PhD Theses
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing PhD Theses by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 31
Results Per Page
Sort Options
Item A study of tense and aspect in Shambala(University of Dar es Salaam, 1985) Besha, Ruth MfumbwaTENSE and ASPECT as grammatical categories have long been the subject of theoretical and emprical studies by linguists, anthropologists and philosophers. The present study which investigates the manifestation of Tense and Aspect in Shambala is a further contribution to those efforts. It attempts to disentangle some of the key issues involved in the area in the light of what obtains in Shambala. The study is modelled on Reichenbach’s (1947) Scheme of Temporal relationships which rests on the idea that temporal relationships encoded in natural languages can be accounted for by the relations which hold between Speech Time: Event Time: Reference Point. Reichenbach’s scheme is modified to take account of the basic theoretical principle underlying this study that “every identifiable grammatical form is assumed to have one basic meaning”. This was necessitated by the need to distinguish clearly which among the many markers of the verb-group in Shambala are tense markers, which are aspect markers, and which are manifestations of other grammatical categories. In order to identify the tense markers the “adverbial test” is developed as a basic methodological tool. Thus the various tense forms are arrived at by considering the co-occurrence relationships between the verb forms and the temporal adverbials. The study is organized into seven main chapters and a short eighth chapter of concluding remarks. In the Introductory Chapter, the aim and objectives of the study are stated and the methods used to collect and analyze the data are discussed. The second chapter contains a broad sketch of the major phonological, morphological and syntactic features of Shambala. The verb-group is given lengthy treatment here, partly because it is complex and partly because it is the carrier of various grammatical markers including those of tense and aspect. Chapter three examines two categories of literature on Tense and Aspect. Section one examines literature that deals with Tense and Aspect from an essentially “sentential” point of view. Section two is concerned with literature that incorporates the role of “context” in the study of Tense and Aspect. Chapter four examines critically the key concepts used in this study and proposes definitions which it is hoped, clarify what has been unclear in many studies of Tense and Aspect. In Chapter Five the Tense Forms are discussed. The adverbial test is used to identify the various tense forms. The distributional constraints of the various forms are discussed and the characterisation of each form proposed. The Chapter further discusses how the tense forms interact with the temporal adverbials to specify the actual TIME of events. Aspect forms are discussed in Chapter Six where they are identified and characterised. The role of the adverbials and auxiliary verbs in expressing various aspectual distinctions is highlighted. Chapter Seven illustrates how the tense and aspect forms interact in actual discourse. It demonstrates the complimentarity between the sentential and the contextual factors in the use of tense and aspect forms. The concluding chapter contains several observations. The study shows that it is possible to reduce substantially the chances of overlap between tense and aspect forms at the grammatical level by adopting the principle of one form one meaning. Secondly the study has tried to show that while tense is a temporal grammatical category, the actual time of events is only established by the co-occurrence relationships holding between the tense forms and the temporal adverbials. Thirdly the study has tried to show that Shambala has limited grammaticalised aspectual distinctions; that many of the aspectual oppositions are manifested through the co-occurrence relationships between the tense forms and various lexical units in the language. Fourthly the study has tried to demonstrate that the use of present tenses in recounting past events can be successfully accounted for by employing the concept of different anchorage points for events in a communicative act.Item A study of the morphophonology of standard Kiswahili, Kipemba, Kitumbatu and Kimakunduchi(University of Dar es Salaam, 1991) Maganga, ClementThis study investigates whether identical morphemes undergo similar or different phonological processes at identical morpheme boundaries in four Kiswahili dialects, namely, Standard Kiswahili, Kipemba, Kitumbatu and Kimakunduchi. The theoretical model which is used in this study is generative phonology and the basic postulate of generative dialectology. The study is organized into six chapters. The first chapter, which is introductory, provides the background to the study. It states the problem, defines its scope, and articulates the objectives of the study. It also presents the hypotheses to be tested and the theoretical framework within which the discussion will be conducted. The methodology used in data collection and analysis is also discussed in this chapter. The four subsequent chapters discuss the major phonological processes which occur in the four Kiswahili dialects. Each dialect is examined separately under the following main sub-headings: underlying segments, pronominal prefixes, pronominal orphophonologica processes, noun classes, verb extensions and nominal deriva-tions. The sixth chapter attempts to synthesize the similarities and differences that have been observed in these dialects. The study shows that all the four dialects use the same inventory of sound segments and the same underlying forms for the prefixes whose underlying shapes are: /(C)u/, /(C)a/, /(C)i/ and /N/. The post-radical affixes are also basically the same in the four dialects. However, different tense aspect markers can be observed in the past and perfective affirmative verb forms, and the present, past and consequential negative verb forms. Seventeen phonological process which are governed by twenty different rules have been identified in this study. The major processes are glide formation (Rules 1, 2, 7 and 8); vowel deletion (Rules 4a, 4b, 5a and 5b); vowel harmony in the verb extensions (Rule 14); Palatalization.