Masters Dissertations

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 320
 • Item
  Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na kindali Hassan Musa Tasnifu ya (Kiswahili) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi Ya Taaluma ya Kiswahili, 2019 Lugha ina miundo mbalimbali, miundo mingine ina upekee na umuhimu fulan. Kwa hiyo, miundo hiyo huvuta udadisi haraka. Moja ya miundo hiyo ni vishazi rejeshi ambavyo vina mwigo mpana katika lugha za kibantu kwa vile vishazi hivi ndivyo vyenye kutumika mara nyingi zaidi kukumusha nomino. Vivumishi katika lugha za kibantu ni vichache kwa vile kazi za vivumishi hufanywa na vishazi rejeshi, kwa hiyo, urejeshi ni muundo muhimu katika lugha hizi. Utafiti huu unahusu “Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na Kindali” utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sarufi Geuzi ya Chomsky (1965) utafiti huu ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika mkoa wa Dar es salaam na Bundali katika wilaya ya Ileje Mkoani Songwe. Data ya utafiti huu ilikusanywa maktabani na uwandani kwa njia ya hojaji, mahojiano na kusoma na kuchambua matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba vishazi rejeshi katika Kiswahili na kindali vinafanana katika matumizi na kutofautiana katika baadhi ya miundo. Muundo wa kishazi rejeshi unatofautiana katika lugha hizi katika idadi ya miundo na mumbo la kiwakilishi rejeshi. Kiswahili kina miundo mitatu wakati kindali kina muundo mmoja wa kishazi rejeshi kwa kuzingatia kiwakilishi rejeshi kinapachikwa wapi. Hata hivyo, kiwakilishi rejeshi katika kiwahili ni mofimu tegemezi wakati katika Kindali kiwakilishi rejeshi ni mofimu huru. Muundo wa Kishazi rejeshi kutokea baada ya neno kuu kutangulia unafanana katika lugha hizi. Vilevile matumizi ya kishazi rejeshi katika lugha hizo yanafanana katika ukumushi bainifu, ukumushi ziada na uelezi wa namna na mahali. Utafiti huu umeonesha masharti na michakato ambayo kishazi rejeshi hupitia katika uundaji wake. Masharti hayo ni kuwepo kwa vishazi huru viwili vyenye uzito sawa, vishazi hivyo sharti niwe na nomino zenye kurejelea kitu kilekile na sharti la tatu ni kukishusha hadhi kishazi huru kimoja. Sharti la kushusha hadhi kishazi huru kimoja linafungamana na michakato ya udondoshaji, uwakilishi na urejeshi, uchopekaji, utegemezaji, uhamishaji na kubadilishana nafasi. Maeneo mengine yanayopendekezwa kufanyiwa utafiti ni katika aina zingine za vishazi tegemezi.
  (Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2019) Musa, H
  Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na kindali Hassan Musa Tasnifu ya (Kiswahili) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi Ya Taaluma ya Kiswahili, 2019 Lugha ina miundo mbalimbali, miundo mingine ina upekee na umuhimu fulan. Kwa hiyo, miundo hiyo huvuta udadisi haraka. Moja ya miundo hiyo ni vishazi rejeshi ambavyo vina mwigo mpana katika lugha za kibantu kwa vile vishazi hivi ndivyo vyenye kutumika mara nyingi zaidi kukumusha nomino. Vivumishi katika lugha za kibantu ni vichache kwa vile kazi za vivumishi hufanywa na vishazi rejeshi, kwa hiyo, urejeshi ni muundo muhimu katika lugha hizi. Utafiti huu unahusu “Muundo na matumizi ya kishazi rejeshi: uchunguzi linganishi kati ya Kiswahili na Kindali” utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sarufi Geuzi ya Chomsky (1965) utafiti huu ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika mkoa wa Dar es salaam na Bundali katika wilaya ya Ileje Mkoani Songwe. Data ya utafiti huu ilikusanywa maktabani na uwandani kwa njia ya hojaji, mahojiano na kusoma na kuchambua matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba vishazi rejeshi katika Kiswahili na kindali vinafanana katika matumizi na kutofautiana katika baadhi ya miundo. Muundo wa kishazi rejeshi unatofautiana katika lugha hizi katika idadi ya miundo na mumbo la kiwakilishi rejeshi. Kiswahili kina miundo mitatu wakati kindali kina muundo mmoja wa kishazi rejeshi kwa kuzingatia kiwakilishi rejeshi kinapachikwa wapi. Hata hivyo, kiwakilishi rejeshi katika kiwahili ni mofimu tegemezi wakati katika Kindali kiwakilishi rejeshi ni mofimu huru. Muundo wa Kishazi rejeshi kutokea baada ya neno kuu kutangulia unafanana katika lugha hizi. Vilevile matumizi ya kishazi rejeshi katika lugha hizo yanafanana katika ukumushi bainifu, ukumushi ziada na uelezi wa namna na mahali. Utafiti huu umeonesha masharti na michakato ambayo kishazi rejeshi hupitia katika uundaji wake. Masharti hayo ni kuwepo kwa vishazi huru viwili vyenye uzito sawa, vishazi hivyo sharti niwe na nomino zenye kurejelea kitu kilekile na sharti la tatu ni kukishusha hadhi kishazi huru kimoja. Sharti la kushusha hadhi kishazi huru kimoja linafungamana na michakato ya udondoshaji, uwakilishi na urejeshi, uchopekaji, utegemezaji, uhamishaji na kubadilishana nafasi. Maeneo mengine yanayopendekezwa kufanyiwa utafiti ni katika aina zingine za vishazi tegemezi.
 • Item
  Utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi
  (University of Dar es salaam, 2020) Jasson, Tasiana
  Utafiti huu umechunguza utokeaji wa kimbishi tangulizi katika lugha ya Kiswahili. Lengo lilikuwa ni kuweka bayana maumbo na mazingira ya utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha hiyo. Data ya utafiti huu ulikusanywa uwandani katika eneo la kata ya Nyaruhungo iliyopo wilayani Biharamuro, Mkoani Kagera. Mbinu ya hojaji na majadiliano ya vikundi lengwa zilitumika kukusanya data ya utafiti huu ulichambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu ya uchambuzi wa data kimaudhui ilitumika.Nadharia ya Utangamano wa mfuatano wa mofimu ya McCalthy na princes (1995) imetumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kiambishi tangulizi katika lugha tya kisubi kina maumbo sahili, yaani; maumbo ya irabu pekee. Maumbo hayo ni [a,e, i,o]. Aidha imebadilika kuwa maumbo hayo hutokea katika mazingira maluum ambayo ni bainifu. Mazingira hayo ni ya kategolia bainifu za maneno ya lugha hiyo zikiwa pwekepweke. Kulingana na utafiti huu kategolia hizo ni nomino, kivumishi, kielezi na kibainishi.Hata hivyo, kuna vighairi vichache vya kategolia hizo visivyokuwa na kiambishi tangulizi, hususan vivumishi viulizi na nomino zinazotaja majina ya ndugu kama vile maha (mama), kaaka (bibi) guuku (babu). Aidha ,imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliopo kwenye kiima au kiarifu cha tungo hatakama tungo hiyo ina ukanushi , taarifa au masharti. Pia, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika kielezi kinapoandamana na kitenzi katika tungo.Kadhalika,imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kabla ya kibainishi kioneshi. Zaidi ya hayo, imebainilka kuwa kiambishi tangulizi hakitokei katika nomino iliyopo baadaya kibainishi kioneshi. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea kwenye kivumishi cha pekee kinachotanguliwa na nomino. Pia, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyotanguliwa na kihusishi nomino ya uhusika milikishi na nomino iliotanguliwa na kiunganishi huru.Utokeaji huo hutokana na michakato udondoshaji, uunganishaji ua urefushaji wa irabu ya kihusishi, irabu ya kimilikishi au kiunganishi huru kilichotangulia nomino husika. Kwa hiyo, utafiti huu umebaini kuwa bazingira ya kimofolojia na kisintaksia ndiyo huamua kutokea au kutokutokea kwa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi .Aidha utafiti huu umependekeza utafiti mwingine ufanyike katika kipengele cha ulinganishi wa ruwaza za utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha mbalimbali za kibantu au zisizo za kibantu.
