PhD Theses

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 31
  • Item
    Uchambuzi linganishi wa Ujumi wa kifasihi katika simulizi teule za watumwa kutoka Afrika, Amerika na Ulaya.
    (Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2020) Henry, G
    Uchambuzi linganishi wa Ujumi wa kifasihi katika simulizi teule za watumwa kutoka Afrika, Amerika na Ulaya. Grace Henry Tasnifu ya phD (Kiswahili) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, 2020 Utafiti huu unachambua kiulinganishi simulizi teule za watumwa kutoka Afrika, Amerika na ulaya ili kuonesha ujumi wa kifasihi unaojitokeza katika simulizi hizo. Aidha, licha ya madai yaliyopo kwamba simulizi za watumwa ni utanzu wenye nduni bainifu majumui, utafiti huu unajadili pia upekee wa simulizi za watumwa kutoka jamii hizo. Aidha licha ya madai yaliyopo kwamba simulizi za watumwa ni utanzu wenye nduni bainifu majumui, utafiti huu unajadili pia upekee wa simulizi za watumwa kutoka jamii hizo. Simulizi teule zilizochzmbuliwa ni Uhuru wa watumwa (1934) na Mama Meli: from Slavery to freedom (1993) kutoka Afrika: interesting narrative of the life of Frederick Douglass: an American slave (1845, na incidents in the life of a Slave Girl: written by Herself (1861) kutoka Amerika: na The letters of Ignatius Sanch. An African (1782) na History of Mary Price: a West Indian Slave (1831). Kutoka ulaya. Pia utafiti huu umechunguza mwingilianomatini uliopo kati ya simulizi za watumwa na kazi teule za fasihi ya Kiswahili ambazo ni tendehogo (1984) , kwaheri iselamagazi (1992), Miradi bubu ya wazalendo (1995) na kasri ya mwinyi fual (2007). Katika kukamilisha malengo ya utafiti huu, utafiti uliongozwa na nadharia za za Sosholojia ya kifasihi,, naratolojia, na mwingilianomatini. Mbinu mbalimbali kama vile eneo la utafiti, sampuli ya utafiti na usampulishaji zilitumika katika ukusanyaji, uhifadhi na uchambuzi wa data. Baada ya uchunguzi, ujumi wa kifasihi katika simulizi za watumwa kama vile msuko wa matukio, motifu, wahusika, na matumizi ya sauti na nafsi za usimulizi umejadiliwa. Aidha, umahususi wa ujumi wa kifasihi katika simulizi za watumwa kutoka jamii tofauti (afrika, Amerika Na Ulaya ) kama vile majina ya vitabu, baadhi ya ruwaza, na motifu umebainishwa. Umahususi huo unasababiswa na miktadha tofauti ya kihistoria, kiuchumi na kijamii iliyokuwapo katika jamii hizo kipindi cha utumwa na wakati wa utunzi wa simulizi husika. Baadhi ya miktadha hiyo ni jadi simulizi ya kiafrika, utawala wa Mwingereza, utangamano wa wa kijamii, mchango wa wanaharakati wa kikomesha utumwa na kadhalika. Pia, kama kazi za fasihi, simulizi za watumwa zinaingiliana na kazi nyingine za ubunifu za fasihi katika vipengele mbalimbali vya kifani na kimaudhui kama vile ruwaza, motifu, sauti za usimulizi, nafsi za usimulizi, na wahusika.
  • Item
    Utokeaji wa Yambwa na dhima zake katika Kimatengo Na Kiswahili
    (Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2020) Nchimbi, F
    Utokeaji wa Yambwa na dhima zake katika Kimatengo Na Kiswahili Fokas Nchimbi Tasnifu ya Kiswahili (PhD) University of Dar es salaam, Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili 2020 Utafiti huu ulichunguza mazingira ya utokeaji wa yambwa na dhima zake katika Kimatengo na Kiswahili. Ili kufikia lengo hilo utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sarufi ya Uamilifu wa Kileksika inayoeleza kwamba katika muundo wa kiambajengo kuna uwasilishwaji wa vipashio vya kileksika vyenye dhima za kisintaksia kama vile kiima cha kiarifu; na vile vyenye sifa za sententiki kama vile mtenda, mtendwa mtendewa. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi mawili. Kwanza, kubainisha sifa msingi zinazohalalisha utokeaji wa yambwa katika maumbo asilia ya vitenzi vya kimatengo na Kiswahili. Pili, kufafanua athari za unyambuzi katika utokeaji na dhima za yambwa katika na Kiswahili. Maswali ya utafiti huu yalikuwa mawili ambayo ni: sifa gani msingi zinaamua utokeaji wa yamba na dhima zake katika maumbo asilia ya vitenzi vya Kimatengo na Kiswahili? Unyambuzi wa vitenzi una athari gani katika mazingira ya utokeaji wa yambwa na dhima zake katika Kimatengo na Kiswahili? Data za utafiti huu ni wa kitaamuli, data za utafiti huu zilikusanywa kusini magharibi mwa Tanzania, katika vvijiji vitatu vya wilaya ya mbinga ambavyo ni Myangayanga, Kindimba na Wukilo. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia kuu nne, ambazo ni maandiko ya maktabani, hojaji, usaili, ushuhudiaji na vikundi vya majadiliano. Kwa sababu utafiti ni wa kitaamuli, data za utafiti zimewasilishwa na kuchanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa kufafanua nduni za kisintaksia na kisemantiki za yambwa kama zinavyoamuliwa na maumbo mbalimbali ya vitenzi vya Kimatengo na Kiswahili. Kulingana na malengo na maswali ya utafiti, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa sifa ya kiwango cha uelekezi wa maumbo asili ya vitenzi ndiyo inayoamua hali ya uwasilishwaji wa nomino kapa, nomino moja hadi nomino mbili za yambwa, ambapo aina za yambwa huwa ni yambwa tendewa na yambwa tendwa. Pili kuna uwezekano wa kuumba maumbo nyambuzi mbalimbali katika Kimatengo na Kiswahili . maumbo hayo nyambuzi yanayoathiri mazingira ya uwasilishwaji wa yambwa na dhima zake kisintaksia na kisemantiki ni utendea, utendesha,utendeshea, utendano, utendeka,utendeano,utendesheano,ujirejea, utendua na utendwa. Hali kadhalika, matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa mazingira ya uwasilishwaji wa yambwa na dhima zake za kisintaksia na kisemantiki yanaamuliwa na aina ya umbo na maana msingi ya kitenzi na maana msingi ya nomino husika ya yambwa. Katika Kimatengo na Kiswahili kuna uwezekano wa kutokea kwa nomino mbili za yambwa, ambazo ni yambwa tendewa na yambwa tendwa. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa katika Kimatengo hakuna maumbo tendwa yanayojitokeza kwenye vitenzi katika lugha nyingine za Kibantu kama vile Kiswahili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna haja ya kuendelea kukifanyia utafiti zaidi kipengele cha yambwa katika lugha za kibantu ili kubaini umahususi wa kila lugha kuhusu viashiria vya kisintaksia na kisemantiki vya yambwa. Katika kimatengo na Kiswahili kuna haja ya kufanya utafiti kuhusu kipengele cha kiambishi cha yambwa katika maumbo mbalimbali ya vitenzi vyake na kuhusu ukwezwaji unaoonesha umada wa nomino ya yambwa pamoja na kategoria nyingine muhimu katika sentensi za lugha hizo
  • Item
    Mkazo Katika Kiswahili Sanifu
    (University of Dar es Salaam, 2019) Mwendamseke, Faraja Japhet