(Ru 11), place assimilation and nasal syllabification (Rules 12a and 12b), and neutralization(Rule 13) of the classes 9 and 10 nominal prefix /N/; and spirantization (Rule 15) and sibilantization (Rule 16) in nominal derivations. By making explicit the rules governing the occurrences of these processes in the different dialects, the study was able to provide a more accurate and systematic characterization of each of the four dialects. This can best be illustrated by referring to the two most common phonological processes, that is glide formation and vowel deletion. In Kipemba, glide formation is restricted to specific nominal stems which begin with nonback vowels while in the other three dialects, it always occurs whenever the /(C)u/ and /(C)i/ prefixes are immediately followed by non-high vowels or a high vowel with the opposite value for the feature [back]. In both Standard Kiswahili and Kipemba: (a) vowel deletion is restricted to specific nominal stems, while in Kitumbatu and Kimakunduchi it occurs before both nominal and verb stems, (b) only one type of vowel coalescence occurs whereby /a + i/- [S] (Rule 6), while in Kitumbatu and Kimakunduchi there are two types, namely, /a + i /- [å]and /a + u/-[É] (Rule 19 ). In standard Kiswahili, Kitumbatu and Kimakunduchi, the prefix /mu/ undergoes vowel deletion -cumnasal syllabification before consonant initial morphemes, while in Kipemba, this prefix as well as the prefix /ni/ and the tense/aspect marker + na + undergo vowel deletion, nasal syllabification and place assimilation in a similar environment (Rules 17a and 17b). Assibilation - cum - vowel deletion in the prefix /ki/ (Rules 10 and 9) only occur in standard Kiswahili, Kitumbatu and Kimakunduchi but not in Kipemba, where glide formation occurs instead. Finally, the study has shown that standard Kiswahili and Kipemba are closer to each other than they are to Kitumbatu and Kimakunduchi which are also very much alike.Item A study of syntax of Kiswahili verbs(University of Dar es Salaam, 1994) Kihore, Y. MThis study is an investigation of various syntactic aspects of the verbal category formation phenomenon in Kiswahili, a Bantu language. This phenomenon involves a constellation of various morphological elements appearing as prefix(es), root and suffix(es) which create verbal structural formations that form core of various sentence constructions. Each of the elements in the sets of morphological categories in question possesses some syntactic cases which become more apparent only in the context of a combination pattern of various such elements. This situation was, previously, taken to manifest an "inextricable link" between two linguistic domains - morphology and syntax. However, the various analyses undertaken in this study reveal that it is the morphological elements themselves that become inextricably linked to yield categories that are accessible to syntactic rules. The Kiswahili syntactic structures resulting from various combinations of such elements are introduced in Chapter one. In this chapter also Generalized Phrase Structure Grammar (GPSG) - the theoretical framework to be applied in this study - is introduced showing its basic concepts and analytical devices. The section on GPSG also incorporates literature review of contributions by the proponents of this framework. This is followed by the consideration of various aspects of the morphological elements involved in verbal structural formations and samples of their combination patterns in Chapter two. In chapters three, four and five, the three construction types earmarked for treatment are fully investigated and the rules formulated far discrete representations of their various structural types. The construction types in question are categorized as Basic, Compound and Complex verbal constructions. Chapter six is a conclusion drawing on the findings of the study and their implications for Kiswahili syntactic studies, syntactic theory in general and the framework used.Item Mabadiliko katika majigambo: uchunguzi wa majigambo ya jadi na ya bongo fleva(University of Dar es Salaam, 2012) Samwel, MethodUtafiti huu umeshughulikia Mabadiliko katika Majigambo: Uchunguzi wa Majigambo ya Jadi na ya Bongo Fleva. Tulifanya utafiti ili kuhakiki madai kwamba tanzu mpya za fasihi zinazoibuka hujengwa katika misingi ya tanzu za awali. Majigambo ya jadi ni utanzu wa fasihi simulizi uliokuwapo tangu awali, majigambo yanayojitokeza katika muziki wa Bongo Fleva ni utanzu mpya; utafiti huu, kwa hiyo, umechunguza jinsi tanzu hizo mbili zinavyohusiana ili kuona kama majigambo ya Bongo Fleva yamechimbuka kutoka katika majigambo ya jadi. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha nduni za ushairi wa majigambo ya jadi na ya Bongo Fleva; kuzilinganisha na kuzilinganua nduni hizo; kueleza sababu za mabadiliko ya majigambo, na kueleza mchango wa mabadiliko hayo katika maendeleo ya fasihi simulizi. Ili kufikia malengo hayo, utafiti huu umetumia mbinu tano ambazo ni ukusanyaji wa matini, usikilizaji wa kanda na sidii, ushuhudiaji, usaili/mahojiano na utumiaji wa dodoso. Nazo nadharia zilizotumika ni nadharia ya Umbuji, na hasa Umbuji wa Daniel Kunene, Semiotiki na nadharia ya Ubadilikaji Mpya. Kuhusu matokeo, imebainika kwamba ushairi wa majigambo ya jadi na ule wa Bongo Fleva unafanana sana kimaudhui na kifani hivyo kuthibitisha kwamba majigambo ya Bongo Fleva yanachimbuka katika majigambo ya jadi. Ingawa kuna kufanana kwingi, aina hizo mbili za majigambo zina tofauti za namna fulani. Tofauti hizo ndogondogo zinazoonekana baina ya aina hizo mbili za majigambo, zinathibitisha kwamba ushairi wa majigambo unabadilika sambamba na mabadiliko yanayotokea katika jamii.Item Ukanushi katika vitenzi vva lugha ya kibena: Msingi wa kimofosintaksia(University of Dar es Salaam,, 2012) Mbunda, Irene EdwardUtafiti huu unaliusu utokeuji wa mofimu za ukunnslii kalika vitenzi vya lugha ya Kibena. Data iliyojadiliwa katika utafiti huu imekusanywa kutoka kalika vjjjjj vitatu ambavyo ni Mlwango, llunda na Kichiwa, Vijiji hivi vipo kalika wilaya ya Njombe, mkoani Njoinbe. Data msingi na data fuatizi /imetumika katika utafiti huu. Data msingi ilikusanywa uwandani, wakati data fuati/i ilikusanywa kutoka maktabani. Utafiti huu umegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeonesha suala lililochunguzwa katika utafiti huu pamoja na mipaka yake. Sura ya pili imeonesha msingi wa nadharia ya Umbo Upeo iliyoasisiwa na Prince na Smolensky (1993), Nadharia hii imetumika kama mwongozo wa uchambuzi wa data iliyokusanywa. Vilevile machapisho mbalimbali yanayoelezea juu ya mofimu za ukanushi katika vitenzi vya lugha mbalimbali za Kibantu yameoneshwa katika sura ya pili. Sura ya tatu inaonesha mbinu zilizotumiwa na mtafiti katika kukusanya data ya utafiti ambayo imechambuliwa na kufafanuliwa katika utafiti huu. Mbinu ya ushuhudiaji, hojaji na usaili zimeelezewa kuwa zimetumika katika kukusanya data uwandani. Mbinu ya kusoma na kunukuu imetumika kukusanya data