 • Item
  Muundo na dhima za vibainishi vioneshi katika kiswahili sanifu.
  (University of Dar es salaam, 2019) Champunga, Shaibu Issa
  Utafitti huu ulinuia kuchunguza vibainishi vioneshi katika lugha ya Kiswahili ili kubaini muundo na dhima za vibainishi hivyo. Lengo hasa ilikuwa ni kujaribu kuondoa ukinzani wa hoja uliopo katika kuchanganua muundo na kudhukuru dhima za vibainishi vioneshi vioneshi ambapo mara nyingi wataalam huelezea dhima moja ya vibainishi ambayo nikuonesha msaafa ya ukaribu au umbali. Data za utafiti huu zilikusanywa maktabani kutoka katika matini za vitabu vya kichwamaji (kezilabai, 1974) na kivuli kinaishi (Mohamed,1990) Mbinu iliyotumika ni usomaji wa maandiko na kunukuu madondoo yanayohusiana na muundo na dhima za vibainishi vioneshi. Data hizo zilichambuliwa kwa mbinu ya maelezo. Nadharia ya mofolojia leksika iliyoasisiwa na Kiparsky (1982 ) ilitumika. kwa muhtasari, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba kuna miundo mitatu ya vibainishi vioneshi. Kwanza, kuna vibainishi vioneshi vya karibu na mzungumzaji vinavyoundwa na mzizi (h-) unaofuatiliwa na irabu iliyonakiliwa kutoka katika kiambishi ngeli cha kibainishi kinachohusika. Pili, kuna vibainishi viambishi vioneshi vya mbali na mzungumzaji ambavyo hutawaliwa na mzizi (h-) unaofuatiliwa na irabu ya kiambishi ngeli na kiambishi rejeshi (-0) mwishoni mwa vibainishi hivyo. Tatu, kuna vibainishi vioneshi vya mbali na mzungumzaji na msikilizaji, ambavyo huundwa na mzizi (-le) unaojitokeza mwishoni mwa kibainishi kinachohusika, ukitanguliwa na viambishi ngeli. Ama kuhusu dhima zilizobainishwa, ipo dhima ya kuonesha mahali ,dhima ya uhimizaji, msisitizo, kuuganisha, kuonesha umbali au ukaribu wa kitu na kuonesha mahali. Utafiti huu unapendekeza kwamba, utafiti mwingine kama huu unaweza kufanyika katika aina nyingine za vibainishi ili kupata maarifa majumui kuhusu muundo na dhima za vibainishi hivyo katika lugha ya Kiswahili, pia utafiti unaweza kufanywa kuchunguza muundo na dhima za vibainishi katika lugha mbalimbali za Kibantu ili kuona namna miundo na dhima zinavyoweza kutofautiana na/au kufanana na lugha ya Kiswahili.
 • Item
  Uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili Mifano kutoka mbazi teule za kiha
  (University of Dar es salaam, 2019) Nzababa, David Edward
  Utafiti huu ulilenga kuchunguza uainishaji wa mbazi katika fasihi simulizi ya Kiswahili ukitumia mifano kutoka mbazi teule za Kiha .Lengo kuu la utafiti huu ilikuwa kuchunguza nafasi ya kigezo cha nduni bainifu katika uainishaji wa mbazi za kiha na fasihi simulizi ya Kiswahili kwa ujumla. Aidha malengo mahususi yalikuwa (i)Kupambanua nduni bainifu zinazojenga ujumi wa mbazi za Kiha (ii)Kuainisha mbazi za Kiha katika tanzu vipare na kumbo mahususi kulingana na nduni zake bainifu na(iii) kuonesha nafasi ya kigezo cha nduni bainifu kaika uainishaji wa mbazi za Kiha na fasihi simulizi ya kiswahili kwa ujumla.Data hizo zilichambuliwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Tanzu iliyoasisiwa na wanafalsafa wa Kigiriki hususani plato na Aristotle.Isitoshe data hizo zilichambuliwa na mihimili miwili ya nadharia hii yaani mhimili wa nduni bainifu na mhimili wa kijamii.Aidha data za utafiti huu zilikusanywa uwandani kupitia mbinu za usaili na ushuhudiaji.Matokeo ya utaiti huu yanaonyesha kuwa mbazi ni kipera cha utanzu wa hadithi. Pia kupitia kigezo cha nduni bainifu utafiti huu ulibaini kuwapo kwa kumbo 11. kumbo hizo zimejumuisha mbazi za ulinganuzi mahususi,viumbe nasaha kinzani,wanadamu, usuluhishi,kuhamasisha jumla.kiishara na mbazi za kimethali .Halikadhalika utafiti huu umebaini kuwa kigezo chan duni bainifu kina manufaa makubwa katika kufanikisha uainishaji wa tanzu vipera na kumbo mahususi za mbazi. Isitoshe utafiti huu umebaini kuwa mchakato wa uainishaji wa umewasilisha dhima kubwa kitaaluma ikiwa ni pamoja na kuondoa mgongano uliokuwepo kuhusu nafasi ya kipera cha mbazi. Mgongano wa nafasi ya mbazi uliondolewa kupitia matokeo ya utafiti huu yaliyobainisha kuwa mbazi ni kipera cha utanzu wa hadithi kutokana na mfungamano mkubwa uliopo kati ya utanzu wa hadithi na mbazi katika nduni zake bainifu .Pia uainishaji umerahisisha ufundishaji wa fasihi simulizi kutokana na kupangiliwa mbazi katika mfumo wa nduni bainifu utanzu. kipera na kumbo .Mfumo huo unasaidia kujenga mantiki kwa mwalimu anayefundisha mbazi na kuwa mwanafunzi anayejifunza fasihi simulizi hususan kipera cha mbazi. Kadhalika tafiti nyingine zinaweza kuchunguza uainishaji wa mbazi kwa kuzingatia vigezo vingine vya uainishaji tofauti na kigezo cha nduni bainifu kilichozingatiwa katika utfiti huu .Utafiti huu umewafaa wanafunzi na wanazuoni kwa kuwa unaongeza maarifa kuhusu uainishaji katika fasihi simulizi ya Kiswahili
 • Item
  Uchambuzi wa takriri ya msamiati katika nyimbo za tamthilia ya nguzo mama (2010)
  (University of Dar es Salaam, 2019) Davison, Monica
  Takriri ni kipengele cha ushikamani wa msamiati ambacho kinahusisha marudio ya neno moja, matumizi ya visawe, hiponimu na hipanimu na maneno jumuishi. Utafiti huu unachambua takriri ya msamiati katika nyimbo zilizo katika tamthilia ya nguzo mama (Muhando 2010). Unaonesha jinsi kipengele kimoja katika matini kinavyoweza kuakisi na kuchanuza maana ya matini nzima. Ili kufanikisha kazi hii, nadharia ya ushikamani (halliday na Hassan 1976) na ya mchomozo ( leech 2008) ziliongoza utafiti huu. Mbinu za utafiti zilihusu: usampulishaji lengwa, usomaji makini na uchambuzi wa data kwa njia ya kitakwimu na kitaamuli. Tumebaini kuwa mwandishi alitumia aina zote za takriri ya msamiati ambazo ni takriri ya neno moja, visawe, hiponiumu na hipanimu na maneno jumuishi. Kadhalika, utafii umebaini kuwa takriri ya msamiati iliyotumiwa na mwandishi inawasilisha vizuri msisitizo wa wadhamira, migogoro ujumbe msimamo na falsafa ya mwandishi katika matini tulizochambua ( nyimbo ) kuna mbanano mkubwa wa takriri ya msamiati ambayo ilisababishwa na utokeaji wa alama za takriri ya msamiati zilizotokea kati ya mstari mmoja hadi wa nne. Mbanano huu unaonesha kuwa mwandishi alikuwa na kusudi la kukazia ujumbe wake kwa hadhira. Vilevile kuna ulegelege wa ala za ushikamani kwa kiwango kidogo. Hata hivo ulegelege huo haukuathiri mbanano uliopo katika nyimbo hizi. Kupitia utaii huu tumegundua kuwa takriri katika matini tulivochunguza ni muhimu katika ujenzi wa matini nzima na inauwezo wa kuwasilisha maana au ujumbe wa matini nzima. Tunapendekeza kuwa tafiti zijazo zichunguze takriri katika vipengele vingine vinavojenga tamdhilia hii kama usimulizi na mazungumzo. Vilevile, tafiti zijazo zinaweza kutumia mbinu yoyote ya kielimu-mitindo katika uchambuzi wa kipengele chochote cha matini na kisha kukihusisha na matini kubwa.