    Utafiti huu ni wa kifonolojia uliochunguza mkazo katiak Kiswahili sanifu. Jumla ya watoa taarifa 20 wamehusika katika kutoa data iliyotumika katika utafiti huu. Watoa taarifa 10 walitoka kata ya Ngamiani Kati na Chumbageni katiak jiji la Tanga, mkoani Tanga. Watoa taarifa wengine 10 walitoka katiak Jiji la Tanga, mkoani Tanga. Watoa taarifa wengine 10 walitoka katika shehia ya Mkunazini na Shehia ya Malindi, UNGUJA MJINI, Zanzibar. Taarifa hizo zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ni wa kiidadi na kimaelezo ambao umefanyika kwa kuongozwa na nadharia ya Fonolojia Mizani. Data zilizokusanywa zilichunguzwa kwa kusikilizwa kwa makini na kwa kutumia program ya “Praat”. Aidha, matokeo ya utafiti huu yaonesha kuwa uchunguzi wa mkazo katika kiwango cha neon hujibainisha tofauti na mkazo katika kirai na sentensi. Mara nyingi mkazo msingi katiak neon hutokea katika silabi ya mwisho kasa moja, wakati mwingine mkazo msingi hutokea katiak katika silabi ya mwisho katika vihisishii. Kwa upande wa kirai na sentensi mkazo msingi hutokea katika neno la mwisho katiak tungo husika. Hata hivyo, katiak Kiswahili sanifu imebainika kuwa licha ya kuwepo mkazo msingi katika neno, kirai na sentensikuna aina nyingine pia za mkazo. Yaani mkazo upili, mkao utatu na mkazo dhaifu, kutegemeana na namna utamkaji unavyojidhihirisha katika neno, kirai na sentensi kuna aina nyingine pia za mkazo. Yaani mkazo wa pili, mkazo utatu na mkazo dhaifu, kutegemeana na namna utamkaji unavyojidhirisha katika viambajengo hivyo. Kwa hiyo, kila kiambajengo kinakiasi Fulani cha nguvumsikiko. Pia, licha ya ruwaza ya mkazo kuwa funge kama ilivyoelezwa na wataalamu wengine kama vile Halle naClements (1983) na Massamba (2011). Utafiti huu umeenda mbele zaidi na kubaini kuwa ruwaza ya mkazo inaweza kuathiriwa na michakato ya kifonolojia kama vile udondoshaji, michako ya kimofolojia kama vile uambatani na uradidi. Aidha, katika uamilifu wa mkazo utafiti huu umebaini kuwa na uaminifu ufuatao: kwanza ni kuwekewa nguvu katika silabi au neno wakati wa utamkaji ili kuonesha msigano wa msikiko katika viambajengo vinavyohusika. Pili, kuna wakati mkazo huwa na uamilifu wa kuonesha msisitizo katika kiambajengo kinachohusika yaani katika neno, kirai au sentensi. Tatu mara chache mkazo huweza kubadili maana ya msingi ya msingi ya neno, hutokea katika baadhi ya maneno mkazo unapohama. Aidha, kutokana na uamilifu wa mkazo tumeweza kutofautisha mkazo na kiimbo pamoja na kidatu katika katika Kiswahili sanifu. Hata hivyo, kuna mazingira mengine kiimbo na kidatu huweza kuathiri mkazo lakini athari hiyo ya kimsikiko haibadili uamilifu wa mkazo.
  • Item
    Ujitokezaji wa falsafa ya Kiafrika katika Riwaya za kiethnografia za Kiswahili
    (University of Dar es Salaam, 2019) Mpalanzi, Lameck
    Utafiti huu unachunguza ujitokezaji wa vipengele vya falsafa ya Kiafrika katika riwaya teule za kiethnografia za Kiswahili. Vipengele vilivyochunguzwa ni dini ya jadi, uganga na uchawi, uzazi, uhai na kifo na uduara wa maisha. Katika kuchunguza vipengele hivyo, riwaya zilizoteuliwa na kuchambuliwa ni Kurwa na Doto, Mirathi ya Hatari na Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka; Ntulanalwo na Bulihwali. Vilevile, utafiti ulilenga kubainisha namna vipengele teule vilivyomo katika riwaya vinavyoakisiwa katika jamii teule za Unguja, Njombe na Ukerewe. Aidha, utafiti ulilenga kuchunguza mwingiliano wa riwaya ya kiethnografia ya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika. Kadhalika, utafiti unafafanua mehango wa falsafa ya Kiafrika katika maendeleo ya fani na maudhui ya riwaya teule. Katika kukamilisha malengo haya, data ilikusanywa maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu ya udurusu wa maandiko maktabani, mahojiano, hojaji, ushuhudiaji na ushiriki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili kuanzia nyakati za ukusanyaji data hadi uchambuzi. Nadharia ya kwanza inaitwa Ontolojia ya Kibantu, na ya pili Sosholojia ya Fasihi. Ontolojia ya Kibantu ilituongoza kuchambua masuala yanayohusu falsafa yaKiafrika na Sosholojia ya Fasihi ilitusaidia kuhakiki masuala yanayohusu uhusiano wa fasihi na jamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa fasihi hubeba falsafa ya jamii kwa kuwa vipengele teule vya falsafa ya Kiafrika vinadhihirika bayana katika riwaya teule. Utafiti umethibitisha kuwa tambiko linachukua sehemu kubwa ya dini ya jadi, ambayo ndiyo mzizi wa imani ya Waafrika. Jamii hizi zina matambiko mengi, mathalani, jamii ya Wamakunduchi ina tambiko is Mwaka-kogwa, tambiko la kumaliza msiba,tambiko la uzazi, tambiko la unyago na tambiko la mazishi. Jamii ya Wabena ina tambiko la kafara (Kipongo), Nyumbanitu na Amalimilo. Kwa upande mwingine, Wakerewe wana tambiko la kuzaliwa, uzazi na kutanabahi katika pembe, tambiko la kumtoa mtoto nje,tambiko la harusi, tambiko la kuvundika ndizi, tambiko la ugonjwa na tambiko la mazishi. Pia, Wakerewe, wana tambiko la machifu huko Kitare, tambiko katika makumbusho ya Handebezyo na katika "Jiwe Linalocheza." Utafiti umebaini kuwapo kwa imani mseto katika jamii teule inayotokana na mwingiliano wa dini ya jadi na dini za kigeni. Kuwapo kwa imani mseto ni jitihada za jamii teule kutafuta utambulisho na ukubalifu wa kila kundi. Utafiti umebaini kuwa upo mpaka bayana kati ya fani ya uganga na uchawi kwa kuzingatia kigezo cha utendaji, dhima, kiwango cha nguvu-hai, miiko na ufantasia wa fani hizo. Uchunguzi katika riwaya na jamii teule umebaini kuwapo kwa makundi kumi (10) ya waganga na makundi mawili (2) ya wachawi. Utafiti unaonesha kuwa baadhi ya waganga na wachawi wanaishi maisha duni kwa kuwa hutumia gharama kubwa kununua viambato vya uganga na uchawi. Licha ya kufumbata falsafa mbalimbali za maisha, suala la uzazi katika jamii ya Ukerewe ni mfano dhahiri wa kuwapo kwa familia pana ya Kiafrika inayojumuisha watu-hai, waft' na watakaozaliwa. Sanjari na hilo, utafiti huu unaafiki kuwa kifo kwa Mwafrika si mwisho wa maisha kwani mfu huendelea kuwapo kama inavyoelezwa katika Ontolojia ya Kibantu. Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa maisha ya maana na halisi ni ya hapa duniani. Aidha, utafiti huu ulibaini kuwapo kwa uhusiano wa kiduara kati ya mtu, jamii na mfumo uliopo. Kiontolojia, utafiti umethibitisha kuwapo uhusiano wa kiduara kati ya Mungu, mizimu, wahenga, binadamu, wanyama na mimea, na vitu na mahali. Katika kudhihirisha fasihi inavyobeba falsafa ya jamii, utafiti huu umetambua kuwa fasihi na falsafa ya Kiafrika hutenda majukumu yanayofungamana. Mwisho, utafiti huu unabainisha kuwa falsafa ya Kiafrika ni malighafi na nyenzo muhimu katika uandishi wa fani na maudhui ya riwaya ya Kiswahili.