maktabani. Sura ya nne imeonesha uchambuzi wa data ulivyofanyika katika utafiti huu kwa kuzingatia masharti zuizi yanayozuia mofimu za ukanushi kujitokeza katika ruwaza zisizo kubalifu katika lugha ya Kibena. Uzingatiaji wa masharti zuizi hayo unatokana na mwongozo wa nadharia ya Umbo Upeo iliyo na madai ya msingi kuwa maumbo mbalimbali ya lugha hutokana na masharti zuizi yaliyopo. Hivyo mofimu za ukanushi zimebainishwa kujitokeza kulingana na masharti zuizi ya utokeaji wa mofimu hizo katika lugha ya Kibena. Sura ya tano imeonesha matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo ya tafiti fuatishi. Data ya utafiti imebaini kuwepo kwa mofimu nne za ukanushi katika lugha ya Kibena. Mofimu hizo zimeoneshwa kuwa hujitokeza mwanzoni mwa vitenzi vinavyokanushwa. Vilevile data ya utafiti imebaini kuwa lugha ya Kibena haina tabia ya kupachika mofimu za ukanushi zaidi ya moja katika kitenzi kimoja.Item Mchango wa lahaja katika kukuza na kuendeleza kiswahili sanifu hazina fiche iliyomo katika lahaja za kiswahili za Zanzibar(University of Dar es Salaam, 2014) Hans, Mussa MohamedUtafiti huu ulikusudia kuchunguza msamiati unaohusu majina ya samaki wa baharini katika jamii ya wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili zilizoko Zanzibar. Lengo likiwa ni kubaini namna lahaja hizi zinavyoweza kuchangia katika kukuza na kuendeleza Kiswahili Sanifu. Hata hivyo, ilionekana kwamba litakuwa jambo la welekevu iwapo pia historia ya wazungumzaji wa lahaja hizo na mchango wao katika historia ya lugha ya Kiswahili vitachunguzwa kwa kina. Data za utafiti zilipatikana uwandani kwa kuhusisha mbinu mbalimbali ambazo ni ushuhudiaji, usaili, hojaji na majadiliano katika majopo. Baaadhi ya data pia zilipatikana maktabani. Kwa upande wa uchambuzi wa data, palitumika mbinu ya kikompyuta kuchambulia data za kimsamiati na data za kihistoria zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Mwachano - Makutano ya Lugha za Kibantu pamoja na nadhariatete ya Ndugu na Ndugu wa Mbali iliyoasisiwa na Massamba (2007). Nadharia hii pamoja na nadhariatete inayoishajihisha kwa kiasi kikubwa inawiana na matokeo ya utafiti. Hata hivyo, katika utafiti huu imependekezwa kwamba nadhariatete ya Ndugu na Ndugu wa Mbali ifanyiwe marekebisho kidogo kwa kuongezewa dhana ya Ndugu wa Karibu ili kuakisi vema uhusiano ulioko miongoni mwa lahaja za Kiswahili na pengine lugha mbalimbali za Kibantu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili kupitia katika lahaja zao wana mchango mkubwa sana katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili hususani katika uwanja wa msamiati unaohusu majina ya samaki wa baharini pamoja na uwanja wa historia ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla. Utafiti kuhusu msamiati wa majina ya samaki wa baharini mbali na kutoa taarifa zinazohusu majina ya aina anuwai za samaki na sifa zao, umebainisha pia msamiati mpya ambao haumo katika Kiswahili Sanifu. Katika mjadala huu pia utafiti umeweka bayana tofauti ya kimsamiati baina ya Zanzibar na Tanzania bara, tofauti ambazo pia zinajitokeza katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyoandikwa na TUKI na Kamusi la Kiswahili Fasaha iliyoandikwa na BAKIZA. Hata hivyo imependekezwa kwamba utafiti mwingine katika jamii za wazungumzaji wa lahaja za Kiswahili unaweza kuelekezwa katika msamiati unaohusu nyanja nyingine kama vile utamaduni na tiba. Katika utafiti wa kihistoria, mbali na mambo mengine utafiti umebainisha kwamba chimbuko la wazungumzaji wa lahaja za Kimakunduchi, Kitumbatu na Kipemba ni maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Kenya hususani maeneo yanayopatikana katika upwa wa Afrika Mashariki. Maeneo hayo ni pamoja na Bagamoyo, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na Mombasa. Hata hivyo, kuna baadhi ya watoa taarifa waliodai kwamba chimbuko lao ni Shiraz (Pashia) ingawa hawakuwa na ushahidi usiosailika.Item Matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es salaam(University of Dar es Salaam, 2014) Peterson, RhodaShauku ya kuchunguza eneo la mandhari-lugha inaendelea kukua miongoni mwa watafiti wa lugha kutokana na kushamiri kwa maandishi katika sehemu za wazi. Ulinganishaji wa maandishi binafsi na ya kiserikali umekuwa kama msingi wa tafiti za kimandhari-lugha. Kigezo hiki pekee hakiakisi matumizi halisi ya lugha katika eneo hilo kwani linahusisha shughuli tofauti za kijamii. Utafiti huu wa matumizi na dhima za lugha katika mandhari-lugha ya jiji la Dar es Salaam umefanywa kwa kuzingatia muktadha wa kibiashara. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki-jamii ya Halliday inayochunguza lugha kwa kuihusisha na jamii. Data zilizoko kwenye mfumo wa kongoo-andishi zilikusanywa kwa njia ya kupiga picha. Ushuhudiaji wa huduma zitolewazo madukani na mahojiano kwa wafanyabiashara zilikuwa njia za nyongeza za ukusanyaji wa data. Ufafanuzi wa data ulifanywa kwa kutumia njia ya uchambuzi mada. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa Dar es Salaam ni jiji lenye matumizi ya wingilugha. Lugha zilizobainika kutumiwa ni Kiingereza, Kiswahili, lugha za asili, Kiarabu, Kichina, Kihindi, na Kikorea. Lugha ya Kiingereza inatawala kimatumizi ikifuatiwa na Kiswahili, kisha lugha zingine zimetumiwa kwa kiasi kidogo sana. Dhima za lugha zilizodhihirika ni kukaribisha na kushawishi wateja wanunue bidhaa, kutambulisha bidhaa, jamii mbalimbali na imani za kidini. Kutokana na data za utafiti huu inapendekezwa kwamba muktadha wa matumizi ni kipengele kingine kinachoweza kutumiwa kuchunguza matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, maudhui ni kipengele kinachoweza kutumiwa kuchunguza dhima za lugha katika mandhari-lugha.Item Athari za kiutamaduni katika tafsiri mifano kutoka matini za Kitalii katika makumbusho za Tanzania(University of Dar es Salaam, 2014) Jilala, HadijaUtafiti huu umeshughulikia athari za kiutamaduni zijibainishazo katika tafsiri kwa kuchambua matini za kitalii zilizopo katika Makumbusho za Tanzania. Nia ya kufanya hivyo ni kuibua modeli ya kutafsiri matini za kiutamaduni ambayo itakuwa kiunzi cha kutafsiri matini za kiutamaduni ili kudhibiti mapungufu ya kimawasiliano. Dira iliyoongoza katika utengenezaji wa modeli ni matokeo ya utafiti huu na mhimili wa mawazo ya Nadharia ya Skopos. Ili kuibua Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni, tulitathmini mbinu za kutafsiri matini za kiutamaduni, mikakati iliyotumika katika uteuzi wa visawe vya kiutamaduni, mapungufu ya kimawasiliano yanayosababishwa na athari za kiutamaduni na namna tunavyoweza kukabiliana nayo. Data za utafiti huu zilipatikana kwa kutumia mbinu za usomaji wa machapisho, dodoso, usaili, uchunguzi shirikishi na upimaji. Utafiti huu umegundua kuwa, mbinu zinazotumika kutafsiri matini za kiutamaduni hazina uangavu na hivyo kusababisha mapungufu mengi ya kimawasiliano. Kichochezi kikuu cha mapungufu ya kimawasiliano ni mwachano wa kiutamaduni baina ya utamaduni chanzi na utamaduni lengwa. Ili kupunguza dosari hizo, utafiti huu umependekeza Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni (MMK) ambayo ni kiunzi cha kutafsiri matini za kiutamaduni ili kuleta ufanisi wa mawasiliano. Mhimili mkuu wa modeli hii ni fikra kwamba, ujumbe wa matini ya kiutamaduni ndiyo huukilia mbinu za tafsiri. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa mbinu inayofaa kutafsiri matini za kiutamaduni ni “uasilishaji na ufafanuzi wa visawe”. Mbinu hii ndiyo nguzo kuu ya Modeli ya Mawasiliano ya Kiutamaduni.Item Mofolojia ya majina ya mahali ya kiswahili na kihaya katika jamii ya wahaya: uzingativu wa masuala ya kiisimujamii(University of Dar es Salaam, 2016) Buberwa, AdventinaBaadhi ya wanaisimu huyatazama majina ya mahali kama maneno yasiyoweza kuchanganuliwa kimofolojia ilhali wengine wakiyatazama kama maneno yaliyojengwa kwa vipashio maalum. Madai haya kinzani ndiyo yaliyoongoza raghba ya mtafiti kufanya utafiti huu unaochunguza mofolojia ya majina ya mahali ya Kiswahili na Kihaya kwa kuzingatia masuala ya kiisimujamii yanayofafanua maumbo hayo. Kwa kutumia mbinu za utafiti zilizoteuliwa, yaani usaili, mijadala katika makundi lengwa na ushuhudiaji, data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka katika wilaya za Muleba, Misenyi, Bukoba vijijini na Bukoba Mjini, mkoani Kagera. Vifaa vya kukusanyia data vilivyotumika ni pamoja na kalamu na daftari, kinasasauti, kompyuta pakatwa na kamera. Uchanganuzi wa data kimofolojia umeongozwa na nadharia ya Mofolojia Leksika. Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa kutumia majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika. Uchanganuzi wa vipengele vya kiisimujamii umefanywa kwa kuongozwa na mkabala wa Uchanganuzi Tunduizi Kilongo. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa majina ya mahali yaliyochunguzwa yameundwa ama kwa neno moja pekee au kwa maneno ambatani, yaani neno zaidi ya moja. Utafiti huu umethibitisha kuwa vipo vipashio maalum vinavyounda majina ya mahali na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia. Licha ya majina ya mahali kutokana na masuala mbalimbali ya kiisimujamii, majina hayo hayateuliwi kama yalivyo kama wanaisimu waliotangulia walivyodhani. Mbinu za uundaji wa maneno huhusika katika uundaji wa majina ya mahali. Utafiti huu unapendekeza kuwa utafiti kama huu unaweza kufanywa katika maeneo mengine. Aidha, inapendekezwa kuwa majina ya mahali yanaweza kuchunguzwa kimofolojia, kisemantiki, kiisimujamii au kisintaksia.Item Ukakamaaji kwa wajifunzaji wa lugha ya kiswahili katika jamii ya wakinga(University of Dar es Salaam, 2016) Gawasike, ArnoldUchunguzi kuhusu ukakamaaji kwa wajifunzaji wa lugha ya pili (kuanzia sasa L2) kumeongezeka katika miaka ya karibuni. Hata hivyo, chanzo cha ukakamaaji huo bado hakijabainishwa japo kuwa uhawilishaji wa lugha ya kwanza (kuanzia sasa L1) katika kujipatia L2 kuna tajwa sana. Utafiti, huu umeshughulikia suala la ukakamaaji kwa wajifunzaji wa L2 katika jamii ya Wakinga kata za Mbalatse, Ipepo na Lupila. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Usasanyuzi Linganishi (kuanzia sasa NULI) ya Lado (1967). Nadharia hii, inachunguza kufanana, na kutofautiana kwa L1 na L2 ili kuboresha ufundishaji wa L2 na Nadhariatete Teuzi ya Ukakamaaji (kuanzia sasa NATEU) ya Han (2009). Nadhariatete hii inaona kuwa katika kujipatia L2 kuna vipengele fulani vya L2 vina satua ya kukakamaa kuliko vingine kutokana na tofauti kati ya L1 na L2. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa njia nne ambazo ni: kuandika insha, kujaza hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Data za insha na hojaji zilikuwa katika mfumo wa kongoo-andishi, wakati data za mahojiano na ushuhudiaji zilikuwa katika mfumo wa kongoo-uneni. Data zilichambuliwa kwa kutumia programu ya Statistical Package for Social Sciences (SPSS) na kutolewa maelezo, vielelezo, majedwali na grafu. Pia, zilichambuliwa kwa njia ya kusoma insha za wajifunzaji L2 na kubainisha vipengele mbalimbali vyenye dosari. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, wajifunzaji wa L2 katika jamii ya Wakinga wamekakamaa. Chanzo kikuu cha ukakamaaji huo ni kutokuwapo kwa mwingiliano kati ya jamii-lugha ya Wakinga na jamii-lugha nyingine. Hii ni tofauti na tafiti tangulizi zilizoonesha kuwa, chanzo kikuu cha ukakamaaji ni uhawilishaji wa L1 katika L2. Pia, tofauti za kifonolojia kati ya lugha ya Kiswahili na Kikinga husababisha ukakamaaji kwa matamshi. Vilevile, kuchelewa kuanza kujipatia lugha ya Kiswahili na muda mwingi kutumia lugha ya Kikinga husababisha hali ya ukakamaaji kwa wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii hii. Utafiti huu umebaini kuwa, msamiati wenye satua ya kukakamaa ni ule unaohusisha fonimu zifuatazo: /r/, /ð/, /ɵ/, /ɤ/, /č/, /ŋ/ na silabi mwambatano. Ili kuondokana na tatizo la ukakamaaji, utafiti umependekeza kuboresha miundombinu ili kuruhusu mwingiliano na jamii-lugha nyingine. Kadhalika, kuimarisha elimu ya awali, kuhamasisha matumizi mapana ya Kiswahili kumezingatiwa pamoja na kupanua mwingiliano baina ya Wakinga na jamii zingine. Mapendekezo ya tafiti fuatizi: mosi, utafiti mwingine ufanywe ili kuchunguza athari za lugha ya Kiswahili katika Kikinga. Pili, utafiti huu ulifanyika vijijini mwa wilaya ya Makete; utafiti mwingine kama huu unaweza kufanywa mjini Makete ili kubaini kinachojiri huko. Tatu, utafiti mwingine wenye welekeo wa kielimu unaweza kufanywa ili kuchunguza mbinu wanazotumia walimu kufundisha lugha ya Kiswahili, na pia mbinu watumiazo wanafunzi katika kujifunza lugha hii.Item Mandhari na usawiri wa ukimwi katika riwaya ya kiswahili 2000-2010(University of Dar es Salaam, 2016) Bulaya, JovietUtafiti huu umechunguza jinsi ugonjwa wa UKIMWI unavyosawiriwa katika fasihi kwa kuiangalia riwaya ya Kiswahili kupitia katika kipengele cha mandhari. Utafiti unalenga kujibu maswali yafuatayo: kwanza, ni jinsi gani mandhari ya riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI inafungamana na dhamira zinazosawiriwa na riwaya husika? Pili, riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI inatumiaje mandhari kuumba wahusika wake? Na mwisho, waandishi wa riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI wanatumiaje mandhari kujenga lugha inayoibua athari na changamoto za UKIMWI katika riwaya zao? Sambamba na maswali hayo, tumefafanua malengo ya utafiti huu kuwa ni: mosi, kujadili jinsi mandhari inavyofungamana na dhamira zinazoelezwa na riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI. Pili, kueleza