 • Item
  Atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira: uchanguzi wa ngano teule kutoka jamii ya wagogo
  (University of Dar es Salaam, 2019) Citungo, Mercy Abel
  Utafiti huu umechunguza atheri ya muundo wa ngano katika uwasilishaji dhamira kwa kutumia ngano teule kutoka jamii ya Wagog. Data zilikusanywa tangu Mei mpaka Juni 2018 katika mkoa wa Dodoma, wilaya ya Mpwapwa katika vijiji vya Inzomvu, Tambi, Mboli na. Mlrmbule. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza athari ya vipashio vya muundo wa ngano katika uwasilishaji wa dhamira.ili kutekeleza lengo hili, utafiti umeongozwa na malengo mahususi matatu ambayo ni kubainisha vipashio vya kisanaa vinavyojenga muundo wa ngano za jamii ya Wagogo, kuainisha miundo ya ngano za Wagogo kulungana na vipashio vya kisanaa vilivyobainishwa na kuchanganua athari vipashio vya kimuundo katika uwasilishaji wa dhamira. Kimsingi, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya ushiriki, mahojiano na majadala wa vikundi lengwa. Data ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ua Umuundo kama ilivyoasisiwa na Ferdnand de Saussure. Nadharia hii imejikita katika msingi mkuu unaoeleza kuwa kitu chochote kitaleta maana endapo kitakuwa na muunganiko wenye sehemu mbalimbali zenye uhusiano ili kukamilisha maana iliyokusudiwa. Utafiti huu umebaini kuwa kimuundo ngano za jamii ya Wagogo hujengwa na vipashio mbalimbali vya kisanaa hususan mianzo na miisho ya kifomula, wahisika na msuko wa matukio. Aidha, tumeibaini miundo mbalimbali ya ngano kama vile, muundo sahili, duara, rejeshi na changamano. Miundo hii katika ngano ndiyo huibua dhamira mbalimbali kulingana na aina ya muundo uliojitokeza. Halikadhalika, utafiti huu umebaini kuwa msuko wa matukio husaidia kutambulisha wahusika, mgogoro na ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira. Kutokana na matokeo hayo, utafiti huu umependekeza kuwa ipo haja ya kafasiri ngano za makabila mbalimbali katika lugha ya Kiswahili ili zisipotee. Hii inatokana na ukweli kwamba kutokana na maendeleo ya sayansi na technolojia, ngano katika jamii nyingi zina hatari ya kupotea kabisa. Aidha, mtafiti anapendekeza kufanyika kwa tafiti nyinginezo ili kufanya ulinganishi na kubainisha vipashio vya kisanaa vinavyopatikana katika ngano za jamii nyingine ili kuweza kubaini kama kuna kufanana au kutofautiana kwa vipashio hivyo.
 • Item
  Matumizi ya nyimbo za watoto katika muziki wa bongo fleva
  (Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2019) Mweta, Samweli Emmanuel
  Utafiti huu unahusu dhima ya matumizi ya nyombo za watoto katika muziki wa bongo fleva. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni;kubainisha nyimbo za muziki wa bongo fleva zinatotumia nyimbo za watoto, kubainisha dhamira zinazotokana na maatumizi ya nyimbo za watoto katika muziki wa bongo fleva , na dhima za matumizi ya nyimbo katika muziki wa bongo fleva . utafiti huu ulifanyika katika jiji la Dar es salaam katika wilaya tatu ambazo ni ilala, kinondoni na temeke, utafiti huu ulipitia maandiko mbalimbali hasa yanayohusu muziki wa bongo fleva na nyimbo za watoto. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini na nadharia ya mwitiko wa msomaji/msikilizaji.misingi ya nadharia hizi ndiyo iliyosababisha katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti huu.utafiti huu ulifanyika maktabani na uwandni na ulitumia mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa data kama vile ukusanyaje nausomaji wa matini, kusikiliza na kutazama video za muziki wa bongo fleva ,na kufanya mahojiano.matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, muziki wa bongo fleva una matumizi ya nyimbo za watoto. Mtafiti amebaini kuwa nyimbo za muziki wa bongo fleva zinazotumia nyimbo za watoto ni pamoja na Mama wa MR.Nice, Hello wa Diamond na Dede wa Aslay kwa kutaja chache.Aidha , dhamira zinazotokana na matumizi yz nyimbo za watoto katika muziki wa bongo fleva ni mgawanyo wa majukumu katika familia, uvumilivu, mapenzi ya dhati na kufichua uovu katika jamii. Aidha kwa upande mwingine dhima za matumizi ya nyimbo hizo ni kuasilisha muziki wa bongo fleva kufanya wimbo/muziki kuwa maarufu, utambulisho wa jamii, kufikisha ujumbe kwa njia ya kitoto, kuleta mvuto katika muziki, kuhifadhi fasihi simulizi na kuleta majaribio katika bongo fleva. Aidha , nyimbo hizi zinatumiwa na wasanii wa muziki wa bongo fleva kutokana na umuhimu wake katika jamii. Nyimbo za watoto katika jamii hutunza historia ya jamii, huleta ushirikiano na yanaonesha kuwa muziki huu ni sehemu ya maisha ya jamii kwa kuwa yanayozungumziwa ni yale yanayotoka katika jamii husika
 • Item
  Ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na Nje ya darasa katika ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili ikiwa lugha ya pili katika jamii ya Wairaki.
  (Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2019) Ginni, Veronica Felix
  Suala la mazingira ya ujifunzaji lugha ya pili (kuanzia sasa Lg2) limewavuta wataalamu mbalimbali. Hata hivyo hakuna utafiti uliofanyika kuhusu ulinganishi wa msamiati katika mazingira ya darasani na nje ya darasa katika kumwezesha mjifunzaji kumudu lugha ya Kiswahili katika jamii ya Wairaki. Hivyo, utafiti huu umechunguza ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na nje ya Darasa katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 katika jamii ya Wairaki. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vitatu vya Gilala, Maran na Kilimatembo katika kata ya Rhotia, Wilayani Karatu, Mkoani Arusha, Tanzania. utafiti ulikuwa na malengo matatu, kubainisha mazingira ya darasani na nje ya darsas yanayodhihirika katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya Wairaki, kuchungua dhima za mazingira ya darasani na nje ya darasa katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii Wairaki na kulinganisha dhima za mazingira ya darasani na nje ya darasa katika ujifunzaji msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya wairaki. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia kuu mbili, hojaji na usaili. Aidha, utafiti wa data uliongozwa na nadharia ya Utamaduni-Jamii. Matokeo ya utafiti ni kuwa mazingira ya nje ya darasa yanayodhihirika katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ni pamoja na mabango yaliyopo barabarani na madukani, mabanda ya video. Mazingira ya darasani yamehusisha: vitabu na matini mbalimbali, kamusi za Kiswahili. Vilevile, imebainika kuwa mazingira ya nje ya darasa yana dhima za kujenga kumbukumbu na kujiamini, kuchochea udadisi. Nayo mazingira ya darasani yana dhima za kujenga uelewa, kutoa motisha kwa mjifunzaji lugha . pia utafiti umebaini kuwa mazigira ya darasani na nyumbani yana dhima kubwa katika ujifunzaji wa Lg2 lakini kwa kiwango tofautitofauti. Hata hivyo, mazingira ya darasani yanaonekana kuwa ni faafu Zaidi katika ujifunzaji wa misamiati wa Kiswahili kwa wanafunzi wa Kiiraki kuliko mazingira ya nje ya darasa. Hii ni kutokana na matumizi makubwa ya Kiswahili katika jamii hiyo. Utafiti huu unapendekeza kufayika kwa tafiti za kina katka ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa kuchunguza tofauti za ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya Kibantu na ule wa jamii ambazo si za kibantu katika vipengele vya fonolojia, mofolojia na sintaksia za lugha husika.