  • Item
    Uchanganuzi wa mbinu za kisarufi na kibalagha katika vilongo teule vya kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015, nchini Tanzania
    (University of Dar es Salaam, 2020) Sovu, Yahya Ahmad
    Utafiti huu ulilenga kuchunguza lugha ya kisiasa, hususani katika kipindi cha kampeni za uchaguzi wa 2015 nchini Tanzania. Hoja kuu ikiwa ni kuchambua kwa undani mbinu za wanasiasa na nduni anuwai wanazozitumia katika mikutano ya kampeni za uchaguzi. Ili kutimiza hoja hii utafiti ulilenga hasa kubaini nduni za kisarufi na kibalagha katika vilongo teule vya hotuba za kampeni za uchaguzi za mwaka 2015, kuchunguza dhima zake katika kampeni za uchaguzi na kupambanua iwapo mbinu hizo zina athari chanya na hasi kwa hadhira. Data za utafiti zilikusanywa maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa nyaraka, usikilizaji wa hotuba, usomaji wa maandiko, usaili, na hojaji. Mkabala wa kitaamuli, na wa kiidadi kwa kiasi kidogo ilitumika kuchambua data zote. Mkabala wa Uchanganuzi Tunduizi Kilongo pamoja na Nadharia ya Balagha zimetumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba, hali ya ukinzani baina ya kambi za UKAWA na CCM imejidhihirisha katika lugha za kampeni kupitia mbinu za uteuzi wa maneno, vijenzi vya sarufi na tamathali za kibalagha. Matokeo yameonesha zaidi kuwa, kauli zenye kutweza afya ya wagombea, kejeli, kashfa na vitisho zilitumiwa. Pia, kauli zenye kuhimiza amani, mshikamano, kufanya kazi kwa bidii zilisikika. Matumizi ya nafsi ya kwanza "ni-", lugha za mitaani, takriri, jazanda, chuku, misimu, methali, mbazi za kidini, sitiari na vionjo anuwai vya lugha vilifumbatwa iii kufikia malengo hayo. Vilevile, matokeo yameonesha kwamba, mbinu hizi zina dhima ya urembeshaji, ufafanuaji, usisimuaji, uthibitishaji na hata ujikurubishaji kwa hadhira. Pia, imebainika kwamba, mbinu za kisarufi na kibalagha zimeibua athari chanya za kuburudisha, kuhimiza, kuzindua, kujenga matumaini na athari hasi zinazochochea ubaguzi, udhalilishaji, na kujenga uhasama miongoni mwa wanajamii.Utafiti huu umechangia katika taaluma ya uchanganuzi vilongo. Mchango mahususi umejikita katika kubaini sifa za lugha ya kampeni za kisiasa kama rejista maalumu. utafiti huu unapendekeza wazungumzaji katika hotuba za kampeni za uchaguzi wazingatie matumizi mazuri ya lugha yenye kujenga umoja na mshikamno, pia waache kuendeleza matumizi ya lugha zisizo za staha, matusi na kejeli ambazo zinaweza kuchochea migogoro miongoni mwa hadhira wanazozihutubia.
  • Item
    Uchambuzi wa sintaksia ya uambatanishaji katika lugha ya kiswahili
    (University of Dar es Salaam, 2019) Kombe, Luinasia Elikunda
    Tafiti zinaonyesha kwamba lugha nyingi ulimwenguni zinaonekana kuwa na tungo ambatani za aina fulani, ingawa kuna tofauti nyingi za kiisimu Camacho,2003;Haspelmath, 2004; Drellishak,2004; Zhang,2009). Utafiti huu ulilenga kuchunguza sintaksia ya uambatishaji katika lugha ya kiswahili kwa kubainisha viunganishi ambatanishi, kuchambua sintaskia ya viunganishi hivyo na kufafanua mwenendo wa lugha ya kiswahili kuhusu masharti ya uambatanishaji. Data za utafiti huu zilipatikana maktabani katika hotuba ya viongozi, ripoti ya serikali, riwaya na magazeti. Mbinu ya usomaji wa maandiko na ununuzi wa tungo ambatani zilitumika kukusanyia data ambazo zilichambuliwa kiuelezi. Utafiti huu ulitumia mkabala wa kitaamuli na uliongozwa na Nadharia Rasmi Panufu. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kiswahili huambatanisha vipashio vyake kwa kutumia viunganishi ambatanishi dhahiri na viunganishi ambatanishi visivyo dhahiri. Mkato katika maandishi. Viungatanishi ambatanishi hivyo vina dhima ya uongezi,uchaguzi, utebguzi, ukanushi na uwakati. Nafasi ya viunganishi ambatanishi katika tungo ambatani ni tatu. Kwanza, viunganishi ambatanishi ambavyo ni maneno huru huwekwa kati ya viambatanishwa. Pili, kiambishi huwekwa ndani ya kitenzi cha kila kiambatanishwa isispokua kiambatanishwa cha kwanza. Tatu, alama ya mkato inayowakilishwa kiimbo huwekwa baada tu ya kila kiambatanishwa isipokua kiambatanishwa cha mwisho. Baadhi ya viunganishi ambatanishi vya lugha ya Kiswahili huambatanishwa vipashio zaidi ya viwili ilhali vingine huambatanisha vipashio viwili tu. Vilevile, imebainika kua baadhi ya vianganishi ambatanishi huambatanisha katerogia zote za vapashio wakati vingine huambatanisha tu kategoria za vipashio zenye kitenzi ndani yake. Aidha, kuhusu sharti la kuambatanisha vipashio vyenye hadhi sawa, matokeo yanaonyesha kuwa kiswahili huambatanisha vipashio vyenye hadhi sawa kinyume na madai yaliyoyolewa na De Vos na Riedel(2017) kuwa kiswahili huambatanisha vipashio visivyo na hadhi sawa. Vilevile, kuhusu shartizuizi la tungo ambatani, matokeo yanaonyesha kuwa linaakisiwa katika lugha ya kiswahili. Hii ni kwa sababu viulizi vya Kiswahili huwa havioneshi uhamishaji wa vipashio bali hukaa mahali pa kawaida pa vipashio husika,kiambatanishwa cha mwisho katika tungo ambatani kinaweza kufanywa kuwa swali jambo ambalo ni kinyume na sharti hilo. Hii inaonesha kuwa ni vigumu kuwa na kanuni moja inayoakisiwa katika lugha zote kwa sababu kila lugha ina upekee wake. Matokeo haya yanamchango mkubwa katika kuonesha upekee wa lugha ya kiswahili katika uwanja wa umbatanishaji. Hivyo, utaiti huu unapendekeza tafiti zaidi kuhusu sintaksia ya uambatanishaji katika lugha za kibantu ili kuonesha upekee wa lugha hizi katika uwanja huu wa uambatanishaji. Kinadharia, utafiti huu umethibitisha kwamba suala la muundo wa ndani na muundo wa nje wa tungo bado lina mashiko katika uchambuzi wa lugha kwa sababu baadhi ya tungo zinazotumika katika mawasiliano ni matokeo ya mageuzi yaliofanyika katika miundo ya ndani ya tungo hizo. Hivyo bni vigumu kupata matokeo sahihi kwakuchunguza miundo ya nje pekee bila kuhusisha miundo ya ndani.
  • Item
    Uumbaji Wa Ualbino Katika Fasihi Ya Kiswahili; Uchambuzi Wa Kazi Teule
    (Chuo Kikuu cha Dar es salaam, 2019) Mahenge, Elizabeth Godwin
    Utafiti huu ulihusu uchambuzi wa kazi teule katika fasihi ya Kiswahili ili kuona namna uumbaji wa albino unavyofanyika. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi manne ambayo ni kubainisha imani zinazoumba ualbino katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili; kuelezea dhima ya msimulizi zinazotumiwa kuumba ualbino katika kazi teule.Utafiti ulihusisha kazi nane za fasihi ya Kiswahili ambazo ni Takadini, Nje Ndani, Zindera, Baba Ne-Musa “Mimi Albino”, Wimbo wangu Albino”, “Albino” na “Mauaji ya Albino,” Mbinu ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika ili kupata matokeo ya utafiti huu. Mbinu hii ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika ili kupata matokeo ya utafiti huu. Mbinu hii ya uchambuzi iliongozwa na Nadharia ya Naratolojia. Nadharia hii inahusika kuchunguza namna usimulizi unavyofanywa katika simulizi.Utafiti unafuata mkabala wa Bal ambao unaona kuna usimulizi kaitika kila kitu. Data zilipatikana baada ya kusoma kwa kina kazi teule pamoja na kufanya mahojiano kwa ajili ya utafiti wa awali wa utafiti huu. Mkabala uliotumika katika uchambuzi wa data ni wa kitaamuli ambao ni wa kimaelezo na uliwezesha kupatikana kwa matokeo ya utafiti huu. Kwanza , utafiti umebaini kuwa kuna imani mbalimbali zinazoelezea asili ya kuzaliwa motto mwenye ualbino. Imani hizi zinatokana na visasili vilivyopo katika jamii.Pili, utafiti umebaini kuwa , msimulizi anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiubaguzi na kiunyanyapaa kwa upande mmoja; na pia anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiujumuishwaji kwa pande mwingine.Tatu, utafiti umebaini kuwa msimulizi anajititokeza kwa dhima ynne ambazo ni kusimulia kuwasiliana, kukosoa na kutekeleza itikadi. Katika dhima hizi, msimulizi anawezakuwa hai (akishiriki katika kusimulia) au tuli( akijenga kusimulia), Nne, utafiti umebaini kuwa , sauti za usimulizi zinatumika kwa makusudi maalum ambayo ni ama kuunga knono jambo Fulani au kulipinga. Matumizi ya nafi ya kwanza nay a pili yanaonesha kuunga mkono jambo; wakati matumizi ya nafsi ya tatu yanaonesha kulipinga. Mapendekezo yanayotolea na utafiti huu ni kufanya utafiti mwingine katika kumbo mahususi za fasihi ili kuona namna ualbino kwa umahususi na ulemavu kwa ujumla unavyoumbwa katika kumbo hizo Vilevile utafiti unapendekeza nadharia ya Naratolojia itumiwe zaidi na wachambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuwa inamwezesha mchambuzi kuufahamu uhalisia wa simulizi kupitia nafsi mahususi zinazotumika katika kusimulia.Nadharia hii iko karibu na uhalisia.
