Ruwaza za toni katika vitenzi na nomino za kirombo

Loading...
Thumbnail Image
Date
2020
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahususu Ruwaza za Toni katika Vitenzi na Nomino za Kirombo. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ruwaza za ujitokezaji wa toni katika vitenzi na nomino za Kirombo na kanuni zinazotawala utokeaji huo. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru kwa kutumia Mkabala wa Tonijuu Msingi kama ulivyoasisiwa na Goldsmith (1976) na kuboreshwa na wanazuoni mbalimbali katika taaluma ya tonolojia. Utafiti ulifanyikia katika Vijiji vya Mengwe Juu na Mengwe Chini, Kata ya Mengwe, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Wango la utafiti ni nomino na vitenzi na wazungumzaji wazawa wa Kirombo. Aidha, mbinu ya usampulishaji iliyotumika ni Nasibu Tabakishi. Pia, Mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni: mahojiano na ushuhudiaji. Katika mahojiano nomino na vitenzi viliandaliwa kwa Kiswahili na watoataarifa walihitajika kuyatamka kwa Kirombo huku mtafiti akirekodi na kualamisha toni katika maneno hayo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna ruwaza mbalimbali za kitoni zinazoleteleza utokeaji wa kanuni za kitoni ambazo hutofautiana kutegemeana na idadi ya silabi na uwepo au kutowepo kwa yambwa. Kwa vitenzi na nomino za silabi moja hutawaliwa na kanuni ya uhusishaji wa tonichini na vitamkwa na sharti la ukubalifu, wakati vitenzi na nomino za silabi tatu hadi ama tano au sita za shina hutawaliwa na kanuni ya msambao wa tonijuu kuelekea kulia mwa shina, uhamaji wa TJM kutoka silabi ya kwanza kwenda katika silabi ya pili ya shina, unakiliji wa TJM katika silabi ya mwisho kasoro moja. TJM katika vitenzi na nomino za silabi moja ya shina hubiruka nyuma na khupachikwa katika kiambishi awali kwa nomino na vitenzi visoukomo sahili, wakati TJM hupachikwa katika mofimu ya yambwa kwa vitenzi visoukomo changamani vya silabi moja ya shina. Pia, kwa upande wa vitenzi visoukomo sahili matokeo yanaonesha kwamba kuna TJM mbili, yaani, ya kwanza ni ya yambwa na ya pili ikiwa ya shina, ambapo katika mchakato wa ukokotozi wa uibuzi wa toni, TJM ya shina hudondoshwa kwa kuwa yambwa ina nguvu zaidi. Aidha, inapendekezwa tafiti fuatizi zifanyike katika viwango vya kirai na sentensi, uradidi katika nomino na vitenzi na tonolojia linganishi katika jamiilugha za Kichaga. Utafiti huu umesaidia kujua namna toni zinavyojitokeza katika Kirombo kwa ujumla.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8701.T34M736)
Keywords
Language and languages, Bantu language, Kirombo, Swahilil language, Tanzania
Citation
Mramba, Peter Thobias (2020) Ruwaza za toni katika vitenzi na nomino za kirombo, Master dissertation, University of Dar es Salaam
Collections