 • Item
  Ulinganishaji wa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili ya Bakiza (2010) na kamusi kuu ya Kiswahili ya Bakita (2017)
  (University of Dar es Salaam, 2020) Haule, Jacob
  Utafiti huu umeshughulikia ulinganishaji wa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili fasaha ya BAKIZA (2010) na Kamusi Kuu ya Kiswahili ya TUKI (2017). Lengo la utafiti huu ni kubainisha vidahizo vyenye maana za msingi katika kamusi la Kiswahili Fasaha zinazotofautiana na maana za msingi za vidahizo hivyo katika Kamusi Kuu ya Kiswahili na kueleza tofauti zinazojitokeza kati ya maana za msingi za vidahizo vya kamusi la Kiswahili fasaha na maana za msingi za vidohizo hivyo katika kamusi kuu ya Kiswahili. Utafiti huu umefanyyika chuo kikuu cha Dar es salaam na data imekusanywa maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Uchambuzi wa data umefanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi linganishi na mkabala wa taamuli. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya metaleksikografia iliyoasisiwa na Wiegand (1983) inayofafanua masuala yote ya kileksikografia; kuanzia katika utafiti , ukusanyaji wa data ya Kamusi, uandishi, matumizi na uhakiki wa kamusi. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kuna vidahizo 53 ambavyo maana zake za msingi zinatofautiana katika kamusi teule. Aidha utafiti huu umeeleza tofauti zinazojitokeza kati ya maana za msingi za vidahizo vya kamusi teule. Tofauti hizo ni pamoja na unyume wa maana za msingi, tafauti za mawanda ya maana yam sing (mawanda finyu na mawanda mapana) , uhasishaji na uchanyishaji wa maana za msingi. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa kunakutofautiana kwa maana za msingi za vidahizo vya Kamusi la Kiswahili Fasaha na maana za msingi za vidahizo hivyo katika Kamusi Kuu ya Kiswahili. Kutofautiana kwa maana kwa maana za msingi za maneno yaleyale katika lugha moja si jambo la kawaida kwa sababu sifa kuu ya maana ya msingi ni kutokubadilika kulingana na muktadha. Kwa hivyo, ni muhimu kwa wanaleksikografia (waandaaji wa kamusi)) walimu kiswahili, wajifunzaji na wanaisimu kwa ujumla kutambua tofauti hizo za maana za msingi kwa kuwa itawasaidia kutumia lugha kwa uangalifu ili kuleta ufanisi katika mawasiliano na maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Pia, tunapendekeza kuwa ikiwa tofauti hizo za maana za msingi zitaendelea kuwepo, waandaaji wa kamusi wanapaswa angalau kueleza katika kamusi zao kwa kuwakamusi hizo (Kamusi la Kiswahili Fasaha na Kamusi Kuu ya Kiswahili) ni za lugha ya Kiswahili kwa ujumla zenye kulenga watumiaji wote wa lugha bila kujali muktadha. Hatimaye tunapendekeza kufanyika kwa tafiti fuatishi ili kuchunguza sababu za kutofautiana kwa maana hizo za msingi katika Kiswahili pamoja na athari zake kwa ujumla.
 • Item
  Michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili
  (University of Dar es salaam, 2020) Ladislaus, Paulina Kulwa
  Kisukuma ni miongoni mwa lugha za kibantu kama ilivyo Kiswahili, kimekopa maneno kutoka lugha mbalimbali za kibantu. Maneno hayo yanapokopwa hupitia michakato mbalimbali ili yafanane na mfumo wa lugha husika. Utafiti huu umechunguza michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili. Ambayo wasukuma wanayatuimia kama sehemu ya msamiati wa lugha yao. Hali hiyo imesababisha baadhi ya maneno ya kisukuma yaliyokuwa yakitumika hapo mwanzo kuanza kupotea na nafasi za maneno hayo kukaliwa na manenoyenye asili ya Kiswahili. Tafiti nyingi zilizofanyika kuhusiana na michakato ya kisemantiki zina mwenga wa lugha za kigeni. Utafiti huu uliazimia kufanyika katika lugha zenye asili asili moja yani Kibantu pekee ili kubaini michakato inayojitokeza nan i mchakato upi unaongoza kuchakata data za lugha zenye asili moja ambazo ni Kiswahili na Kisukuma zote zikiwa ni lugha za kibantu. Utafiti huu ulilenga kubainisha michakato ya kisemantiki katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili na kulinganisha michakato ya kisemantiki iliyobainishwa katika maneno ya kisukuma yenye asili ya Kiswahili ili kubaini ni mchakato upi unaotawala zaidi . utafiti huu utatoa mwongozo kwa watafiti wanaotaka kuchunguza michakato ya kisemantiki katika lugha nyingine za kibantu. Nadharia ya maana kama matumizi ya Wittgenstein (1953) iliongoza utafiti huu. Msing mkuu wa nadharia hii ni kwamba, ni kosa kuyawekea maneno mipaka katika matumizi, kwani kufanya hivyo ni kuyawekea mipaka maumbo ya kiiisimu. Hivyo maana za maneno zitokane na mahitaji ya jamii husika inayotumia maneno hayo. Maneno yaliyokopwa yametumika sawa na mahitaji ya jamii za Wasukuma. Eneo la utafiti lilikuwa mkoa wa Simiyu katika wilaya ya Busega kata ya Nyaluhande. Vijiji viwili vya Bdugu na Ng’wagindi viliteuliwa kuhakiki na kupata data nyingine za uhakiki zilizohitajika. Sampuli ya utafiti ilitokana na kundi la vijana 20 na wazee 20 wenye uwezo wa kuzungumza Kiswahili na Kisukuma. Utafitio huu ulitumia mbinu tatu ambazo ni mbinu ya maktabani, dodoso na mahojiano, data zilizokusanywa maktabani katika kamusi ya KKS (2013) toleo la tatu, kamusi ya Kisukuma yenye orodha ya maneno ya Kisukuma na kitabu cha dini nyimbo za sifa za Kisukuma (Mimbo). Data zilizokusanywa zilipelekwa uwandani kwa watoa taarifa kuhakikiwa kwa kutumia mbinu ya dodoso na majadiliano. Watafitiwa walipewa uhuru wakuondoa maneno ambayo hayakuwa ya mkopo kwa kuongeza mengine ambayo mtafiti hakuwa nayo. Utafiti ulitumia mkabala wa kimaelezo, data zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa data kimada na uchambuzi linganishi ili kurahisisha uchambuzi wake. Michakato minne ilibainishwa kuchakata data za lugha zenye asili moja ambayo ni MPK, MKK, MGK, MFK. Mchakato uliotawala zaidi ulibainishwa kuwa ni MFK ambao umeonekana kuchakata maneno mengi zaidi. Aidha, utafiti huu unapendekeza kuwa, tafiti fuatishi ziangalie michakato ya kisemantiki katika lugha nyingine za kibantu ili kuona hali inakuwaje katika lugha hizo.