  • Item
    Uumbaji wa ualbino katika fasihi ya kiswahili: uchambuzi wa kazi teule
    (University of Dar es Salaam, 2019) Mahenge, Elizabeth Godwin
    Utafiti huu ulihusu uchambuzi wa kazi teule katika fasihi ya kiswahili ili kuona namna uumbaji wa ualbino unavyofanyika. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi manne ambayo ni: kubainisha imani zinazoumba ualbino katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili; kuchambua jinsi lugha inavyoumba ualbino katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili; kuelezea dhima ya msimulizi anayesimulia hadithi ya ualbino katika kazi teule; na kujadili sauti za usimulizi zinazotumiwa kuumba ualbino katika kazi teule. Utafiti ulihusisha kazi nane za fasihi ya Kiswahili ambazo ni: Takadini, Nje Ndani, Zindera, Baba Ne-Musa!,"Mimi Albino", "Wimbo Wangu Albino" "Albino", na "Mauaji ya Albino". Mbinu ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika ili kupata matokeo ya utafiti huu. Mbinu hii ya uchambuzi iliongozwa na Nadharia ya Naratolojia. Nadharia hii inahusika kuchunguza namna usimulizi unavyofanywa katika simulizi. Utafiti unafuata mkabala wa Bal ambao unaona kuna usimulizi katika kila kitu. Data zilipatikana baada ya kusoma kwa kina kazi teule pamoja na kufanya mahojiano kwa ajili ya utafiti wa awali wa utafiti huu. Mkabala uliotumika katika uchambuzi wa data ni wa kitaamuli ambao ni wa kimaelezo na uliwezesha kupatikana kwa matokeo ya utafiti huu. Kwanza, utafiti umebaini kuwa kuna imani mbalimbali zinazoelezea asili ya kuzaliwa mtoto mwenye ualbino. Imani hizi zinatokana na visasili vilivyopo katika jamii. Pili, utafiti umebaini kuwa, msimulizi anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiubaguzi na kiunyanyapaa kwa upande mmoja; na pia anatumia tamathali za usemi ili kuumba ualbino kiujumuishwaji kwa upande mwingine. Tatli, utafiti umebaini kuwa msimulizi anajitokeza kwa dhima nne ambazo ni kusimulia, kuwasiliana, kukosoa na kutekeleza itikadi. Katika dhima hizi, msimulizi anaweza kuwa hai (akishiriki katika kusimulia) au tuli (akijitenga kusimulia). Nne, utafiti umebaini kuwa, sauti za usimulizi zinatumika kwa makusudi maalumu ambayo ni ama kuunga mkono jambo fulani au kulipinga. Matumizi ya nafsi ya kwanza na ya pili yanaonesha kuunga mkono jambo; wakati matumizi ya nafsi ya tatu yanaonesha kulipinga. Mapendekezo yanayotolea na utafiti huu ni kufanya utafiti mwingine katika kumbo mahususi za fasihi ili kuona namna ualbino kwa umahususi na ulemavu kwa ujumla unavyoumbwa katika kumbo hizo. Vilevile utafiti unapendekeza Nadharia ya Naratolojia itumiwe zaidi na wachambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuwa inamwezesha mchambuzi kuufahamu uhalisia wa simulizi kupitia nafsi mahususi zinazotumika katika kusimulia. Nadharia hii iko karibu na uhalisia.
  • Item
    Majukumu ya wahusika kijinsia katika nyimbo za watoto za Kiswahili na uhalisia wake katika malezi ya watoto nchini Tanzania
    (Chuo kikuu cha Dar es Salaam, 2019) Mosha, Doroth Felician
    Tasnifu hii ni matokeo ya mada ya utafiti ‘’ Majukumu’’ ya wahusika kijinsia katika nyimbo za watoto za Kiswahili na Uhalisia wake katika Malezi ya watoto nchini Tanzania’’ Tum’echunguza namna watunzi wa nyimbo za watoto walivyowateua wahusika kuwapa majukumu anuwai kwa mujibu wa jinsi zao. Vilevile, tumechambua maoni ya wanajamii (walimu, wanafunzi na wataalamu wa masuala ya jinsia) kuona namna wanavyogawanya majukumu kwa watoto wanapowatia malezi. Lengo ni kufanya ulinganishi ili kuona endapo kuna uhalisia wa majukumu ya kijimsia katika nyimbo za watoto na malezi ya watoto nchini Tanzania. Utafiti uliongozwa na malengo muhususi manne: Mosi, kubainisha wahusika waliojitokeza katika nyimbo za watoto kwa mujibu wa jinsi zao. Pili, kuchambua majukumu ya wahusika hao. Tatu, kujadili moni ya jamii kuhusu majukumu ya kijinsia katika malezi ya watoto na kulinganisha na yale ya nyimbo za watoto kwa watoto na jamii. Data zilizokusanywa kwa njia ya mahojiano, ushuhudiaji na maandiko mbalimbali ziifanikisha malengo tajwa. Data hizi zimewasilishwa na kuchambuliwa kwa njia ya kitaamuli kukiwa pia na matumizi ya uchambuzi wa kitakwimu na majedwali. Utafiti umeongozwa na nadharia za Skima ya kijinsia na uhalisia. Skima ya kijinsia ni nadharia ya mrengo wa jinsia inayoangazia namna mtoto anavyojifunza majukumu yanayomhusu kwa kuhushudia yale yanayofanywa na wanaume na wanawake wakiongozwa na utamaduni wa jamii husika. Nadharia ya uhalisia imezingatia ukweli na uyakinifu wa majukumu ya kijisnisia katika malezi ya watoto kama yalivyosawiriwa katika nyimbo za watoto ili kubaini kufanana na kutofautiana kwake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa: Mosi, wahusika wa kike ni wengi kuliko wahusika wa kiume na wamebebeshwa majukumu mengi. Pili, watunzi wa nyimbo za watoto wamesawiri mgawanyo sawia wa majukumu ya kijinsia ya wahusika. Tatu, maoni ya wanajamii yamebaini kutokuwa na unyoofu wa mgawanyo wa majukumu ya kijinsia katika malezi ya watoto. Hali hii huchangiwa na tofauti za kiutamduni na malezi ya kifamilia, mitazamo na itikadi tofauti, dini, elimu, tofauti za kihistoria na hatua ya maendeleo ilivyofikiwa katika familia au jamii husika. Hivyo, hakuna usahili wa kiuhalisia baina ya majukumu ya wahusika kijinsia katika za watoto na majukumu ya wahusika kijisinsia katika nyimbo za watoto umebainika kuwa na athari chanya na hasi kwa watoto na jamii.
