Athari za kifonolojia na kimofolojia za Kiswahili cha mwambao wa ziwa Tanganyika Katika Kiswahili sanifu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umechunguza sifa na athari za kifonolojia na kimofolojia za Kiswahili cha Mwambao wa ziwa Tanganyika katika Kiswahili sanifu ili kubaini hali ya kiisimu ya Kiswahili sanifu katika eneo ambalo ni makutano ya watumiaji wa Kiswahili kutoka Tanzania, Kongo, Burundi na Zambia wakiwa na lugha zao za makabila pia. Utafiti huu umetumia data kutoka uwandani na maktabani. Data ya uwandani, imekusanywa katika kata za mwambao wa ziwa Tanganyika, wilayani Nkasi kwa kutumia mbinu za ushuhudiaji, hojaji, usaili na utungaji wa insha. Kata hizo zimeteuliwa kutokana na uhusiano mkubwa wa kibiashara na kijamii baina ya watumiaji wa Kiswahili sanifu kutoka Tanzania, Kiswahili cha Kongo, Kiswahili cha Zambia na Kiswahili cha Burundi. Data ya maktabani imetumika kufafanua na kushadidia hoja na data ya uwandani katika ilivyofafanua vipengele mbalimbali. Data imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kiidadi. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Mwachano na Makutano na Nadhariatete ya Ndugu na Ndugu wa Mbali iliyoasisiwa na Massamba (2007). Nadharia hii imeonekana kulandana na hali halisi ya Kiswahili kinachotumiwa eneo la utafiti. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa Kiswahili sanifu katika mwambao wa ziwa Tanganyika kimepata athari katika vipengele vya fonolojia na mofolojia kutokana na makutano ya watumiaji wake na watumiaji kutoka maeneo mengine ya utafiti huu. Aidha, uthari hizo zimesababisha baadhi ya maumbo katika msamiati wa Kiswahili sanifu kuathirika na kuonekana kuwa msamiati mpya katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Utafiti unapendekeza kufanyika kwa utafiti mwingine kama huu utakaojikita katika kuchunguza mchango wa KMZT katika msamiati wa Kiswahili sanifu. Aidha, unaweza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu vipengele vya kiisimu kinachotajwa na baadhi ya wanaisimu kuwa Kiswahili sanifu cha Kongo.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8702.I74)
Keywords
Swahili language, Morphology, Phonology
Citation
Isindikiro, Joseph (2016) Athari za kifonolojia na kimofolojia za Kiswahili cha mwambao wa ziwa Tanganyika Katika Kiswahili sanifu,Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam