Changamoto zinazowakabili wanafunzi wa sekondari wanapotafsiri kutoka kiingereza hadi Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu kuhusu Changamoto zinazowakabili wanafunzi wa sekondari nchini Uganda wanapotafsirimatinikutokaKiingerezahadiKiswahiliunakusudiwakupunguzachangamotozakutafsirimatinikutokaKiingerezahadiKiswahili. Utafitiulikuwanamalengomawiliyafuatayo: Kwanza, kubainisha changamoto zinazowakabili wanafunzi wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Lengo la pili lilikuwa kuchunguza chanzo cha changamoto zinazowakabili wanafunzi wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Kutokana na uchunguzi watoa tarifa walitoa mapendekezo na mikakati ya kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili, ambalo ni lengo la tatu. Katika utafiti huu, mtafiti alitumia hojaji na mahojiano kukusanya data aliyotumia kujibu maswali yake ya utafiti. Ufafanuziwa data na matokeo ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kiidadi. Nadharia ya Ulinganifu Matini ndio iliyotumika katika utafitihuu. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kwamba kuna changamoto nyingi katika kutafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili kwa wanafunzi wasekondari. Uchunguzi unaonyesha kwamba kuna changamoto ya kukosa msamiati wa kutumia wakati wanapotafsiri matini kutoka Kiingereza hadi Kiswahili, ukosefu wa vitabu vya kutosha vya kutumia, athari za lugha mama na kadhalika. Mikakati mingi ilipendekezwa kupunguza changamoto hizi. Mapendekezo ya Wanafunzi: vitabu vinavyofaavya Kiswahili viwekwe kwenye maktaba, walimu wa Kiswahili wasahihishe kazi zao kila wakati ili waweze kuwarekebisha wanaposhindwa, Kiswahili kama Kiingereza kifundishwe kuanzia shule za msingi, nawanafunzi wanaofaulu kutunukiwa. Walimu pia walipendekeza yafuatayo: kuwepo sera nzuri zinazoeleweka na kuianzisha lugha hii ya Kiswahili katika shule na vipimo viwekwe ili wanafunzi wapunguze utumiaji wa lugha za mitaani na zakienyeji, wapate kozi za kukuza lugha, vipindi vya Kiswahili darasani viongezwe, serikali iwaajiri walimu wa Kiswahili wakutosha na kutoaf edha za kununua vitabu vinavyofaa na vifaa vingine vya kujifunza na kufundishia lugha ya Kiswahili, kunahitajika programu za ufundishaji wa walimu wa Kiswahili ambazo zitawachangamsha na kuleta nguvu mpya na kutengeneza upya mielekeo mipya katika ujifunzaji na utafsiri wa matini za Kiingereza kwenda Kiswahili kwa jumla. Pia, walimuwa Kiswahili wanapaswa kupanua mbinu za kufundisha na kuchangamsha masomo yao ili yapendeze kwa wanafunzi wao. Majukumu ya Serikali: inastahili kuifanya Kiswahili lugha rasmi ya pili ya nchi ili kila Mganda aongee lugha hii jambo ambalo litawasaidia wanafunzi kupanua msamiati katika lugha. Wizara ya Elimu ikuze na kuweka katika mtalaa wa nchi silabasi ya kuanzisha na kufundisha Kiswahili kuanzia shule za msingi.
Description
Inapatikana maktaba ya Dkt Wilber Chagula, East Africana klasimaki (THS EAF PE1498.2.S8N56)
Keywords
Changamoto, wanafunzi, kiingereza
Citation
Ninsiima, B. (2017) Changamoto zinazowakabili wanafunzi wa sekondari wanapotafsiri kutoka kiingereza hadi Kiswahili. Shahada ya Uzamli, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.