  • Item
    Ulinganishi wa lugha za ‘’Runyaċitara’’
    (Chuo kikuu cha Dar es Salaam, 2019) Asiimwe, Caroline
    Utafiti, huu ulihusu ulinganishi wa lugha za ‘’Runyaċitara’’ ili kufanunua kama zina uhusiano wa kimnasaba baina yake au la. Malengo mahususi yaliyoshughulikiwa ni kubainisha historia ya lugha hizi, kufanunua kutofautiana na kufanana kulikopo kati ya lugha hizi na tatu ni kutathmini kama hizi ni lugha moja, makundi mawili au kila lugha inajitegemea. Nadharia ya mwanachano na Makutano ya lugha za kibantu na nadhariatete yake ya ndugu na ndugu wa mbali kiisimu ambazo ziliasisiwa na Massamba (2007) zimetumiwa kueleza historia ya lugha hizi pamoja na kutathamini uhusiano wa lugha hizi kwa kuegemea kiwango cha ukaribu kiisimu. Aidha, ya Isimu historian na linganishi ambayo mwasisi wake ni William Jones 1786 imetumiwa kuelezea vipengele vya kiisimu na msamiati wa msingi kisinkroniki na kidikronuki. Mikabala mchanganyiko imetumiwa katika utafiti huu, na maeneo ya utafiti yamehusisha Wilaya za Kabarole, Hoima, Mbarara na Kabale ambazo zimo nchini Uganda. Vilevile, usampulishaji hatua ulitumiwa kuchagua maeneo mahususi na watoa taarifa kimaksudi na pia kwa kutumia usampulishaji tajwa. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, kuptia maandiko, mahojiano, uthibitishaji kauli na usaili. Data hizi zilihusu historia ya wazungumzaji na lugha zaopamoja na taarifa za kiisimu; msamiati wa msingi, mfumo wa sauti na sauti mrejeo, mofolojia, ngeli za nomino na hali na njeo ili kufanunua uhusiano wa lugha hizi. Data zimechanganuliwa kwa kutumia mbinu linganishi, takwimu leksika, maelezo na programu ya ‘linganishi lugha kwa mfumo wa kompyuta’. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo nay a kitakwimu ili kuelezea uhusiano wa lugha za ‘’Runyacitara’’. Matokeo yanaonesha kwamba hizi ni lugha zenye mnasaba ambazo zilitokana na mame- lugha moja. Lugha hiz zinajibainisha katika makundi mawili ya Runyoro na Rutooro na kundi la Runyankore na Ruċiga kutokana na mabadiliko ya lugha na kila kundi ni ndugu ya mbali kwa kundi jingine. Hali ya lugha hizi tunayoiona leo hii inaweza kufafanuliwa kidikroniki kama matokeo yanavyoonesha mabadiliko ya lugha yaliyotokea kiisimu. Kwa upande mwingine, kwa sababu yawazungumzaji kutaka kujibainisha kama watu wa jamii tofauti huwa wanaibuka na miundo mipya ili kujitofautisha na wenzao. Hitimisho ni kwamba lugha hizi zina uhusiano wa kimnasaba kwa kuhusisha mfanano wa 85.39% katika msamiati wa msingi na vipengele vingine vya kiisimu. Matokeo ya uundaji upya yalionesha kwamba maumbo tunayoyaona leo hii ya;itokana na maumbo ya awali. Kwa hivyo, lugha hizi ni kundi moja la lugha lenye makundi ndani mwake ambayo ni lahaja. Matokeo haya yana mchango mkubwa katika kufafanua uhusiano wa lugha za Runyoro, Rutooro, Runyankore na Ruċiga kwa kuegemea historia ya wazungumzaji wake na maendelo ya lugha kiisimu, nadharia, utafiti umethibitisha kwamba hali ya lugha kisinkronia inaweza kufafanuliwa kidikronia na vilevile kuthibitisha kwamba mijongeo ya watu inaweza kusababisha mwanachano na makutano ya lugha. Aidha, matokeo yanachangia katika data za kisiimu za lugha za kibantu na nadharia ya isimu kwa ujumla pamoja na data zilizoko makavazini. Inapendekezwa kuwe na utafiti zaidi juu ya; lugha nyingine zinazoonesha mfanano na hizi; nafasi ya teknolojia katika mwachano na makutano ya lugha; athari ya uhusiano wa lugha hizi katika vipengele vingine vya kijamii na vipengele mahususi vya kiisimu katika lugha hizi. Aidha, kuna haja ya kuwa na usanifishaji wa mfumo rasmi wa ‘’Runyaċitara’’.
  • Item
    Ruwaza za toni katika vitenzi na nomino za kirombo
    (University of Dar es Salaam, 2020) Mramba, Peter Thobias
    Utafiti huu unahususu Ruwaza za Toni katika Vitenzi na Nomino za Kirombo. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ruwaza za ujitokezaji wa toni katika vitenzi na nomino za Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya tonolojia. Utafiti ulifanyikia katika Vijiji vya Mengwe Juu na Mengwe Chini, Kata ya Mengwe, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Wango la utafiti ni nomino na vitenzi na wazungumzaji wazawa wa Kirombo. Aidha, mbinu ya usampulishaji iliyotumika ni Nasibu Tabakishi. Pia, Mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni: mahojiano na ushuhudiaji. Katika mahojiano nomino na vitenzi viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuyatamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika maneno hayo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwepo au kutowepo kwa yambwa. Kwa vitenzi na nomino za silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa tonichini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi na nomino za silabi tatu hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja. TJM katika vitenzi na nomino za silabi moja ya shina hubiruka nyuma na khupachikwa katika kiambishi awali kwa nomino na vitenzi visoukomo sahili, wakati TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina. Pia, kwa upande wa vitenzi visoukomo sahili matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi. Aidha, inapendekezwa tafiti fuatizi zifanyike katika viwango vya kirai na sentensi, uradidi katika nomino na vitenzi na tonolojia linganishi katika jamiilugha za Kichaga. Utafiti huu umesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika Kirombo kwa ujumla.
  • Item
    Nafasi ya lugha ya kiswahili katika mandhari- lugha ya jiji la Mbeya nchini Tanzania
    (University of Dar es salaam, 2020) Kawonga, Gervas
    Utafiti huu ulihusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Lengo kuu lilikuwa kuchunguza nafasi ya lugha ya Kiswahili katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Malengo mahususi yalikuwa matatu: kwanza, kubainisha ruwaza za lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Pili, kudhihirisha nafasi ya lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia ruwaza za lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Tatu, kuwianisha sera ya lugha ya Tanzania na nafasi ya lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu yenye msingi kwamba katika jamii kuna vipengele vya kimfumo na kiitikadi vinavyosababisha uhusiano usio wa usawa miongoni mwa lugha za jamii mbalimbali. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya upigaji wa picha za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu na mbinu ya usaili. Uchambuzi wa data za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu ulifanyika kwa mbinu ya usomaji wa matini na Programu Tarakilishi ya Takwimu (PTT). Uwasilishaji wa data umefanyika kwa kutumia vielelezo vya majedwali, grafu na picha kwa data za kiidadi za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu. Nukuu za usaili na ufafanuzi wa kinathari umetumika kwa data za kitaamuli. Matokeo yanaonesha kwamba kuna ruwaza nne za lugha katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Ruwaza zilizobainishwa ni Kiswahili pekee, Kiingereza pekee, Kiswahili-Kiingereza na Kiingereza-Kiswahili. Kiswahili kinajitokeza kwa asilimia 54.5 katika ruwaza ya Kiswahili pekee mbele ya Kiingereza. Kwa kigezo cha ukubwa wa maandishi Kiswahili kinajitokeza cha kwanza kwa asilimia 63 kwa maandishi makubwa zaidi kuliko Kiingereza. Vilevile, kwa kigezo cha idadi ya maneno Kiswahili kinajitokeza katika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 72.23. Kwa hiyo, Kiswahili kinajitokeza katika nafasi ya kwanza kimatumizi katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Aidha, kuna uwiano baina ya Sera ya Lugha ya Tanzania na nafasi ya matumizi ya lugha katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya. Hata hivyo, tunapendekeza serikali ifanye mapitio ya sera ya lugha ili kuunda kanuni za matumizi ya lugha katika mandhari-lugha na kuweka urari wa matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, tafiti fuatishi zifanyike kwa kuchunguza mabango ya makampuni mahususi tofautitofauti ili kupanua uelewa kuhusu ruwaza za lugha, nafasi ya Kiswahili na uwiano wa nafasi ya matumizi ya lugha na Sera ya lugha ya Tanzania.
