Changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya kiswahili nchini Tanzania.

Loading...
Thumbnail Image
Date
2018
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Matumizi ya katuni-mnato-bubu katika kufikisha ujumbe kwa jamii yanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaana katika kusimbua ujumbe. Lengo la utafiti lilikuwa ni kuchunguza changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania. Ili kukamilisha utafiti huu, data ilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Mbinu ya uchambuzi matini ilitumika kwa kuwa iliwezesha kukusanywa kwa katuni. Mbinu ya mahojiano ilitumika uwandani na kuwezesha kupatikana kwa data kutoka kwa watoa data asilia. Aidha, nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Nadharia ya Alama ya Piece ya mwaka (1904). Misingi yake iliwezesha kubaini changamoto za kimaana zinazotokana na kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya Kiswahili. Pia sababu za kutokea kwa changamoto hizo zimebainika na kujadiliwa katika ripoti hii ya utafiti. Kimsingi utafiti umebaini kuwa katuni zina maana na zinabeba ujumbe. Pia, utafiti umebaini kuwa, kuna changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni. Baadhi ya changamoto hizo ni: kuwapo kwa mkanganyiko wa kimaana, kushindwa kuhusisha matukio katika safu za katuni, kushindwa kusimbua alama ili kujenga maana, na kupotoshwa kwa ujumbe uliokusudiwa na nyingine zilizojadiliwa. Changamoto hizo zinasababishwa na uzoefu wa kimaisha, mtazamo wa mtu au jamii, mila na desturi za jamii, eneo la kijiografia, itikadi zilizopo katika jamii na nyingine zilizojadiliwa. Mwisho, mtafiti anatoa mapendekezo kuwa kuna haja ya kufanya tafiti nyingine kubaini changamoto za kimaana zinazojitokeza katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato za aina nyingine na mambo mengine mbalimbali yanayohusu katuni kwa ujumla.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.T34K424)
Keywords
Swahili literature, Magazeti ya kiswahili, Katuni mnato bubu, Tanzania
Citation
Kilapilo, V. (2018). Changamoto za kimaana katika kusimbua ujumbe kwenye katuni-mnato-bubu za magazeti ya kiswahili nchini Tanzania. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.