 • Item
  Matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam, nchini Tanzania: Uchunguzi kifani wa majina ya watu
  (University of Dar es Salaam, 2020) Madila, Zacharia
  Utafiti huu unahusu matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam, nchini Tanzania. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha kiwango cha matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam. Aidha, utafiti huu ulilenga kutathimini mitazamo ya wanajamii kuhusu matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam. Kadhalika, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa njia ya usaili. Vilevile, utafiti huu umeshughulikiwa kiisimujamii kwa kuongozwa na Toleo la Wastani la Nadharia tete ya Uumbaji ya Sapir na Whorf ya mwaka 1958. Aidha data ya utafiti huu imechanganuliwakwa kutumia mkabala wa kitakwimu na kitaamuli. Hivyo kiwango cha matumizi ya majina ya Kiswahili jijini Dar es salaam ni asilimia ishirini na sita nukta mbili tano (26.25%) ya majina yote yaliyokusanywa katika utafiti huu . Aidha, kiwango cha matumizi ya majina kutoka lugha zingine ni asilimia sabini na tatu nukta saba tano (73.75%) ya majina yote yaliyokusanywa katika utafiti huu. Kadhalika, asilimia hamsini na moja nukta nane saba tano (51.875%) ya watoataarifa wameona kuwa majian ya Kiswahili yatumike katika uteuzi wa majina ya watu jijini Dar es salaam ilihali asilimia kumi na sita nukta mbili tano (16.25%) ya watoataarifa wameona kuwa majina ya Kiswahili yatumike lakini majina teule yanapaswa kuwa na maana nzuri. Pia asilimia nne nukta tatu saba tano (4.375%) ya watoataarifa wameona kuwa lugha yoyote inaweza kutumika katika uteuzi wa majina. Kwea upande mwingine, asilimia ishirini na tatu nukta moja mbili tano (23.125%) ya watoataarifa wameona kuwa majina ya Kiswahili yasitumike. Hivyo, ingawa matumiza ya Kiswahili katika shughuli za kila siku jijini Dar es salaam yamewashawishi watoatarifa wengi waone kuwa kuna haja ya kutumia majina ya Kiswahili lakini kuna vipengele vya kiisimujamii kama maana mbaya za majina, kasumba ya kupenda majina kutoka lugha za kigeni na athari za dini ambavyo vimeukilia kiwango kidogo cha matumizi ya majina hayo. Aidha ,utafiti huu unatoa wito wa tafiti zijazo kufanyika kuhusu matumizi ya majina ya Kiswahili katika maeneo mengine nchini Tanzania. Pia, utafiti ufanyike kuhusu sababu na athari za ubadilishaji wa majina katika jamii. Kadhalika, utafiti mwingine ufanyike kuhusu nafasi ya Kiswahili katika uteuzi wa majina ya utani katika jamii.
 • Item
  Mabadiliko katika fasihi simulizi ya wagogo
  (University of Dar es Salaam, 1977) Balisidya, May L.Y.
  Tasnifu hii ina 1engo la kuonyesha kuwa. ingawaje fasihl simulizi hutumiwa na jamii kisanaa kujieleza na hivyo kuielekeza na kuiendesha, hujengwa, na ni zao la jamii hiyo na mabadiliko yake. kwa hivi hutokea kuwa Itabadilika pamoja na jamii na katika kubadilika huku, itadhihirisha yale mabadiliko yanayoifika jamii, Fasihi simulizi haiachani na mwenendo wa jamii katika nyakati na maendeleo yake. ina ukongwe katika upokezi wa sanaa yenyewe, kama sanaa nyingine, hii sanaa iendayo wakati. Pia ni lengo la tasnifu hii kuuzingatia umiliki wa jamii wa fasihi simulizi na nafasi ya fanani wa fasihi hiyo katika jamii. Fasihi simulizi ni mali ya jamii kidhamira na kiutoaji, na kila mtu ana fursa ya kumilikl na kuzitumia tanzu mbali mbali. Fasihi hii ina fanani wake ambao hupewa hadhi kutegemea na nafasi inayopewa fasihi wanayo jihusishanayo l/ Tafasi ipewayo fasihi hiyo hutegemea dhima yake katika jamii yenyewe na jinsi gani fanani anaiwezesha fasihi hiyo kuitekeleza dhima hiyo. kwa hivi fasihi na fanani wake wataangaliwa katika nafasi na dhima yao katika nyakati mbali mbali za mabadiliko ya jamli. Kwa vile hivi sasa fani nyingi za fasihi hii zimo katika Lugha za makabila, iIi kuyakinisha kazi ya tasniîu hii, jamii ya Wagogo Imeteuliwa kufanylwa uchunguzi. lakini, hata huko Ugogonl, fani za fasihi Birnulizi zimetarnba katika: nathari, ushairl na semi kiasi kwamba kuziinglza zote katika tasnifu hii kutakuwa ni kurudufu mambo yanayozungumziwa kwa hivi, tanzu moja tu imeteuliwa kuehunguzwa ili inasibishe hoja zilizotolewa hapo juu. Tanzu hii ni hadithi. ”Hadithi” kwa mujibu wa tasnifu hii ni tanzu nzima ya fasihî simulizl ambayo inazo fani mbali mbali ndani yake. Hadîthi, Itakuwa ni aina ya faslhi inayojihusisha na usimulizi katika umbo Ia nathari (Iugha ya ujazo ya maongezi ya kila siku). Usimulizi ambao hupangwa katika mtiririko wa vituko unaokamilisha kisa/visa 2 fulani. igawanyo huu umetokana na mijadala ya Mwaka wa III, Idara ya Kiswahill Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 1975/76. Ruth Finnegan katike oral Literature in Africa, The Clarendon Press. oxford,1970 anagawanya Sasihi Simul izi katika sehemu tatu: Ushairi, Nathari na Fani Nyingżnezo. Fani ya Semi kwą muujibu wa tasniîu hii ni tungo fupi fupi zenye uzito wa taswira, aghalebu zenye mafunzo na maadili mathalan:methali, misemo, nahau, misimu vitendawili n.k. Kisa ina maana ya mfu1ulizo wa vituko unaokamilisha maelezo juu ya tukio fulani, Wahusika ndio nyenzo zitumiwazo (kwa kutenda, kutendewa na kujengwa kusimamia hali maridhawa za binadamu). Wao huzungumza, huzungumziwa na huzungumzishwa katika lengo la kutoa dhamira, maadili, ujumbe na falsafa zitakiwazo na mtunzi wa hadithi. kwa dhana hii, hadithi Ugogoni ina maumbo matatu: Simo Nghomo na Mbazi. Hata katika uteuzi wa tanzu hii, kulitafiti şuala la fasihi simulizi kama hilivyooneshwa, fani mbili tu zimeteuliwa kushughulikiwa, nazo ni Simo na Nghono. Hizi zinechaguliwa kwa vile ndizo kuu katika tanzu hii. Mbazi hazitashughulikiwa na tasnifu hii kwani si maarufu sana za huondokea kutungwa papo kwa papo zaidi kutegemea ufundi wa binafsi katika mazingira yanayo husika. mifano itakayotuniwa katika tasnifu hii itatolewa katika tafsiri sisisi iIi isipoteze ladha, usanii na maana yale katika Kigogo. tafsiri sabilia itakapotumiwa, ni pale tu ambapo kwa ajili ya kuapata maudhui kiujumla, pamelazimika kutolewa. ufupisho wa mfano mzima. Tasnifu yenyewe itagawanyika katika sehemu zifuatazo: Utangulizl: ambayo jamii ya Wagogo itaangaliwa katika muundo, mahusiano yake,historia na mazingira yake. Sehemu I Dhana ya hadithi kama Inavyoeleweka kwa Wagogo itazingatiwa na kugawanywa katika sura mbili kufuatana na fani zenyewe za hadithi. Sura ya Kwanza: Simo Sura ya Pill: Nghomo Sehemu II Kiini cha tasnifu hii kitakuwa hapa. Mabadiliko katika hadithi yataangaliwa kwa kugawanya sehemu hii katika sura tatu. Sura ya Kwanza: Mabadiliko katika Dhamana na Dhima ya hadithi.