  • Item
    Synthesis of anthraquinone based dyes from anacardic Acid component of cashew nut shell liquid (CNSL) for Textiles applications
    (University of Dar es salaam, 2020) Nambela, Lutamyo
    The aim of this study was to develop a method for the synthesis of anthraquinone based dyes from anacardic acid isolated from CNSL and then to test the performance of the synthesised dyes on textile fabrics. CNSL was extracted in 20% yield from CNSs using petroleum ether as the solvent. Anacardic acid was then isolated from CNSL through the addition of Ca(OH)2 to form calcium anacardate and then acidification with HCl to recover the anacardic acid in 64% yield. With anacardic acid in hand, a procedure was developed for its conversion to phthalic anhydride and then anthraquinone dyes. Conversion of anacardic acid to a 3-methoxyphthalic anhydride in overall yield of 9% involved methylation of the two hydroxyl groups, alkene reduction, benzylic bromination, elimination of HBr, ozonolysis, oxidation and acid anhydride formation. The prepared 3-methoxyphthalic anhydride was subsequently reacted with benzene and substituted benzenes in the presence of AlCl3 to give three anthraquinone dyes or dye intermediates namely 1-hydroxyanthraquinone, 7-bromo-1-hydroxyanthraquinone and 1,7-hydroxyanthrquinone in 40%, 39% and 15% yields, respectively. Subsequently, 1-aminoanthraquinone was prepared in 80% yield from 1-hydroxyanthraquinone. Dimerisation of 1-aminoanthraquinone gave indanthrone in 93%. The prepared dyes were characterised using melting point measurements, UV, IR, NMR and mass spectrometry. The three prepared anthraquinone dyes were tested on 100% polyester fabric while the indanthrone dye was tested on 100% cotton fabric. 1-hydroxyanthraquinone and 7-bromo-1-hydroxyanthraquinone dyes gave yellow shade on the fabric, while 1-aminoanthraquinone gave an orange shade. Indanthrone on the other hand gave blue shade on 100% cotton fabric. The affinity of the dyes to the fabrics were determined using colour yield values which were measured using a reflectance spectrophotometer. All the dyes showed high affinity to dyed fabrics and this demonstrates that CNSL has a potential as a source of a precursor of intermediates in the synthesis of dyes.
  • Item
    Ujitokezaji wa tashtiti katika fasihi ya Kiswahili: Uchunguzi wa kazi teule
    (University of Dar es Salaam, 2019) Daniel, Zawadi Limbe
    Utafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili ukiongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha mbinu zinazotumika kuunda tashtiti, kueleza dhima ya tashtiti na kuainisha tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Uchunguzi wa ujitokezaji huu ulifanywa kupitia kazi teule za fasihi ya Kiswahili za: Kaptula la Marx 9Kezilahabi, 1999), Amezidi (Mohamed, 1995), Walenisi (Mkangi, 1995), na Miradi Bubu ya Wazalendo (Ruhumbika, 1992). Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchambuzi matini na mkabala wa kitaamuli. Aidha nadharia za semiotiki-jamii na Mwingiliano- matini ziliongoza utafiti huu. Matokeo katika utafiti huu yanaonesha tashtiti katika kzi teule ni mtindo wa kisanaa unaoundwa kwa kutumia mbinu za dhihaka, kejeli, ufyosi, matumizi ya tamadhali ya usemi hasa sitiari, tashbiha na uchuku ubeuzi, taswira na ishara, mandhari pamoja na ujenzi wa wahusika. Matokeo haya yanapingana na madai yaliyokwishatolewa na Msokile (1992), Mbonde (2002), Senkoro(2011), na Wamitila (2003) kwamba tashtiti katika fasihi ya Kiswahili hujitokeza kama kipengele cha kitamathali pekee, madai ambayo yalichukulia tashtiti kuwa kipengele kinachofungamanishwa na matumizi ya lugha pekee. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa tashtiti ni dhana pana, ambayo katika kujipambanua kwake inatumia si tu vipengele vya lugha na kitamathali, bali pia mbinu mbalimbali za kifani na kimaudhui. Vilevile, matokeo yanaonesha kuwa tashtiti ina dhima kuu tatu katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili. Dhima hizi ni za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Katika dhima ya kisiasa tashtiti inahakiki uongozi, inakemea rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, inapinga ukoloni mamboleo na utegemezi wa misaada, na inatathimini utoaji wa haki na usawa. Katika dhima ya kiuchumi tashtiti inaumbua hali ya umaskini, na inashambulia hali ya utabaka. Kijamii tashtiti ina dhima ya kukosoa mfumo wa elimu, kuhakiki utamaduni na maadili na pia kuumbua hali duni za afya na uzazi . Aidha utafiti huu umependekeza aina tano za tashtiti ambazo ni tashtiti ya mtindo jumuishi, tashtiti –tamathali, tashtiti-husika, tashtiti-ufyosi na tashtiti-fiche. Kutokana na matokeo ya utafiti huu uainishaji huu ndiyo unafaa kumika katiak kazi za fasihi ya Kiswahil
  • Item
    Uchanganuzi Kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya bunge la Tanzania
    (University of Dar es Salaam, 2016) Sylivester, Johanes
    Utafiti huu unahusu uchanganuzi kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya BJMT katika kipindi cha mwaka 1980 hadi 2014.Data ilikusanywa kwa mbinu za uchambuzi wa nyaraka, ushuhudiaji, hojaji na usaili na kuchambuliwa na kufasiriwa kwa mkabala wa uchanganuzi kilongo shirikishi na mpishano huru. Walengwa wa utafiti walikuwa Wabunge wa BJ MT. Nadharia iliyotuongoza ni Nadharia ya Staha ya Brown na Levmson (1987) inayodai kuwa , kuna kauli zenye kutweza staha na iii kauli hizo zikweze staha mzungumzaji anatakiwa kuzisuka kwa kutumia mbinu faafu za kistaha. Pia, tulizingatia maboresho ya Fraser (1990) anayedai kuwa ili mzungumzaji akweze staha lazima azungumze kwa kuzingatia kanuni zinazodhibiti majadiliano. Kutokana na uchanganuzi kilongo uliozingatia vipengele vya kinadharia, kanuni za Bunge na muktadha wa mazungumzo data tuliyoipata imetupa vipengele vinavyohusiana na kauli zenye kutweza au kukweza. Miongoni mwa kauli hizo ni matusi, kumshambulia Mbunge kuwa ni mnafiki au sio makini, kusema uongo, kuhamasisha uvunjifu wa sheria, kuonesha kuwa wenzio ni punguani, vichaa au wendawazimu, kujivuna au kubeza wengine, kumpa taarifa Spika (Kiti) au kutotii maelekezo yake, kutotumia neno 'Mheshimiwa' kabla ya jina la Mbunge, kauli za kibaguzi na mwisho kuzungumzia mambo ya siri ya Mbunge. Kwa upande wa kauli zenye kukweza staha, utafiti unaweka wazi kuwa ili zijitokeze ni lazima mzungumzaji ateue mbinu faafu za kistaha zitakazomwezesha kulinda utu wa wasikilizaji pamoja na makatazo yanayodhibiti matumizi ya lugha Bungeni. Mbinu hizo ni pamoja na ubadili haji msimbo, matumizi ya kauli ya kutendwa na kutendana, kunukuu, matumizi ya nafsi ya kwanza wingi, matumizi ya vitambulisho hadhi, uteuzi mzuri wa msamiati, matumizi ya njeo ya wakati uliopita //-Ii-// mahali pa wakati uliopo //-na-// wakati wa kuuliza swali na uepukaji. Kwa ujumla, utafiti umeonesha kuwa, uwepo wa kauli zenye kutweza staha Bungeni unatokana na kutotumia mbinu faafu za ki taha. Matokeo ya utafiti huu yanachangia maarifa mapya katika taaluma ya isimu-tumizi Y . Kiswahili hasa katika taaluma za pragmatiki, isimujamii na elimu-mitindo. Pia, yanachangia katika kipengele cha uchanganuzi kilongo kwa kupendekeza mbinu za uchanganuzi kilongo shirikishi na uchanganuzi kilongo mpishano huru kama mbmu za kuchambua na kufasiri data. Kipekee kabisa, utafiti huu unachambua kwa undani kipengele cha staha ambacho ni cha pragmatiki katika mijadala ya Bunge ili kuweza kupata ruwaza za lugha ya kibunge zenye kukweza staha. Ili kubainisha ruwaza za lugha ya kibunge tunapendekeza utafiti zaidi utakaobainisha vipengele vya kiisimu vinavyounda lugha hiyo. Pia, kuhusu mbinu za kistaha katika lugha ya Kiswahili kwa ujumla , tupendekeza tafiti nyingine kufanyika kwenye taasisi nyingine pia na katika mazmgua yasiyo rasmi.