jinsi riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI inavyotumia mandhari kuumba wahusika wake. Na tatu ni kubainisha namna waandishi wa riwaya ya Kiswahili ihusuyo UKIMWI wanavyotumia mandhari kuumba lugha inayoibua athari na changamoto za UKIMWI katika riwaya zao. Ili kufikia kusudi la utafiti huu , tumetumia mbinu mbalimbali za utafiti zikiwamo za utafiti wa nyaraka na mahojiano. Mbinu hizi kwa pamoja zimetumika kukusanya data zilizosaidia kujibu maswali ya utafiti huu. Nadharia ya Mwingiliano-matini ndiyo imeongoza utafiti huu. Nadharia hii inasisitiza kuwa hakuna matini asilia, bali uhai wa matini moja hutegemea matini nyingine. Kwa hiyo, matini za kifasihi hutegemeana katika kukamilisha maana. Kwa kutumia nadharia hii tumeona kuwa, mandhari zinaingiliana, kukamilishana na kutegemeana katika kuliumba tatizo la UKIMWI. Hii inatokana na ukweli kuwa, riwaya zinazochunguzwa zimetumia mandhari mbalimbali kuwaumba wahusika, kuibua dhamira na kuchomoza lugha inayoelezea athari na changamoto za UKIMWI. Kutokana na utafiti huu, upo uhusiano mkubwa kati ya mandhari na uibuaji wa dhamira za kazi ya fasihi. Pili, kuna uhusiano kati ya mandhari na ujenzi wa wahusika. Wasifu, tabia na mienendo ya wahusika wa riwaya teule kwa sehemu kubwa ni matokeo ya mandhari wanamokuwa. Vilevile, mandhari inahusiana na lugha kwani, lugha inayotumiwa na wahusika katika riwaya inategemea mandhari wanamokuwa. Hii inathibitisha kuwa, mandhari ina umuhimu mkubwa katika kuibua dhamira, kuwaumba wahusika pamoja na kutolea ujumbe uliokusudiwa katika kazi ya fasihi hasa riwaya. Kutokana na uchunguzi wa riwaya teule, kazi ya fasihi hasa riwaya haikamilishwi na mandhari moja, bali upo mwingiliano mkubwa wa mandhari mbalimbali ambao unaifanya riwaya ikamilishe maana na kusudi la mwandishi. Na kwa hiyo, mandhari ni mojawapo ya mihimili muhimu katika kuumba maana ya kazi ya fasihi.Item Dhima ya visasili katika riwaya ya Kiswahili: uchambuzi wa Nagona, Mzingile na Ziraili na Zirani(University of Dar es Salaam, 2016) Mbijima, RoseUtafiti huu unahusu “Dhima ya Visasili katika Riwaya ya Kiswahili: Uchambuzi wa Nagona (1990), Mzingile (1991) na Ziraili na Zirani (1999).” Tulifanya utafiti ili kuhakiki madai ya baadhi ya wataalamu wa fasihi wanaoona kuwa uandishi wa Kezilahabi unarudisha nyuma maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Tulichokifanya ni kujadili dhima ya visasili katika riwaya tatu tulizoziteua ili kuona kama madai hayo yana ukweli. Utafiti huu, kwa hiyo, umechunguza dhima ya visasili ambayo ni matini simulizi, ndani ya riwaya ambayo ni matini andishi. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha visasili katika riwaya teule; kujadili dhima ya kimaudhui ya visasili katika riwaya teule na kujadili dhima ya kifani ya visasili katika riwaya teule. Utafiti huu ni wa maktabani na uwandani. Ili kufikia malengo ya utafiti huu mbinu za aina mbili zilitumika kukusanya data. Mbinu ya mahojiano ilitumika kukusanya data za uwandani wakati, kwa upande wa utafiti wa maktabani, mbinu ya kusoma matini ilitumika. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo na Nadharia za Mwingilianomatini na Uhemenitiki ndizo zimetumika katika uchambuzi wa data. Utafiti umebaini kwamba riwaya teule zimesheheni visasili ambavyo vina dhima za kimaudhui na kifani. Dhima hizo ni kubwa na nyingi kiasi cha kuwa na athari chanya katika utanzu wa riwaya na hivyo kuchangia katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili na siyo kuyarudisha nyuma.Item Uchanganuzi Kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya bunge la Tanzania(University of Dar es Salaam, 2016) Sylivester, JohanesUtafiti huu unahusu uchanganuzi kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya BJMT katika kipindi cha mwaka 1980 hadi 2014.Data ilikusanywa kwa mbinu za uchambuzi wa nyaraka, ushuhudiaji, hojaji na usaili na kuchambuliwa na kufasiriwa kwa mkabala wa uchanganuzi kilongo shirikishi na mpishano huru. Walengwa wa utafiti walikuwa Wabunge wa BJ MT. Nadharia iliyotuongoza ni Nadharia ya Staha ya Brown na Levmson (1987) inayodai kuwa , kuna kauli zenye kutweza staha na iii kauli hizo zikweze staha mzungumzaji anatakiwa kuzisuka kwa kutumia mbinu faafu za kistaha. Pia, tulizingatia maboresho ya Fraser (1990) anayedai kuwa ili mzungumzaji akweze staha lazima azungumze kwa kuzingatia kanuni zinazodhibiti majadiliano. Kutokana na uchanganuzi kilongo uliozingatia vipengele vya kinadharia, kanuni za Bunge na muktadha wa mazungumzo data tuliyoipata imetupa vipengele vinavyohusiana na kauli zenye kutweza au kukweza. Miongoni mwa kauli hizo ni matusi, kumshambulia Mbunge kuwa ni mnafiki au sio makini, kusema uongo, kuhamasisha uvunjifu wa sheria, kuonesha kuwa wenzio ni punguani, vichaa au wendawazimu, kujivuna au kubeza wengine, kumpa taarifa Spika (Kiti) au kutotii maelekezo yake, kutotumia neno 'Mheshimiwa' kabla ya jina la Mbunge, kauli za kibaguzi na mwisho kuzungumzia mambo ya siri ya Mbunge. Kwa upande wa kauli zenye kukweza staha, utafiti unaweka wazi kuwa ili zijitokeze ni lazima mzungumzaji ateue mbinu faafu za kistaha zitakazomwezesha kulinda utu wa wasikilizaji pamoja na makatazo yanayodhibiti matumizi ya lugha Bungeni. Mbinu hizo ni pamoja na ubadili haji msimbo, matumizi ya kauli ya kutendwa na kutendana, kunukuu, matumizi ya nafsi ya kwanza wingi, matumizi ya vitambulisho hadhi, uteuzi mzuri wa msamiati, matumizi ya njeo ya wakati uliopita //-Ii-// mahali pa wakati uliopo //-na-// wakati wa kuuliza swali na uepukaji. Kwa ujumla, utafiti umeonesha kuwa, uwepo wa kauli zenye kutweza staha Bungeni unatokana na kutotumia mbinu faafu za ki taha. Matokeo ya utafiti huu yanachangia maarifa mapya katika taaluma ya isimu-tumizi Y . Kiswahili hasa katika taaluma za pragmatiki, isimujamii na elimu-mitindo. Pia, yanachangia katika kipengele cha uchanganuzi kilongo kwa kupendekeza mbinu za uchanganuzi kilongo shirikishi na uchanganuzi kilongo mpishano huru kama mbmu za kuchambua na kufasiri data. Kipekee kabisa, utafiti huu unachambua kwa undani kipengele cha staha ambacho ni cha pragmatiki katika mijadala ya Bunge ili kuweza kupata ruwaza za lugha ya kibunge zenye kukweza staha. Ili kubainisha ruwaza za lugha ya kibunge tunapendekeza utafiti zaidi utakaobainisha vipengele vya kiisimu vinavyounda lugha hiyo. Pia, kuhusu mbinu za kistaha katika lugha ya Kiswahili kwa ujumla , tupendekeza tafiti nyingine kufanyika kwenye taasisi nyingine pia na katika mazmgua yasiyo rasmi.Item Michakato ya kisemantiki kwenye maneno ya mkopo katika kiswahili: mifano kutoka Kiingereza na Kiarabu(University of Dar es Salaam, 2017) Shembilu, Musa MohamedKiswahili kama zilivyo lugha nyingine kimekopa maneno