 • Item
  Utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya kisubi
  (University of Dar es Salaam, 2020) Jasson, Tasiana
  Utafiti huu umechunguza utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha ya Kisubi Lengo lilikuwa kuweka bayana maumbo na mazingira ya utokeaji wa kiambishi tangulizi katika lugha hiyo. Data ya utafiti huu ilikusanywa uwandani katika eneo la Kata ya Nyarubungo iliyopo Wilayani Biharamulo, Mkoani Kagera. Mbinu ya hojaji na majadiliano ya vikundi lengwa zilitumika kukusanya data ya utafiti huu. Aidha, data ya utafiti huu ilichambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu ya uchambuzi wa data kimaudhui ilitumika. Nadharia ya Utangamano wa Mfuatano wa Mofimu ya McCarthy na Prince (1995) imetumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kiambishitangulizi katika lugha ya Kisubi kina maumbo sahili, yaani; maumbo ya irabu pekee. Maumbo hayo ni [a, e, i, o]. aidha, imebainika kuwa maumbo hayo hutokea katika mazingira maalumu ambayo ni bainifu. Mazingira hayo ni ya kategoria hizo ni nomino, kivumishi, kielezi na kibainishi. Hata hivyo, kuna vighairi vichache vya kategoria hizo visivyokuwa na kiambishi tangulizi, hususan vivumishi viulizi na nomino zinazotaja majina ya ndugu kama vile maha (mama), kaaka (bibi) na guuku (babu). Aidha, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kwenye kiima au kiarifu cha tungo hata kama tungo hiyo ina ukanushi, taarifa au ,asharti. Pia, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika kielezi kinapoandamana nakitenzi katika tungo. Kadhalika, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kabla ya kibainishi kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyopo kabla ya kibainishi kioneshi. Zaidi ya hayo, imenainika kuwa kiambishi tangulizi hakitokei katika nomino iliyopo baada ya kibainishi kioneshi. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa kiambishi tangulizi hutokea kwenye kivumishi cha pekee kinachotanguliwa na nomino. Pia, imebainika kuwa kiambishi tangulizi hutokea katika nomino iliyotanguliwa na kihusishi, nomino ya uhusika milikishi na nomino iliyotanguliwa na kiunganiishi huru. Utokeaji huu hutokana na michakato ya udondoshaji, uunganishaji na urefushaji wa irabu ya kihusishi, irabu ya kimilikishi au kiunganishi huru kilichotangulia nomino husika. Kwa hiyo, utafiti huu umebaini kuwa mazingira ya kimofolojia na kisintaksia ndiyo huamua kutokea au kutokutokea kwa kiambishi tangulizi katika lugha ya Kisubi. Aidha, utafiti huu umependekeza utafiti mwingine ufanyike katika kipengele cha ulinganishi wa ruwaza za utokeaji wa kiambiishi tangulizi katika lugha mbalimbali za Kibantu au zisizo za Kibantu.
 • Item
  Makosa ya kiisimu katika uandishi wa magazeti
  (University of Dar es salaam, 2011) Mghase, Gloria Elineema
  Utafiti huu unashughulikia makosa ya kiisima katika Uandishi wa magazeti hususani magazeti ya Kiswahili ya uhuru wa mtanzania ya nchini Tanzania ya kuanzia Julai hadi Disemba, 2010. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha na kuainisha makosa yanayojitokeza katika uandishi wa magazeti, kuelezea sababu za ujitokezaji wa makosa hayo pamoja pamoja na kupendekeza mbinu za kuyapunguza au kuyakomesha kabisa. Ili kufikia lengo hilo, utafiti huu ni nadharia ya Isimu zalishi (Geerative Linguistic Theory) na hasa mkabala wa umilisi na utumizi wa kiisimu (Linguistic competence and Perfomance) ambayo hushughulikia usahihi wa lugha katika matawi yote ya isimu ambayo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantic. Vyanzo vya makosa hayo vimebainika kuwa ni pamoja na kutokuelewa maana za maneno yanayotumika katika uandishi, athari za lugha ya mazungumzo katika uandishi pamoja na mazoea mabaya ya matumizi ya maneno mbalimbali. Aidha baadhhi ya mapendekezo yaliyotolewa ili kukomesha kama si kupunguza kabisa utokeaji wa makosa hayo ni pamoja hayo ni pamoja na kuboresha mfumo mzima wa ufundishaji na kuwajengea stadi stahiki za lugha za uandishi makini
 • Item
  Utohozi wa istilahu za kiingereza katika Kiswahili: uchunguzi kifani wa taaluma za tiba na compyuta
  (University of Dar es Salaam, 2019) Adolph, Editha
  Kila lugha huwa na utaratibu wake wa ukuzaji na uendelezaji wa msamiati. Katika mchakato wa kupata msamiati wa lugha husika, mbinu mbalimbali hutumika. Utohozi ni mbinu moja wapo ambayo lugha hutumia katika kujitajirisha kimsamiati. Ili msamiati uweze kukubalika katika mbinu hii, kuna michakato mbalimbali inayopitiwa. Michakato hiyo huweza kusababisha athari katika lugha pokezi. Utafiti huu umechunguza utohozi wa istilahi za fani ya tiba na kompyuta za kiingereza katika lugha ya Kiswahili kwa kuangazia michakato na athari zake. Utafiti umefanyika katika jiji la Dar es Salaam hususan katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kilichoko Wilaya ya Ubungo pamoja na baraza la Kiswahili la taifa lililopo wilaya ya Kinondoni. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya Fonolojia Zalishi (NFZ) iliyoasisiwa na Naomi Chomsky na Moris Halle (1968) pamoja na andharia ya mofolojia Leksika (NML). Ambayo mwasisi wake ni Kiparsky (1982). Aidha, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji na uchambuzi wa matini. Data iliyokusanywa ilichambuliwa kwa kutumia mkataba wa maelezo na wa kitakwimu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa lugha ya Kiswahili imetoa istilahi za fani ya tiba na kompyuta kutoka katika kiingereza. Pia, utafiti umebaini kuwa wakati wa utohozi wa istilahi katika Kiswahili, michakato mbalimbali ya kifonolojia, kimofolojia na kisintaksia hufanyika. Michakato hufanyika kadiri kanuni na taratibu za lugha ya Kiswahili ili istilahi ziweze kukubalika. Michakato ya kifonolojia iliyobainishwa katika utafiti huu ni pamoja na mchakato wa udondoshaji, uchopekaji, usahilishaji wa irabu uangalifu kuwa irabu sahili na mchakato wa ufupishaji wa irabu ndefu. Michakato ya kimofolojia iliyoonekana kutokana na uchambuzi wa data ni pamoja na uambishaji ambao unafungamana na upangaji wa istilah za Kiingereza katika ngeli za Kiswahili uchakataji wa istilahi zenye muundo wa maneno ambatani Kisintaksia, imabainika kuwa istilahi hutoholewa kwa kuhusisha mchakato wa kuchopeka vihusishi kati ya istilahi za Kiingereza. Halikadhalika, utafiti huu umebaini kuwa utohozi wa istilahi za fani ya tiba na kompyuta za kiingereza za kiingereza katika Kiswahili una athari chanya na hasi katika lugha ya Kiswahili. Athari chanya zilizobainika ni pamoja na zile za kifonolojia, kisemantiki na kileksia. Athari za kifonolojia zilizoonekana katika utafiti huu ni pamoja na muundo mpya wa silabi katika Kiswahili na athari za kimatamshi zinazoambatana na ufifishaji wa sauti. Athari za kisemantiki zilizobainika ni pamoja na upatikanaji wa dhana za kisayansi pamoja na visawe vinavyotokana na utohozi. Kwa upande wa athari za kileksika, imedhihirika kuwa baadhi ya istilahi za fani za tiba ya compyuta zimeonekana kuongezeka katika Kiswahili. Athari hasi zilizobainika ni pamoja na pamoja na zile za kimofolojia, kisemantiki na kileksika. Kimofolojia imeonekana kuwa utohozi umesababisha muundo wa istilahi ndefu na zenye kutatanisha katika matamshi. Halikadhalika, Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kisemantiki kumezuka mfumuko wa visawe katika Kiswahili. Kileksika imebainika kuwa zipo istilahi za tiba na kompyuta zinazotumika mara chache. Utafiti huu umependekeza kwamba utohozi wa istilah za lugha mbalimbali ufuate kanuni na taratibu zinazowekwa katika Kiswahili. Aidha kuna haja ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kutumia istilahi za Kiswahili hata kama kuna istilahi zinazotoholewa. Hivyo mtafiti anapendekeza kuwa pawepo na uhamasishaji wa matumizi ya istilah za Kiswahili zilizopo ili kuepuka mfumko wa istilahi nyingi zinazorejelea dhana moja. Mtafiti kuwa kuna haja ya kufanya uchunguzi zaidi kuhusu utohozi wa istilahi za kiingereza katika Kiswahili kwa miaka ijayo kwa kuwa ni bayana kuwa mchakato wa utohozi ni endelevu.