  • Item
    Uchanganuzi wa upinduzi wa kimahali katika lugha ya Kiswahili
    (University of Dar es Salaam, 2019) Hassan, Fabiola
    Kwa kawaida kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na za kisarufi za viambajengo vya sentensi. Uhusiano huo ni kwamba kiambajengo chenvc dhima ya kisemantiki inayotokea katika nafasi ya juu ndicho kinapaswa kuwa kiimacha sentensi. Upinduzi wa kimahali ni mchakato unaoibua changamoto katika uhusiano huo. Changamoto iliyopo ni kwamba kimahali ambacho kinatokea katikanafasi ya chini katika udarajia wa dhima za kisemantiki, kinapandishwa hadhi na kuwa kiima hata kama katika tungo kuna kiambajengo kinachopaswa kuwa kiima ikilinganishwa na kimahali. Aidha, licha ya kufanyika tafiti katika lugha nvingine za Kibantu na Kiswahili, kuna masuala hayakufafanuliwa kwa uwazi, mengine yalikuwa na utata, na mengine yalionekana kutofautiana kati ya lugha moja na nyingine.Mathalani, ilielezwa kwamba lugha ina ama tungo zenye upinduzi wa kimahali chakimofolojia au zile zenye upinduzi wa kimahali cha kisemantiki. Pamoja na kuclezwa hivyo, haikuelezwa iwapo lugha moja inaweza kuwa na aina zote mbili za tungo. Hivyo, tatizo la ukiukwaji wa uhusiano wa udarajia wa dhima za kisemantiki na zakisarufi za viambajengo vya sentensi pamoja na masuala ambayo hayakufafanuliwa kwa uwazi katika tafiti zilizopita, kuliibuka haja ya kufanya utafiti unaoripotiwa katika tasinifu hii. Utafiti huu umechanganua Upinduzi wa Kiniahali katika Lugha ya Kiswahili. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi manne. Mosi, kubainisha aina za tungo zenye upinduzi wa kimahali, vitenzi vinavyoruhusu na vile visivyoruhusu utokeaji wa tungo hizo. Pili, kubainisha vimahali vinavyoweza na vile visivyoweza kupinduliwa katika tungo. Tatu, kufafanua dhima za kisarufi za viambajengo vinavyohusika katika tungo zisizo na upinduzi wa kimahali na zile zenye upinduzi huo. Mwisho, kufafanua muundo wa taarifa na umuhimu wa kimawasiliano wa tungo zenye upinduzi. Uchanganuzi wa data umetumia misingi ya mkabala wa Saruti Leksia Amilifu ulioasisiwa na Bresnan na Kaplan mwishoni mwa miaka ya 1970. Utafiti ulifanyika katika Idara za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Data zilikusanywa kutoka katika vitabu 2 pamoja na watoataarifa 40. Data zilipatikana kwa njia za usomaji wa nyaraka, ushuhudiaji shiriki, upimaji wa usahihi wa kisarufi, usaili, na hojaji. Matokeo yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inatungo zenye mapinduzi wa kimaana cha kimoforojia na zile zenye upinduzi wa kimaana yake na kithimu na kimahali. Na mtenda ambayc hajapinduliwa ni kiima, na aliyepinduliwa ni chagizo. Kuhusu muundo wa taarifa, katika tungo zenye upinduzi mada ni kimahali kilichopinduliwa na fokasi ni kithimu kilichopinduliwa. Aidha, tungo zenye upinduzi wa kimahali zina umuhimu wa umadaishaji wa kimahali, ufokalishaji wa kithimu, na ufokalishaji linganuzi wa kithimu. Kutokana na matokeo haya, inapendekezwa kwamba kufanyike utafiti kama huu katika lugha nyingine za Kibantu ambazo hazijafanyiwa utafiti iii kulinganisha na kulinganua ruwaza za upinduzi wa kimahali baina ya Kiwahili na lugha nyingine.
  • Item
    Ulinganishi wa Kiisimu wa “Lugha” za kibantu za Mara Kaskazini
    (University of Dar es Salaam, 2019) Boniphase, Alphonce Morango
    Utafiti huu unahusu "Ulinganishi wa Kiisimu wa "Lugha" za Mara Kaskazini" ili kubaini karna ni lugha zinazojitegemea au ni lahaja tu za lugha moja kuu ya awali. ''Lugha" za Mara Kaskazini zilizolinganishwa ni Kikurya, Kisimbiti, Kikiroobha, Kisweeta, Kikabwa, Kisuba, Kikine na Kikenye. Utafiti huu una malengo mahsusi mawili: kubainisha mfanano na tofauti ya vi gezo vya kiisimu ambavyo ni msamiati wa msingi , mfu mo wa sauti, mfurno wa ngeli , mfumo wa njeo na mfumo wa ukanushi . Lengo la pili ni kuanisha kiwango cha uhusiano kilichopo kinachoweza kubainisha karna ''lu gha" za Mara Kaskazini ni lugha au lahaja. Utafiti urneongozwa na nadharia kuu mbili ambazo ni Nadharia ya Mwachano na Makutano ya Lugha za Kibantu pamoja na nadhariatete ya Ndugu na Nd ugu wa Mbali i liyoasisi wa na M assamba mwaka 2007. Nadharia ya pili ni Isimu Historia-Linganishi i liyoasisi wa na Jones rnwaka 1786. Utafiti huu unategemewa kuwa na umuhi mu kwa wanaisi rnu na wanajami i wal iokuwa wanatatizika kuhusu "lugha" hizi na wale wote wenye kiu ya kutaka kujua namna ya kulinganisha lugha mbalimbali kiisirnu. Aidha, data zautafiti huu zilipatikana uwandani kwa kuhusisha mbinu mbal imbali za utafiti arn bazo nikusikiliza, usaili , hojaji na majad iliano katika majopo. Eneo la utafiti lilihusisha vijiji 14 kutoka katika Wilaya za Tarime, Rorya, Butiama, Musoma Mjini na Musoma Vijijini. Matokeo ya utafiti huu yamedhihi risha kuwa "lugha" zilizolinganishwa si lugha zinazojitegemea, bali ni lahaja zilizotokana na lugha moja ya awali . "Lugha" hizi zimeonesha mfanano wa zaidi ya asilimia sabini (70%). Mfanano huo umezigawa "lugha" hizi katika makundi mawili: kundi la "lugha" za Kikurya, Kisimbiti, Kisweeta, Kikine na Kikenye na kundi la "lugha" za Ki kabwa, Kisuba l na Kikiroobha.Tunapendekeza tafiti zaidi zifanywe katika vipengele kadhaa vya ki isimu ambavyo havikushughulikiwa katika utafiti huu. V ipengel e hivyo, ni kama vile kipengele cha toni. Kipengele hiki kimeonekana kuwa changamani katika "lugha" za Mara Kaskazini, kimeonesha kutofautisha njeo, hivyo kina athari katika matamshi. Suala lingine ni kukosekana kwa "lugha" ya Kishashi, mojawapo ya "lugha" zilizopangwa kuchunguzwa katika utafiti huu lakini haikuwepo kat ika mazingira hal isi kule uwandani na wala wazungumzaji wake, japokuwa eneo la Ushashi lipo.