kutoka lugha mbalimbali. Miongoni mwa lugha hizo ni Kiingereza na Kiarabu. Maneno hayo yanapoingia katika Kiswahili huchakatwa katika viwango mbalimbali vya kiisimu kama vile kifonolojia, kimofolojia na kisemantiki ili yaendane na mfumo wa lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umechunguza michakato ya kisemantiki inayojitokeza kwenye maneno ya mkopo katika Kiswahili ili kubainisha njia za kutambua maneno ya mkopo katika Kiswahili, kanuni za kuwakilisha michakato hiyo, sababu za kutokea kwa michakato hiyo na kuonesha tofauti za utokeaji wa michakato ya kisemantiki kati ya maneno yenye asili ya Kiingereza na yale yenye asili ya Kiarabu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili ambazo ni Nadharia ya Alama na Nadharia ya Sarufi Amilifu. Kwa kiasi kikubwa data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya maktabani ambapo data zilizopatikana kwa mbinu hiyo ndio zilipelekwa uwandani kuhakikiwa kwa kutumia mbinu za hojaji na usaili. Uchambuzi wa data ulitumia mbinu ya uchambuzi mada ambapo maelezo ndio yametumika kwa kiasi kikubwa japo kulikuwa na matumizi ya kanuni, majedwali na vielelezo. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa maneno ya mkopo yaliyomo katika Kiswahili yanaweza kubainishwa kwa kutumia njia za kileksikografia, kifonolojia na kimatamshi. Vilevile, utafiti huu umebaini kuwa tunaweza kuibainisha michakato mikuu minne ya kisemantiki kwa kutumia kanuni mbalimbali. Mathalani, kuna kanuni ya kubainishia Mchakato Panuzi wa Kisemantiki (MPK), Mchakato Finyazi wa Kisemantiki (MFK), Mchakato Geuzi wa Kisemantiki (MGK) na Mchakato Kapa wa Kisemantiki (MKK). MFK umeonekana kuchakata idadi kubwa ya maneno ya mkopo kuliko mingine. MFK umechakata 84% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 64% ya maneno yenye asili ya Kiarabu. Mchakato unaofuatia ni MPK umechakata 8% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 20% yenye asili ya Kiarabu. MGK umechakata 0% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 14% yenye asili ya Kiarabu ilhali MKK umechakata 8% ya maneno yenye asili ya Kiingereza na 2% yenye asili ya Kiarabu. Pia, matokeo yameonesha kuwa kuna sababu mahususi za kutokea kwa michakato ya kisemantiki kwenye maneno ya mkopo na utokeaji wa michakato hiyo katika maneno ya mkopo unatofautiana kati ya lugha kopwaji moja na nyingine. Aidha, utafiti huu unapendekeza kuwa tafiti fuatishi ziangalie michakato ya kisemantiki katika maneno yenye asili ya Kibantu katika Kiswahili, kwani utafiti huu umechunguza yale tu yenye asili ya Kingereza na Kiarabu.Item Ushujaa katika motifu ya safari ya msako: ulinganishi wa ngano za kiewe kutoka ghana na riwaya za Shaaban robert kutoka Tanzania.(University of Dar es Salaam, 2018) Sosoo, Felix KwameUtafiti huu ulihusu ushujaa katika motifu ya safari ya msako ulinganishi ukiwa katika ngano za Kiewe kutoka Ghana na riwaya teule za Shaaban Robert kutoka Tanzania. Tulifanya utafiti kutokana na mgongano wa kinadharia ambapo kuna wataalamu wa fasihi wanaoona kuwa, kwa vile kila jamii ina utamaduni wake, kazi zao za fasihi hutofautiana na wengine wanaoona kuwa jamii zenye mfanano mkubwa wa kiutamaduni huweza kuwa na kazi za fasihi zinazofanana. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza na kulinganisha ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert. Aidha, utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi manne ambayo ni: Kubainisha ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako katika ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert; kueleza kufanana na kutofautiana kwa ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert; kufafanua jinsi ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako unavyobainisha utamaduni na falsafa ya Kiafrika katika ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert; na kubainisha dhima ya ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaza teule za Shaaban Robert katika maendeleo ya fasihi. Ili kuweza kutimiza malengo hayo, data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za aina mbili, ambazo ni majadiliano/mahojiano ya vikundi na udurusu matini. Mkabala wa uchambuzi uliotumika ni ule wa kitaamuli. Aidha, uchambuzi huo ulifanywa kwa kutumia ruwaza ya shujaa, nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika na nadharia ya Mwingilianomatini. Kuhusu matokeo ya utafiti, imebainika kuwa ngano za Kiewe na riwaya teule kwa kiasi kikubwa zimesheheni ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako. Aidha, imebainika kuwa, kuna mfanano mkubwa baina ya ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako katika ngano za Kiewe na riwaya teule. Pia, utafiti huu umebaini kuwa ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako katika tanzu husika unabainisha utamaduni na falsafa ya Kiafrika. Mwisho, utafiti huu umebainisha dhima ya ushujaa unaosawiriwa katika motifu ya safari ya msako kwenye ngano za Kiewe na riwaza teule za Shaaban Robert katika maendeleo ya fasihi teule. Mbali na kufafanua masuala hayo, bado utafiti wa kina unahitajika katika maeneo mbalimbali. Kwanza, kuna haja ya kufanya utafiti utakaohusisha ngano nyingi zaidi na riwaya nyingine zaidi ya zilizotumika katika utafiti huu. Pia, utafiti zaidi utakaohusisha tanzu nyingi zaidi unahitajika ili kutoa mahitimisho ya kimajumui.Item Uchanganuzi wa upinduzi wa kimahali katika lugha ya Kiswahili(University of Dar es Salaam, 2019) Hassan, FabiolaKwa kawaida kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na za kisarufi za viambajengo vya sentensi. Uhusiano huo ni kwamba kiambajengo chenvc dhima ya kisemantiki inayotokea katika nafasi ya juu ndicho kinapaswa kuwa kiimacha sentensi. Upinduzi wa kimahali ni mchakato unaoibua changamoto katika uhusiano huo. Changamoto iliyopo ni kwamba kimahali ambacho kinatokea katikanafasi ya chini katika udarajia wa dhima za kisemantiki, kinapandishwa hadhi na kuwa kiima hata kama katika tungo kuna kiambajengo kinachopaswa kuwa kiima ikilinganishwa na kimahali. Aidha, licha ya kufanyika tafiti katika lugha nvingine za Kibantu na Kiswahili, kuna masuala hayakufafanuliwa kwa uwazi, mengine yalikuwa na utata, na mengine yalionekana kutofautiana kati ya lugha moja na nyingine.Mathalani, ilielezwa kwamba lugha ina ama tungo zenye upinduzi wa kimahali chakimofolojia au zile zenye upinduzi wa kimahali cha kisemantiki. Pamoja na kuclezwa hivyo, haikuelezwa iwapo lugha moja inaweza kuwa na aina zote mbili za tungo. Hivyo, tatizo la ukiukwaji wa uhusiano wa udarajia wa dhima za kisemantiki na zakisarufi za viambajengo vya sentensi pamoja na masuala ambayo hayakufafanuliwa kwa uwazi katika tafiti zilizopita, kuliibuka haja ya kufanya utafiti unaoripotiwa katika tasinifu hii. Utafiti