Athari za kiswahili katika msamiati wa kiwanji
No Thumbnail Available
Date
2014
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia Athari za Kiswahili katika Msamiati wa Kiwanji. Utafiti huu umefanyika wilayani Makete, Mkoa wa Njombe nchini Tanzania. Ili kufikia malengo yake, mbinu na njia mbalimbali za utafiti zikiwa ni pamoja na mbinu ya maktabani na uwandani zimetumika. Na njia zilizotumika katika ukusanyaji wa data ni mahojiano pamoja na ushuhudiaji. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Makutano na Mwachano ya Giles na Byrne (1982), ambayo inaeleza kuwa lugha zinazokaribiana kimaeneo zinaweza kuathiriana. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kuna athari mbalimbali za Kiswahili katika msamiati wa Kiwanji ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya msamiati wa Kiswahili katika Kiwanji, athari ya uchanganyaji lugha, upotoshaji wa matamshi sahihi ya msamiati wa Kiwanji, msamiati asilia wa Kiwanji kupotea, na msamiati wa Kiwanji kupungua matumizi. Vilevile, sababu zilizobainika ambazo huchangia athari hizi ni pamoja na mwingiliano wa kimatumizi wa Kiswahili na Kiwanji, baadhi ya maeneo kutozungumza Kiwanji, pia fahari ya kutumia Kiswahili kuliko Kiwanji, uhaba wa msamiati wa Kiwanji, na shughuli za kijamii na kibiashara. Mapendekezo yaliyotolewa ili kupunguza athari hizi ni pamoja na kuandaa makongamano na warsha mbalimbali za kuelimisha kuhusu umuhimu wa lugha za asili kama Kiwanji. Pia lugha ya Kiwanji ifanyiwe tafiti zaidi, ili iweze kuandikiwa kwa lengo la kusomwa na watu mbalimbali pamoja na kuitunza, kukipa Kiwanji dhima mbalimbali katika jamii, na kudumisha uhalisia wa lugha hiyo kwa kuzienzi mila na desturi.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.L87)
Keywords
Wanji language, Swahili language, Wanji (African people), Languages
Citation
Lusanjala, S. U. (2014) Athari za kiswahili katika msamiati wa kiwanji, Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.