  • Item
    Mandhari na usawiri wa ukimwi katika riwaya ya kiswahili 2000-2010
    (University of Dar es Salaam, 2016) Bulaya, Joviet
    Utafiti huu umechunguza jinsi ugonjwa wa UKIMWI unavyosawiriwa katika fasihi kwa kuiangalia riwaya ya Kiswahili kupitia katika kipengele cha mandhari. Utafiti unalenga kujibu maswali yafuatayo: kwanza, ni jinsi gani mandhari ya riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI inafungamana na dhamira zinazosawiriwa na riwaya husika? Pili, riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI inatumiaje mandhari kuumba wahusika wake? Na mwisho, waandishi wa riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI wanatumiaje mandhari kujenga lugha inayoibua athari na changamoto za UKIMWI katika riwaya zao? Sambamba na maswali hayo, tumefafanua malengo ya utafiti huu kuwa ni: mosi, kujadili jinsi mandhari inavyofungamana na dhamira zinazoelezwa na riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI. Pili, kueleza jinsi riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI inavyotumia mandhari kuumba wahusika wake. Na tatu ni kubainisha namna waandishi wa riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI wanavyotumia mandhari kuumba lugha inayoibua athari na changamoto za UKIMWI katika riwaya zao. Ili kufikia kusudi la utafiti huu , tumetumia mbinu mbalimbali za utafiti zikiwamo za utafiti wa nyaraka na mahojiano. Mbinu hizi kwa pamoja zimetumika kukusanya data zilizosaidia kujibu maswali ya utafiti huu. Nadharia ya Mwingiliano-matini ndiyo imeongoza utafiti huu. Nadharia hii inasisitiza kuwa hakuna matini asilia, bali uhai wa matini moja hutegemea matini nyingine. Kwa hiyo, matini za kifasihi hutegemeana katika kukamilisha maana. Kwa kutumia nadharia hii tumeona kuwa, mandhari zinaingiliana, kukamilishana na kutegemeana katika kuliumba tatizo la UKIMWI. Hii inatokana na ukweli kuwa, riwaya zinazochunguzwa zimetumia mandhari mbalimbali kuwaumba wahusika, kuibua dhamira na kuchomoza lugha inayoelezea athari na changamoto za UKIMWI. Kutokana na utafiti huu, upo uhusiano mkubwa kati ya mandhari na uibuaji wa dhamira za kazi ya fasihi. Pili, kuna uhusiano kati ya mandhari na ujenzi wa wahusika. Wasifu, tabia na mienendo ya wahusika wa riwaya teule kwa sehemu kubwa ni matokeo ya mandhari wanamokuwa. Vilevile, mandhari inahusiana na lugha kwani, lugha inayotumiwa na wahusika katika riwaya inategemea mandhari wanamokuwa. Hii inathibitisha kuwa, mandhari ina umuhimu mkubwa katika kuibua dhamira, kuwaumba wahusika pamoja na kutolea ujumbe uliokusudiwa katika kazi ya fasihi hasa riwaya. Kutokana na uchunguzi wa riwaya teule, kazi ya fasihi hasa riwaya haikamilishwi na mandhari moja, bali upo mwingiliano mkubwa wa mandhari mbalimbali ambao unaifanya riwaya ikamilishe maana na kusudi la mwandishi. Na kwa hiyo, mandhari ni mojawapo ya mihimili muhimu katika kuumba maana ya kazi ya fasihi.
  • Item
    Michakato ya kisemantiki kwenye maneno ya mkopo katika kiswahili: mifano kutoka Kiingereza na Kiarabu
    (University of Dar es Salaam, 2017) Shembilu, Musa Mohamed
    Kiswahili kama zilivyo lugha nyingine kimekopa maneno kutoka lugha mbalimbali. Miongoni mwa lugha hizo ni Kiingereza na Kiarabu. Maneno hayo yanapoingia katika Kiswahili huchakatwa katika viwango mbalimbali vya kiisimu kama vile kifonolojia, kimofolojia na kisemantiki ili yaendane na mfumo wa lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umechunguza michakato ya kisemantiki inayojitokeza kwenye maneno ya mkopo katika Kiswahili ili kubainisha njia za kutambua maneno ya mkopo katika Kiswahili, kanuni za kuwakilisha michakato hiyo, sababu za kutokea kwa michakato hiyo na kuonesha tofauti za utokeaji wa michakato ya kisemantiki kati ya maneno yenye asili ya Kiingereza na yale yenye asili ya Kiarabu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili ambazo ni Nadharia ya Alama na Nadharia ya Sarufi Amilifu. Kwa kiasi kikubwa data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya maktabani ambapo data zilizopatikana kwa mbinu hiyo ndio zilipelekwa uwandani kuhakikiwa kwa kutumia mbinu za hojaji na usaili. Uchambuzi wa data ulitumia mbinu ya uchambuzi mada ambapo maelezo ndio yametumika kwa kiasi kikubwa japo kulikuwa na matumizi ya kanuni, majedwali na vielelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa maneno ya mkopo yaliyomo katika Kiswahili yanaweza kubainishwa kwa kutumia njia za kileksikografia, kifonolojia na kimatamshi. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa tunaweza kuibainisha michakato mikuu minne ya kisemantiki kwa kutumia kanuni mbalimbali. Mathalani, kuna kanuni ya kubainishia Mchakato Panuzi wa Kisemantiki (MPK), Mchakato Finyazi wa Kisemantiki (MFK), Mchakato Geuzi wa Kisemantiki (MGK) na Mchakato Kapa wa Kisemantiki (MKK). MFK umeonekana kuchakata idadi kubwa ya maneno ya mkopo kuliko mingine. MFK umechakata 84% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 64% ya maneno yenye asili ya Kiarabu. Mchakato unaofuatia ni MPK umechakata 8% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 20% yenye asili ya Kiarabu. MGK umechakata 0% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 14% yenye asili ya Kiarabu ilhali MKK umechakata 8% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 2% yenye asili ya Kiarabu. Pia, matokeo yameonesha kuwa kuna sababu mahususi za kutokea kwa michakato ya kisemantiki kwenye maneno ya mkopo na utokeaji wa michakato hiyo katika maneno ya mkopo unatofautiana kati ya lugha kopwaji moja na nyingine. Aidha, utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti fuatishi ziangalie michakato ya kisemantiki katika maneno yenye asili ya Kibantu katika Kiswahili, kwani utafiti huu umechunguza yale tu yenye asili ya Kingereza na Kiarabu.
  • Item
    Ukanushi katika vitenzi vva lugha ya kibena: Msingi wa kimofosintaksia
    (University of Dar es Salaam,, 2012) Mbunda, Irene Edward
    Utafiti huu unaliusu utokeuji wa mofimu za ukunnslii kalika vitenzi vya lugha ya Kibena. Data iliyojadiliwa katika utafiti huu imekusanywa kutoka kalika vjjjjj vitatu ambavyo ni Mlwango, llunda na Kichiwa, Vijiji hivi vipo kalika wilaya ya Njombe, mkoani Njoinbe. Data msingi na data fuatizi /imetumika katika utafiti huu. Data msingi ilikusanywa uwandani, wakati data fuati/i ilikusanywa kutoka maktabani. Utafiti huu umegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeonesha suala lililochunguzwa katika utafiti huu pamoja na mipaka yake. Sura ya pili imeonesha msingi wa nadharia ya Umbo Upeo iliyoasisiwa na Prince na Smolensky (1993), Nadharia hii imetumika kama mwongozo wa uchambuzi wa data iliyokusanywa. Vilevile machapisho mbalimbali yanayoelezea juu ya mofimu za ukanushi katika vitenzi vya lugha mbalimbali za Kibantu yameoneshwa katika sura ya pili. Sura ya tatu inaonesha mbinu zilizotumiwa na mtafiti katika kukusanya data ya utafiti ambayo imechambuliwa na kufafanuliwa katika utafiti huu. Mbinu ya ushuhudiaji, hojaji na usaili zimeelezewa kuwa zimetumika katika kukusanya data uwandani. Mbinu ya kusoma na kunukuu imetumika kukusanya data maktabani. Sura ya nne imeonesha uchambuzi wa data ulivyofanyika katika utafiti huu kwa kuzingatia masharti zuizi yanayozuia mofimu za ukanushi kujitokeza katika ruwaza zisizo kubalifu katika lugha ya Kibena. Uzingatiaji wa masharti zuizi hayo unatokana na mwongozo wa nadharia ya Umbo Upeo iliyo na madai ya msingi kuwa maumbo mbalimbali ya lugha hutokana na masharti zuizi yaliyopo. Hivyo mofimu za ukanushi zimebainishwa kujitokeza kulingana na masharti zuizi ya utokeaji wa mofimu hizo katika lugha ya Kibena. Sura ya tano imeonesha matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo ya tafiti fuatishi. Data ya utafiti imebaini kuwepo kwa mofimu nne za ukanushi katika lugha ya Kibena. Mofimu hizo zimeoneshwa kuwa hujitokeza mwanzoni mwa vitenzi vinavyokanushwa. Vilevile data ya utafiti imebaini kuwa lugha ya Kibena haina tabia ya kupachika mofimu za ukanushi zaidi ya moja katika kitenzi kimoja.