Ujitokezaji wa tashtiti katika fasihi ya Kiswahili: Uchunguzi wa kazi teule

Loading...
Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili ukiongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha mbinu zinazotumika kuunda tashtiti, kueleza dhima ya tashtiti na kuainisha tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Uchunguzi wa ujitokezaji huu ulifanywa kupitia kazi teule za fasihi ya Kiswahili za: Kaptula la Marx 9Kezilahabi, 1999), Amezidi (Mohamed, 1995), Walenisi (Mkangi, 1995), na Miradi Bubu ya Wazalendo (Ruhumbika, 1992). Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchambuzi matini na mkabala wa kitaamuli. Aidha nadharia za semiotiki-jamii na Mwingiliano- matini ziliongoza utafiti huu. Matokeo katika utafiti huu yanaonesha tashtiti katika kzi teule ni mtindo wa kisanaa unaoundwa kwa kutumia mbinu za dhihaka, kejeli, ufyosi, matumizi ya tamadhali ya usemi hasa sitiari, tashbiha na uchuku ubeuzi, taswira na ishara, mandhari pamoja na ujenzi wa wahusika. Matokeo haya yanapingana na madai yaliyokwishatolewa na Msokile (1992), Mbonde (2002), Senkoro(2011), na Wamitila (2003) kwamba tashtiti katika fasihi ya Kiswahili hujitokeza kama kipengele cha kitamathali pekee, madai ambayo yalichukulia tashtiti kuwa kipengele kinachofungamanishwa na matumizi ya lugha pekee. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa tashtiti ni dhana pana, ambayo katika kujipambanua kwake inatumia si tu vipengele vya lugha na kitamathali, bali pia mbinu mbalimbali za kifani na kimaudhui. Vilevile, matokeo yanaonesha kuwa tashtiti ina dhima kuu tatu katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili. Dhima hizi ni za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Katika dhima ya kisiasa tashtiti inahakiki uongozi, inakemea rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, inapinga ukoloni mamboleo na utegemezi wa misaada, na inatathimini utoaji wa haki na usawa. Katika dhima ya kiuchumi tashtiti inaumbua hali ya umaskini, na inashambulia hali ya utabaka. Kijamii tashtiti ina dhima ya kukosoa mfumo wa elimu, kuhakiki utamaduni na maadili na pia kuumbua hali duni za afya na uzazi . Aidha utafiti huu umependekeza aina tano za tashtiti ambazo ni tashtiti ya mtindo jumuishi, tashtiti –tamathali, tashtiti-husika, tashtiti-ufyosi na tashtiti-fiche. Kutokana na matokeo ya utafiti huu uainishaji huu ndiyo unafaa kumika katiak kazi za fasihi ya Kiswahil
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr.Wilbert Chagula Library, (THS EAF PL8704.Z8.T34D364)
Keywords
Swahili literature, Rhetoric questions, Expression style, Kaptula la marx, Amezidi, Walensi, Miradi bubu ya wazalendo, Tanzania
Citation
Daniel, Z. L. (2019). Ujitokezaji wa tashtiti katika fasihi ya Kiswahili: Uchunguzi wa kazi teule, Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.
Collections