huu umechanganua Upinduzi wa Kiniahali katika Lugha ya Kiswahili. Utafiti ulikuwa na malengo mahususi manne. Mosi, kubainisha aina za tungo zenye upinduzi wa kimahali, vitenzi vinavyoruhusu na vile visivyoruhusu utokeaji wa tungo hizo. Pili, kubainisha vimahali vinavyoweza na vile visivyoweza kupinduliwa katika tungo. Tatu, kufafanua dhima za kisarufi za viambajengo vinavyohusika katika tungo zisizo na upinduzi wa kimahali na zile zenye upinduzi huo. Mwisho, kufafanua muundo wa taarifa na umuhimu wa kimawasiliano wa tungo zenye upinduzi. Uchanganuzi wa data umetumia misingi ya mkabala wa Saruti Leksia Amilifu ulioasisiwa na Bresnan na Kaplan mwishoni mwa miaka ya 1970. Utafiti ulifanyika katika Idara za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Data zilikusanywa kutoka katika vitabu 2 pamoja na watoataarifa 40. Data zilipatikana kwa njia za usomaji wa nyaraka, ushuhudiaji shiriki, upimaji wa usahihi wa kisarufi, usaili, na hojaji. Matokeo yanaonesha kwamba lugha ya Kiswahili inatungo zenye mapinduzi wa kimaana cha kimoforojia na zile zenye upinduzi wa kimaana yake na kithimu na kimahali. Na mtenda ambayc hajapinduliwa ni kiima, na aliyepinduliwa ni chagizo. Kuhusu muundo wa taarifa, katika tungo zenye upinduzi mada ni kimahali kilichopinduliwa na fokasi ni kithimu kilichopinduliwa. Aidha, tungo zenye upinduzi wa kimahali zina umuhimu wa umadaishaji wa kimahali, ufokalishaji wa kithimu, na ufokalishaji linganuzi wa kithimu. Kutokana na matokeo haya, inapendekezwa kwamba kufanyike utafiti kama huu katika lugha nyingine za Kibantu ambazo hazijafanyiwa utafiti iii kulinganisha na kulinganua ruwaza za upinduzi wa kimahali baina ya Kiwahili na lugha nyingine.Item Ujitokezaji wa falsafa ya Kiafrika katika Riwaya za kiethnografia za Kiswahili(University of Dar es Salaam, 2019) Mpalanzi, LameckUtafiti huu unachunguza ujitokezaji wa vipengele vya falsafa ya Kiafrika katika riwaya teule za kiethnografia za Kiswahili. Vipengele vilivyochunguzwa ni dini ya jadi, uganga na uchawi, uzazi, uhai na kifo na uduara wa maisha. Katika kuchunguza vipengele hivyo, riwaya zilizoteuliwa na kuchambuliwa ni Kurwa na Doto, Mirathi ya Hatari na Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka; Ntulanalwo na Bulihwali. Vilevile, utafiti ulilenga kubainisha namna vipengele teule vilivyomo katika riwaya vinavyoakisiwa katika jamii teule za Unguja, Njombe na Ukerewe. Aidha, utafiti ulilenga kuchunguza mwingiliano wa riwaya ya kiethnografia ya Kiswahili na falsafa ya Kiafrika. Kadhalika, utafiti unafafanua mehango wa falsafa ya Kiafrika katika maendeleo ya fani na maudhui ya riwaya teule. Katika kukamilisha malengo haya, data ilikusanywa maktabani na uwandani kwa kutumia mbinu ya udurusu wa maandiko maktabani, mahojiano, hojaji, ushuhudiaji na ushiriki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili kuanzia nyakati za ukusanyaji data hadi uchambuzi. Nadharia ya kwanza inaitwa Ontolojia ya Kibantu, na ya pili Sosholojia ya Fasihi. Ontolojia ya Kibantu ilituongoza kuchambua masuala yanayohusu falsafa yaKiafrika na Sosholojia ya Fasihi ilitusaidia kuhakiki masuala yanayohusu uhusiano wa fasihi na jamii. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa fasihi hubeba falsafa ya jamii kwa kuwa vipengele teule vya falsafa ya Kiafrika vinadhihirika bayana katika riwaya teule. Utafiti umethibitisha kuwa tambiko linachukua sehemu kubwa ya dini ya jadi, ambayo ndiyo mzizi wa imani ya Waafrika. Jamii hizi zina matambiko mengi, mathalani, jamii ya Wamakunduchi ina tambiko is Mwaka-kogwa, tambiko la kumaliza msiba,tambiko la uzazi, tambiko la unyago na tambiko la mazishi. Jamii ya Wabena ina tambiko la kafara (Kipongo), Nyumbanitu na Amalimilo. Kwa upande mwingine, Wakerewe wana tambiko la kuzaliwa, uzazi na kutanabahi katika pembe, tambiko la kumtoa mtoto nje,tambiko la harusi, tambiko la kuvundika ndizi, tambiko la ugonjwa na tambiko la mazishi. Pia, Wakerewe, wana tambiko la machifu huko Kitare, tambiko katika makumbusho ya Handebezyo na katika "Jiwe Linalocheza." Utafiti umebaini kuwapo kwa imani mseto katika jamii teule inayotokana na mwingiliano wa dini ya jadi na dini za kigeni. Kuwapo kwa imani mseto ni jitihada za jamii teule kutafuta utambulisho na ukubalifu wa kila kundi. Utafiti umebaini kuwa upo mpaka bayana kati ya fani ya uganga na uchawi kwa kuzingatia kigezo cha utendaji, dhima, kiwango cha nguvu-hai, miiko na ufantasia wa fani hizo. Uchunguzi katika riwaya na jamii teule umebaini kuwapo kwa makundi kumi (10) ya waganga na makundi mawili (2) ya wachawi. Utafiti unaonesha kuwa baadhi ya waganga na wachawi wanaishi maisha duni kwa kuwa hutumia gharama kubwa kununua viambato vya uganga na uchawi. Licha ya kufumbata falsafa mbalimbali za maisha, suala la uzazi katika jamii ya Ukerewe ni mfano dhahiri wa kuwapo kwa familia pana ya Kiafrika inayojumuisha watu-hai, waft' na watakaozaliwa. Sanjari na hilo, utafiti huu unaafiki kuwa kifo kwa Mwafrika si mwisho wa maisha kwani mfu huendelea kuwapo kama inavyoelezwa katika Ontolojia ya Kibantu. Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa maisha ya maana na halisi ni ya hapa duniani. Aidha, utafiti huu ulibaini kuwapo kwa uhusiano wa kiduara kati ya mtu, jamii na mfumo uliopo. Kiontolojia, utafiti umethibitisha kuwapo uhusiano wa kiduara kati ya Mungu, mizimu, wahenga, binadamu, wanyama na mimea, na vitu na mahali. Katika kudhihirisha fasihi inavyobeba falsafa ya jamii, utafiti huu umetambua kuwa fasihi na falsafa ya Kiafrika hutenda majukumu yanayofungamana. Mwisho, utafiti huu unabainisha kuwa falsafa ya Kiafrika ni malighafi na nyenzo muhimu katika uandishi wa fani na maudhui ya riwaya ya Kiswahili.Item Majukumu ya wahusika kijinsia katika nyimbo za watoto za Kiswahili na uhalisia wake katika malezi ya watoto nchini Tanzania(Chuo kikuu cha Dar es Salaam, 2019) Mosha, Doroth FelicianTasnifu hii ni matokeo ya mada ya utafiti ‘’ Majukumu’’ ya wahusika kijinsia katika nyimbo za watoto za Kiswahili na Uhalisia wake katika Malezi ya watoto nchini Tanzania’’ Tum’echunguza namna watunzi wa nyimbo za watoto walivyowateua wahusika kuwapa majukumu anuwai kwa mujibu wa jinsi zao. Vilevile, tumechambua maoni ya wanajamii (walimu, wanafunzi na wataalamu wa masuala ya jinsia) kuona namna wanavyogawanya majukumu kwa watoto wanapowatia malezi. Lengo ni kufanya ulinganishi ili kuona endapo kuna uhalisia wa majukumu ya kijimsia katika nyimbo za watoto na malezi ya watoto nchini Tanzania. Utafiti uliongozwa na malengo muhususi manne: Mosi, kubainisha wahusika waliojitokeza katika nyimbo za watoto kwa mujibu wa jinsi zao. Pili, kuchambua majukumu ya wahusika hao. Tatu, kujadili moni ya jamii kuhusu majukumu ya kijinsia katika malezi ya watoto na