dhamira kwa kutumia ngano teule kutoka jamii ya Wagog. Data zilikusanywa tangu Mei mpaka Juni 2018 katika mkoa wa Dodoma, wilaya ya Mpwapwa katika vijiji vya Inzomvu, Tambi, Mboli na. Mlrmbule. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza athari ya vipashio vya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira.ili kutekeleza lengo hili, utafiti umeongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni kubainisha vipashio vya kisanaa vinavyojenga muundo wa ngano za jamii ya Wagogo, kuainisha miundo ya ngano za Wagogo kulungana na vipashio vya kisanaa vilivyobainishwa na kuchanganua athari vipashio vya kimuundo katika uwasilishaji wa dhamira. Kimsingi, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushiriki, mahojiano na majadala wa vikundi lengwa. Data ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ua Umuundo kama ilivyoasisiwa na Ferdnand de Saussure. Nadharia hii imejikita katika msingi mkuu unaoeleza kuwa kitu chochote kitaleta maana endapo kitakuwa na muunganiko wenye sehemu mbalimbali zenye uhusiano ili kukamilisha maana iliyokusudiwa. Utafiti huu umebaini kuwa kimuundo ngano za jamii ya Wagogo hujengwa na vipashio mbalimbali vya kisanaa hususan mianzo na miisho ya kifomula, wahisika na msuko wa matukio. Aidha, tumeibaini miundo mbalimbali ya ngano kama vile, muundo sahili, duara, rejeshi na changamano. Miundo hii katika ngano ndiyo huibua dhamira mbalimbali kulingana na aina ya muundo uliojitokeza. Halikadhalika, utafiti huu umebaini kuwa msuko wa matukio husaidia kutambulisha wahusika, mgogoro na ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira. Kutokana na matokeo hayo, utafiti huu umependekeza kuwa ipo haja ya kafasiri ngano za makabila mbalimbali katika lugha ya Kiswahili ili zisipotee. Hii inatokana na ukweli kwamba kutokana na maendeleo ya sayansi na technolojia, ngano katika jamii nyingi zina hatari ya kupotea kabisa. Aidha, mtafiti anapendekeza kufanyika kwa tafiti nyinginezo ili kufanya ulinganishi na kubainisha vipashio vya kisanaa vinavyopatikana katika ngano za jamii nyingine ili kuweza kubaini kama kuna kufanana au kutofautiana kwa vipashio hivyo.
Description
Available in print form, Dr. Wilbert Chagula Library. East Africana Collection, (THS EAF PL8703.C578)
Keywords
Swahili literature, Folk literature, Theme, Style
Citation
Citungo, M.A. (2019). Atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira: uchanguzi wa ngano teule kutoka jamii ya wagogo. Masters dissertation. University of Dar es Salaam. Dar es Salaam