 • Item
  Changamoto za ufafanuzi wa maana za nomino za pekee katika kamusi za kiswahili: uchambuzi wa majina ya siku za wiki
  (University of Dar es Salaam, 2020) Nzala, Mayolwa John
  Utafiti huu ulilenga kuchunguza changamoto za ufafanuzi wa maana za Nomino za Pekee kwenye majina ya siku za wild katika kamusi za Kiswahili. Majina ya siku za wild yaliyokuwa yakichunguzwa kwenye utafiti huu ni Ijumaa, Jumapili, Alhamisi,Jumanne, Jumamosi, Jumatatu na Jumatano. Lengo kuu la utafiti huu liligawanywa katika malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha maana za majina ya siku za wild, kupambanua changamoto za kimaana kwenye majina hayo pamoja na kudabiri sababuza kuwapo kwa maana tofautitofauti na changamoto hizo za kimaana. Data zilikusanywa kutoka manispaa mbili za jiji la Dar es Salaam, ambazo ni Kinondoni na Ubungo. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni uchambuzi wa matini, hojaji pamoja na usaili.Nadharia Sababishi ya Urejelezi ya Kripke (2013) ndiyo iliyotumika katika uwasilishaji na uchanganuzi wa data. Sambamba na nadharia hiyo, uchanganuzi wa data ulitumia mikabala miwili; mkabala wa kitaamuli na mkabala wa kiidadi. Aidha, mikabala yote hiiilitumia mbinu ya uchanganuzi mada wa data. Data za utafiti huu zilionesha kuwa, tofauti na Alhamisi na Ijumaa yaliyotoholewa kutoka lugha ya Kiarabu, majina mengine ya siku za wild katika lugha ya Kiswahili kwa asili yalitokana na muunganiko wa nenola Kiarabu `juma' lenye maana ya `wiki' katika lugha ya Kiswahili na nambakadinali za Kibantu, mosi, pili, tatu hadi tano ndipo tukawa na majina ya Jumamosi, Jumapili hadi Jumatano (Kihore, 1997). Hata hivyo ilibainika kuwa, licha ya mpishano wa kimaanauliopo miongoni mwa kamusi teule za Kiswahili na miongoni mwa wazungumzaji wake, maana za majina ya siku za wild zilizoko kwenye kamusi zilionekana kupishana na maana zilizotolewa na watumiaji wa lugha hiyo. Msingi wa maelezo haya ulitokana na malengo ya utafiti ambayo yalibainisha kuwa katika lugha ya Kiswahili, majina ya siku za wild yamefasiliwa kwa maana zisizopungua tatu. Hii ina maana kwamba, kila jina la siku ya wild lina fasili tofauti zisizopungua tatu. Aidha, ilibainika kuwa, changamoto za kimaana kwenye majina ya siku za wiki zinatokana na mpishano wa fafanuzi za majina hayo kwenye machapisho ya kamusi pamoja na fasili za watumiaji wenyewe wa lugha ya Kiswahili. Sababu za kuwapo kwa half hii zimekuwa ni uhesabuji wa siku za wiki kwa mtazamo wa kidini, uhesabuji wa siku wa wiki kiserikali, kufasili maana za majina ya siku bila kuzingatia kanuni za kiisimu na ukosefu wa istilahi maalumu za kuyaita majina ya siku za wild katika lugha ya Kiswahili. Sababu zingine mbalimbali zilitolewa na watoataarifa. Sababu hizo zilikuwa ni mwingiliano wa tamaduni za kigeni katika jamii ya Waswahili, uigaji wa mpangilio wa siku za wiki za mataifa mengine duniani, athari za mfumo wa kalenda wa nchi za Magharibi katika Kiswahili pamoja na kuwapo kwa taratibu kubalifu za kikalenda kutoka nchi zilizoendelea. Kutokana na mkanganyiko wa kimaana unaoukiliwa na sababu hizo, utafiti huu umependekeza mtazamo unaofaa kutumika katika kuzifasili NP hususani majina ya siku za wiki katika lugha ya Kiswahili.
 • Item
  Dhima ya korasi katika utendaji wa ushairi simulizi mifano kutoka tamasha teule la nyimbo za bongo fleva la msanii nasibu abduli “diamond”
  (University of Dar es Salaam, 2015) Sway, Neema Benson
  Tasinifu hii ililenga katika kuchunguza dhima ya korasi katika utendaji wa ushairi simulizi kupitia tamasha teule “Diamonds are Forever” la nyimbo za bongo fleva la msanii Nasib Abdul “Diamond”. Malengo mahususi yalidhamiria kufafanunua vipengele vya korasi vya kifani na vya kiamudhui kupitia uttendaji wa nyimbo izo, kisha kueleza dhima ya vipengele hivyo katika kukamilisha utendaji wa ushairi simulizi. Utafiti huu katika ukusanyaji wa data, umetumia mbinu ya kusoma maandiko maktabani, utazamaji wa nyimbo zilizo rekodiwa, mahojiano, hojaji na majadiliano ya wasanii, madijei, wanafunzi na umahiri (M.A Kiswahili Fasihi) na wadau wa muziki wa bongo fleva wa mtandaoni na mashabiki wa huu. Nadharia ya Korasi iliyoasisiwa na Mutembei (2012) ndiyo iliotumika katika uchambuzi wa data za utafiti huu pamoja na mbinu ya kitaamuli. Matokeo ya utafiti kwa upande wa fani yamedhihirisha kwamba katika utendaji wa nyimbo za bongo fleva korasi inaweza kujitokeza , mathalani, kama mhusika (mhusika mkuu, mhusika kiungo, ahusika ambatani na wahusika watazamaji), kama kiitikio, mkarara, kimya, muundo, na mtindo (matumiziya giza, simulizi na mazungumzo mwanzo wa onesho na matendo bubu) ambao huweza kuwa ni wa kiparodosi (kitangulizi) au kiukengeushi. Vilevile, korasi katika utafiti huu imejitokeza kama falsafa na kama dhamira. Vipengele hivi vimekua ni mhiliwa utokeajii wa kazi nzima ya kisanaa ambapo kwavyo maadili ya jamii yameweza kupimwa na kuegemezwa. Kwa ujumla vipengele vya korasi kifani na kimaudhui vimesaidia kukamilisha utendaji wa ushairi simulizi kwa; kuhamasisha ushirikishwaji wa hadhira, kuchochea hisia za hadhira, kuibua fikra za hadhira, kudokeza na kusisitiza maudhui ya kazi ya fasihi kwa hadhira, kujenge mshikamano thabiti wa kazi ya sanaa, kutambulisha upekee wa msanii, kuvuta usikivu na umakini wa hadhira, na kuimarisha utendaji wa fanani kwa ujumla.
 • Item
  Nafasi ya dhana ya moyo katika kuibua dhamira na hisia za kishairi: uchunguzi wa ushairi wa andenenga
  (University of Dar es Salaam, 2015) Gawaza, Mwananuru Ismail
  Utafiti huu unahusu “ Nafasi ya Dhana ya Moyo Kiatika Kuibua Dhamira na Hisia za Kishairi: Uchunguzi wa Ushairi wa Andenenga. Utafiti ulihusisha mashairi kutoka katika Diwani ya Ustadh Andanenga na Bharii ya Elimu ya Ushairi. Lengo kuu l utafiti huu lilikua ni kuchunguza namna matumizi ya dhana ya moyo katika ushairi wa Andanenga yalivyo chochea uteuzi wa mbinu za kimtindo pamoja na uteuzi wa dhamira na hisia za kishairi. Maandiko na mchapisho mbalimbali yahusianayo na mada ya utafiti yamepitwa kwa kina kwa kuongoza na nadharia za Mwigo, Uhusivu n Mwingiliano Matini. Utafiti umetumia mbinu ya uchambuzi matini katika kukusanya data za msingi na data za ufatizi kutoka maandiko mbalimbali. Uchambuzi wa utafiti huu umefanywa kwa kuongoza na mbinu ya uchambuzi wa kimaelezo, uchambuzi matini na uchambuzi wa kifasihi ulioongoza na nadharia za Mwigo, Uhusivu na Mwingiliano Matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kua Andanenga amefanikiwa kutumia dhana ya moyo kwa kuikamilisha ushikamani wake kifani na kimaudhui. Tumelioma hili kupitia mbinu za kimtindo zilizotumika sanjari na dhana ya moyo pia katika dhamira na hisia tulizozichambua zilizonasibishwa na dhana ya moyo. Mwisho, tumetoa hitimisho kuu la utafiti na kuaiisha nyanja mbalimbali za kiutafiti zinazoweza kuibuliwa katika mashairi teule na ushairi wa Kiswahili kwa ujumla
 • Item
  Dhamana ya wakati kiusimulizi inavyojitokeza katika riwaya ya kiswahili ya kifantansia: uchunguzi kutoka Walenisi (1995) na babu alipofufuka (2001)
  (University of Dar es Salaam, 2019) Mushi, Anna Michael
  Utafiti huu umechunguza dhana ya wakati kiusimulizi katika riwaya ya Kiswahili ya kifantasia. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza jinsi dhana ya wakati inavyojitokeza kiusimulizi katika riwaya ya Kiswahili ya kifantasia. Malengo ya utafiti yalikuwa: Kuonesha aina za wakati kiusimulizi zilizotumiwa na wasanii wa riwaya teule, kubainisha viashiria vya wakati kiusimulizi vilivyotumiwa na wasanii kupitia riwaya teule, na kufafanua dhima ya wakati kiusimulizi katika riwaya ya Kiswahili ya kifantasia. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Naratolojia kwa mujibu wa Genette (1980), atnbapo mihimili ya kipengele cha wakati ilitumika kuchanganua data zilizohusiana na wakati. Ili kufikia malengo hayo, data za utafiti zilipatikana kutokana na uchambuzi wa riwaya teule za Walenisi (1995) na Babu Alipofufuka (2001). Tumebaini kuwa, dhana ya wakati ni nyenzo muhimu katika kusimulia matukio kwa mbinu na viashiria mbalimbali kwani matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, riwaya zote mbili zinatumia aina mbalimbali za wakati kiusimulizi . Aina hizi ni pamoja na wakati hadithi, wakati kamili, wakati husishwa na wakati unaotaja muda halisi uliotumika. Aidha, katika lengo la kubainisha viashiria vya wakati, wasanii wametumia viashiria mbalimbali ambavyo ni: giza, nyota, mwezi, pia wametumia viashiria vya maji ya mto, maji ya bomba lililopasuka pamoja na viashiria vya kiwakati kama ballad na mawimbi. Matumizi ya wakati yana dhima mbalimbali kwa mujibu wa utafiti huu. Wakati umeonesha mpangilio wa kazi ya msanii, umetumika kuonesha mtuo, umebainisha udondoshi wa matukio na umeibua mandhari. Pia, wakati umetumika kuelezea vipindi vya historia ya jamii, kufafanua muda maalumu wa matukio, na kutoa muhtasari katika kazi za fasihi. Aidha, wakati umetumika kuonesha hali ya maisha ya wahusika na kudhihirisha mabadiliko mbalimbali chanya ya wahusika kwenye jamii. Mchango wa utafiti huu ni kwamba, umeweka wazi aina za wakati zinazotumiwa na waandishi wa riwaya ya Kiswahili ya kifantasia pamoja na viashiria vya wakati vinavyotumiwa kwenye riwaya hizo, zaidi umechangia kufafanua dhima mbalimbali za matumizi ya wakati katika riwaya ya Kiswahili. Mchango mwingine ni kwamba umeendeleza hoja za wataalamu wengine wanaosema kuwa waandishi hawawezi kuukana wakati katika uandishi wao kwani matukio huhusishwa kwa kutazama majira ya siku hata mwaka. Mtafiti anapendekeza kuwa, kwa sababu utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Naratolojia, utafiti mwingine unaweza kufanyika kwa kutumia nadharia nyingine kama vile Uhalisia iii kuona kama wakati unaoelezwa katika riwaya ya kifantasia unaweza kuhusishwa na hali halisi au la na kueleza dhima yake. Aidha, utafiti mwingine unaweza kufanywa katika kazi nyingine za kifantasia za fasihi andishi ya Kiswahili kama vile tamthilia, hadithi fupi au ushairi andishi iii kujua kama matokeo yatakuwa sawa na matokeo ya utafiti huu na hivyo kutoa hitimisho la jumla la dhana ya wakati kiusimulizi katika kazi za kifantasia za fasihi andishi ya Kiswahili.
 • Item
  Ujitokezaji wa Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya ya Kiswahili; uchaguzi wa adili na nduguze (1952) na siku ya watenzi wote (1968).
  (University of Dar es Salaam, 2019) Kavishe, Agricola Roman
  Utafiti huu umechunguza ujitokezaji wa falsafa ya Ubuntu katika riwaya ya (1952) na Siku ya Watenzi Kiswahili ukijikita katika riwaya ya Adili na Nduguze Wale (1968). Utafiti huu uliongozwa na lengo kuu na malengo mahususi. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza ujitokezaji wa falsafa ya Ubuntu katika riwaya za Adili na Nduguze (1952) na Siku ya Walenzi Wow (1968) za Shaaban Robert.Malengo mahususi yalikuwa matatu nayo ni kubainisha vipengele vya falsafa ya Ubuntu vinavyojitokeza katika riwaya teule za Shaaban Robert, kueleza mbinu anuwai zinazotumika kusawiri vipengele hivyo vya Ubuntu na kufafanua umuhimu wa falsafa ya Ubuntu kisiasa katika riwaya hizo. Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu iliyoasisiwa na Tempels (1959) pamoja na wataalamu wengine ndiyo iliyotumika kutikia malengo ya utafiti huu. Ontolojia ya Kibantu ni mtazamo wa jamii ya Wabantu kuhusu maisha, kuwapo kwa mwanadamu na ulimwengu kwa ujumla. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani, mbinu za ukusanyaji wa data maktabani ulifanywa kwa kusoma maandiko na machapisho mbalimbali kwenye magazeti, majarida, vitabu vinavyohusiana na mada husika, pamoja na makala zilizo mtandaoni. Mtafiti alikusanya data zinazohusiana na falsafa ya Ubuntu kutoka katika riwaya zilizoteuliwa na kuzifafanua, kisha kubaini mbinu zilizotumika kusawiri falsafa ya Ubuntu katika riwaya hizo na umuhimu wa falsafa hiyo kisiasa. Tasinifu mbalimbali zilizozungumzia falsafa ya Ubuntu kwa namna mbalimbali zilitumika kupata taarifa. Vipengele vilivyojitokeza ndivyo vilivyojenga data kuu iliyofanyiwa uchambuzi na uhakiki. Matokeo ya data katika uchambuzi yalibainisha kwamba vipengele vya falsafa ya Ubuntu vinavyojitokeza katika riwaya hizo ni: utu, kazi, wema, busara, hekima na haki na usawa. Vipengele vingine ni ndoa, ukarimu, upendo, malezi, huruma halikadhalika umoja na ushirikiano. Mbinu mbalimbali zilizotumika kusawiri vipengele hivyo ni methali, barua, nyimbo, kilio, kicheko na lugha ya watoto. Ilibainika kwamba vipengele vya falsafa ya Ubuntu vina umuhimu mkubwa kisiasa katika riwaya teule. Umuhimu huo ni pamoja na kujenga uongozi bora, kusaidia raia wenye shida, kupigania haki na usawa, kujali utu wa raia, na kuwa mwema kwa raia. Aidha, utafiti umebaini kuwa mwandishi Shaaban Robert katika riwaya zake zilizotafitiwa amesawiri vipengele mbalimbali vya falsafa ya Ubuntu ambavyo tunaamini ndiyo falsafa iliyomkuza pamoja na jamii yake. Hii inatueleimisha zaidi kuhusu falsafa ya Shaaban Robert kuwa hakuathiriwa to na falsafa ya Kimagharibi na mtazamo wa dini ya Kiislamu. Utafiti huu umetoa muongozo kwa waandishi na wahakiki wa kazi za fasihi kuhusu ujitokezaji wa falsafa ya Ubuntu na inavyosawiri maisha ya waandishi na jamii kwa ujumla.