kulinganisha na yale ya nyimbo za watoto kwa watoto na jamii. Data zilizokusanywa kwa njia ya mahojiano, ushuhudiaji na maandiko mbalimbali ziifanikisha malengo tajwa. Data hizi zimewasilishwa na kuchambuliwa kwa njia ya kitaamuli kukiwa pia na matumizi ya uchambuzi wa kitakwimu na majedwali. Utafiti umeongozwa na nadharia za Skima ya kijinsia na uhalisia. Skima ya kijinsia ni nadharia ya mrengo wa jinsia inayoangazia namna mtoto anavyojifunza majukumu yanayomhusu kwa kuhushudia yale yanayofanywa na wanaume na wanawake wakiongozwa na utamaduni wa jamii husika. Nadharia ya uhalisia imezingatia ukweli na uyakinifu wa majukumu ya kijisnisia katika malezi ya watoto kama yalivyosawiriwa katika nyimbo za watoto ili kubaini kufanana na kutofautiana kwake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa: Mosi, wahusika wa kike ni wengi kuliko wahusika wa kiume na wamebebeshwa majukumu mengi. Pili, watunzi wa nyimbo za watoto wamesawiri mgawanyo sawia wa majukumu ya kijinsia ya wahusika. Tatu, maoni ya wanajamii yamebaini kutokuwa na unyoofu wa mgawanyo wa majukumu ya kijinsia katika malezi ya watoto. Hali hii huchangiwa na tofauti za kiutamduni na malezi ya kifamilia, mitazamo na itikadi tofauti, dini, elimu, tofauti za kihistoria na hatua ya maendeleo ilivyofikiwa katika familia au jamii husika. Hivyo, hakuna usahili wa kiuhalisia baina ya majukumu ya wahusika kijinsia katika za watoto na majukumu ya wahusika kijisinsia katika nyimbo za watoto umebainika kuwa na athari chanya na hasi kwa watoto na jamii.Item Ujitokezaji wa tashtiti katika fasihi ya Kiswahili: Uchunguzi wa kazi teule(University of Dar es Salaam, 2019) Daniel, Zawadi LimbeUtafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili ukiongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha mbinu zinazotumika kuunda tashtiti, kueleza dhima ya tashtiti na kuainisha tashtiti katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Uchunguzi wa ujitokezaji huu ulifanywa kupitia kazi teule za fasihi ya Kiswahili za: Kaptula la Marx 9Kezilahabi, 1999), Amezidi (Mohamed, 1995), Walenisi (Mkangi, 1995), na Miradi Bubu ya Wazalendo (Ruhumbika, 1992). Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchambuzi matini na mkabala wa kitaamuli. Aidha nadharia za semiotiki-jamii na Mwingiliano- matini ziliongoza utafiti huu. Matokeo katika utafiti huu yanaonesha tashtiti katika kzi teule ni mtindo wa kisanaa unaoundwa kwa kutumia mbinu za dhihaka, kejeli, ufyosi, matumizi ya tamadhali ya usemi hasa sitiari, tashbiha na uchuku ubeuzi, taswira na ishara, mandhari pamoja na ujenzi wa wahusika. Matokeo haya yanapingana na madai yaliyokwishatolewa na Msokile (1992), Mbonde (2002), Senkoro(2011), na Wamitila (2003) kwamba tashtiti katika fasihi ya Kiswahili hujitokeza kama kipengele cha kitamathali pekee, madai ambayo yalichukulia tashtiti kuwa kipengele kinachofungamanishwa na matumizi ya lugha pekee. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa tashtiti ni dhana pana, ambayo katika kujipambanua kwake inatumia si tu vipengele vya lugha na kitamathali, bali pia mbinu mbalimbali za kifani na kimaudhui. Vilevile, matokeo yanaonesha kuwa tashtiti ina dhima kuu tatu katika kazi teule za fasihi ya Kiswahili. Dhima hizi ni za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Katika dhima ya kisiasa tashtiti inahakiki uongozi, inakemea rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, inapinga ukoloni mamboleo na utegemezi wa misaada, na inatathimini utoaji wa haki na usawa. Katika dhima ya kiuchumi tashtiti inaumbua hali ya umaskini, na inashambulia hali ya utabaka. Kijamii tashtiti ina dhima ya kukosoa mfumo wa elimu, kuhakiki utamaduni na maadili na pia kuumbua hali duni za afya na uzazi . Aidha utafiti huu umependekeza aina tano za tashtiti ambazo ni tashtiti ya mtindo jumuishi, tashtiti –tamathali, tashtiti-husika, tashtiti-ufyosi na tashtiti-fiche. Kutokana na matokeo ya utafiti huu uainishaji huu ndiyo unafaa kumika katiak kazi za fasihi ya KiswahilItem Mkazo Katika Kiswahili Sanifu(University of Dar es Salaam, 2019) Mwendamseke, Faraja JaphetUtafiti huu ni wa kifonolojia uliochunguza mkazo katiak Kiswahili sanifu. Jumla ya watoa taarifa 20 wamehusika katika kutoa data iliyotumika katika utafiti huu. Watoa taarifa 10 walitoka kata ya Ngamiani Kati na Chumbageni katiak jiji la Tanga, mkoani Tanga. Watoa taarifa wengine 10 walitoka katiak Jiji la Tanga, mkoani Tanga. Watoa taarifa wengine 10 walitoka katika shehia ya Mkunazini na Shehia ya Malindi, UNGUJA MJINI, Zanzibar. Taarifa hizo zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ni wa kiidadi na kimaelezo ambao umefanyika kwa kuongozwa na nadharia ya Fonolojia Mizani. Data zilizokusanywa zilichunguzwa kwa kusikilizwa kwa makini na kwa kutumia program ya “Praat”. Aidha, matokeo ya utafiti huu yaonesha kuwa uchunguzi wa mkazo katika kiwango cha neon hujibainisha tofauti na mkazo katika kirai na sentensi. Mara nyingi mkazo msingi katiak neon hutokea katika silabi ya mwisho kasa moja, wakati mwingine mkazo msingi hutokea katiak katika silabi ya mwisho katika vihisishii. Kwa upande wa kirai na sentensi mkazo msingi hutokea katika neno la mwisho katiak tungo husika. Hata hivyo, katiak Kiswahili sanifu imebainika kuwa licha ya kuwepo mkazo msingi katika neno, kirai na sentensikuna aina nyingine pia za mkazo. Yaani mkazo upili, mkao utatu na mkazo dhaifu, kutegemeana na namna utamkaji unavyojidhihirisha katika neno, kirai na sentensi kuna aina nyingine pia za mkazo. Yaani mkazo wa pili, mkazo utatu na mkazo dhaifu, kutegemeana na namna utamkaji unavyojidhirisha katika viambajengo hivyo. Kwa hiyo, kila kiambajengo kinakiasi Fulani cha nguvumsikiko. Pia, licha ya ruwaza ya mkazo kuwa funge kama ilivyoelezwa na wataalamu wengine kama vile Halle naClements (1983) na Massamba (2011). Utafiti huu umeenda mbele zaidi na kubaini kuwa ruwaza ya mkazo inaweza kuathiriwa na michakato ya kifonolojia kama vile udondoshaji, michako ya kimofolojia kama vile uambatani na uradidi. Aidha, katika uamilifu wa mkazo utafiti huu umebaini kuwa na uaminifu ufuatao: kwanza ni kuwekewa nguvu katika silabi au neno wakati wa utamkaji ili kuonesha msigano wa msikiko katika viambajengo vinavyohusika. Pili, kuna wakati mkazo huwa na uamilifu wa kuonesha msisitizo katika kiambajengo kinachohusika yaani katika neno, kirai au sentensi. Tatu mara chache mkazo huweza kubadili maana ya msingi ya msingi ya neno, hutokea katika baadhi ya maneno mkazo unapohama. Aidha, kutokana na uamilifu wa mkazo tumeweza kutofautisha mkazo na kiimbo pamoja na kidatu katika katika Kiswahili sanifu. Hata hivyo, kuna mazingira mengine kiimbo na kidatu huweza kuathiri mkazo lakini athari hiyo ya kimsikiko haibadili uamilifu wa mkazo.