Uchanganuzi Kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya bunge la Tanzania

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu uchanganuzi kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya BJMT katika kipindi cha mwaka 1980 hadi 2014.Data ilikusanywa kwa mbinu za uchambuzi wa nyaraka, ushuhudiaji, hojaji na usaili na kuchambuliwa na kufasiriwa kwa mkabala wa uchanganuzi kilongo shirikishi na mpishano huru. Walengwa wa utafiti walikuwa Wabunge wa BJ MT. Nadharia iliyotuongoza ni Nadharia ya Staha ya Brown na Levmson (1987) inayodai kuwa , kuna kauli zenye kutweza staha na iii kauli hizo zikweze staha mzungumzaji anatakiwa kuzisuka kwa kutumia mbinu faafu za kistaha. Pia, tulizingatia maboresho ya Fraser (1990) anayedai kuwa ili mzungumzaji akweze staha lazima azungumze kwa kuzingatia kanuni zinazodhibiti majadiliano. Kutokana na uchanganuzi kilongo uliozingatia vipengele vya kinadharia, kanuni za Bunge na muktadha wa mazungumzo data tuliyoipata imetupa vipengele vinavyohusiana na kauli zenye kutweza au kukweza. Miongoni mwa kauli hizo ni matusi, kumshambulia Mbunge kuwa ni mnafiki au sio makini, kusema uongo, kuhamasisha uvunjifu wa sheria, kuonesha kuwa wenzio ni punguani, vichaa au wendawazimu, kujivuna au kubeza wengine, kumpa taarifa Spika (Kiti) au kutotii maelekezo yake, kutotumia neno 'Mheshimiwa' kabla ya jina la Mbunge, kauli za kibaguzi na mwisho kuzungumzia mambo ya siri ya Mbunge. Kwa upande wa kauli zenye kukweza staha, utafiti unaweka wazi kuwa ili zijitokeze ni lazima mzungumzaji ateue mbinu faafu za kistaha zitakazomwezesha kulinda utu wa wasikilizaji pamoja na makatazo yanayodhibiti matumizi ya lugha Bungeni. Mbinu hizo ni pamoja na ubadili haji msimbo, matumizi ya kauli ya kutendwa na kutendana, kunukuu, matumizi ya nafsi ya kwanza wingi, matumizi ya vitambulisho hadhi, uteuzi mzuri wa msamiati, matumizi ya njeo ya wakati uliopita //-Ii-// mahali pa wakati uliopo //-na-// wakati wa kuuliza swali na uepukaji. Kwa ujumla, utafiti umeonesha kuwa, uwepo wa kauli zenye kutweza staha Bungeni unatokana na kutotumia mbinu faafu za ki taha. Matokeo ya utafiti huu yanachangia maarifa mapya katika taaluma ya isimu-tumizi Y . Kiswahili hasa katika taaluma za pragmatiki, isimujamii na elimu-mitindo. Pia, yanachangia katika kipengele cha uchanganuzi kilongo kwa kupendekeza mbinu za uchanganuzi kilongo shirikishi na uchanganuzi kilongo mpishano huru kama mbmu za kuchambua na kufasiri data. Kipekee kabisa, utafiti huu unachambua kwa undani kipengele cha staha ambacho ni cha pragmatiki katika mijadala ya Bunge ili kuweza kupata ruwaza za lugha ya kibunge zenye kukweza staha. Ili kubainisha ruwaza za lugha ya kibunge tunapendekeza utafiti zaidi utakaobainisha vipengele vya kiisimu vinavyounda lugha hiyo. Pia, kuhusu mbinu za kistaha katika lugha ya Kiswahili kwa ujumla , tupendekeza tafiti nyingine kufanyika kwenye taasisi nyingine pia na katika mazmgua yasiyo rasmi.
Description
Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library (THS EAF PL8703.5.S94)
Keywords
Swahili literature
Citation
Sylivester, Johanes (2016) Uchanganuzi Kilongo wa kauli zenye kutweza au kukweza staha katika mijadala ya bunge la Tanzania, PhD Dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam
Collections