Athari za maendeleo ya Sayansi na teknolojia katika nyimbo za michezo ya watoto: mifano kutoka katika Mkoa wa Dar es Salaam

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unabainisha athari za maendeleo ya sayansi na teknolojia katika fasihi ya watoto hususani nyimbo za michezo ya watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam .Watoto wa Mkoa huo wanachukuliwa kama kiwakilishi tu cha watoto wakitanzania popote walipo mijini na vijijini nchini Tanzania ili kufanikisha kupata data za utafiti huu, mtafi ti alitcmbelea rnaeneo yal iyoteul iwa katika Mkoa wa Dar es Salaam katika wilaya zote talu yaani, Wilaya ya Temeke, Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Kinondoni, ambayo kwa kiasi fulani yanah usika na maendeleo ya sa) ansi na teknolojia. Mbinu zilizotumika katika kupata data za utafiti huu ni mbinu ya mahojiano/ usaili, mbinu ya hojaji na mbinu ya ushiriki Katika utafiti huu, nadharia ya Sosholojia ilifanikisha uchambuzi sahih wa data za utafiti. Hivyo mtafiti alifanikiwa kubainisha athari Chanya ambazo ni kurahisisha kuenea kwa nyimbo za watoto kutoka eneo moja kwenda nyingine kukuza vipaji vya watoro. kukuza ajira, kuleta umoja miongoni mwa watoto, kutunza kumbukumbu, kuungan isha vizazi mbalimbali na jamii na kukuza ubunifu miongoni mwa watoto. Athari Hasi ni kupoteza utendaji, k.utobadil ika kwa kazi ya sanaa ku lingana na wakati na malezi ya watoto. Hivyo malengo ya utafiti huu yamefikiwa na maswali yamejibiwa kama yalivyokusudiwa. Utafiti huu ulibaini pia kwamba kuna Fulani zilizofanyika na wanazuoni mbalimbali ili kuendeleza Fasihi ya Watoto hususani michezo ya watoto wadogo, na hasa ile inayoambatana na nyimbo. Hata hivyo tafiti zilizofanyiwa kuhusu nyimbo za michezo ya watoto bado hazitoshelezi.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wirbert Chagula Library, Class mark (THS EAFM1997.A85U72)
Keywords
Children's song, science, Technology, Dar es Salaam
Citation
Urassa, C. C (2011) Athari za maendeleo ya Sayansi na teknolojia katika nyimbo za michezo ya watoto: mifano kutoka katika Mkoa wa Dar es Salaam, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.