Utokeaji wa Yambwa na dhima zake katika Kimatengo Na Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2020
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Abstract
Utokeaji wa Yambwa na dhima zake katika Kimatengo Na Kiswahili Fokas Nchimbi Tasnifu ya Kiswahili (PhD) University of Dar es salaam, Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili 2020 Utafiti huu ulichunguza mazingira ya utokeaji wa yambwa na dhima zake katika Kimatengo na Kiswahili. Ili kufikia lengo hilo utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Sarufi ya Uamilifu wa Kileksika inayoeleza kwamba katika muundo wa kiambajengo kuna uwasilishwaji wa vipashio vya kileksika vyenye dhima za kisintaksia kama vile kiima cha kiarifu; na vile vyenye sifa za sententiki kama vile mtenda, mtendwa mtendewa. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi mawili. Kwanza, kubainisha sifa msingi zinazohalalisha utokeaji wa yambwa katika maumbo asilia ya vitenzi vya kimatengo na Kiswahili. Pili, kufafanua athari za unyambuzi katika utokeaji na dhima za yambwa katika na Kiswahili. Maswali ya utafiti huu yalikuwa mawili ambayo ni: sifa gani msingi zinaamua utokeaji wa yamba na dhima zake katika maumbo asilia ya vitenzi vya Kimatengo na Kiswahili? Unyambuzi wa vitenzi una athari gani katika mazingira ya utokeaji wa yambwa na dhima zake katika Kimatengo na Kiswahili? Data za utafiti huu ni wa kitaamuli, data za utafiti huu zilikusanywa kusini magharibi mwa Tanzania, katika vvijiji vitatu vya wilaya ya mbinga ambavyo ni Myangayanga, Kindimba na Wukilo. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia kuu nne, ambazo ni maandiko ya maktabani, hojaji, usaili, ushuhudiaji na vikundi vya majadiliano. Kwa sababu utafiti ni wa kitaamuli, data za utafiti zimewasilishwa na kuchanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa kufafanua nduni za kisintaksia na kisemantiki za yambwa kama zinavyoamuliwa na maumbo mbalimbali ya vitenzi vya Kimatengo na Kiswahili. Kulingana na malengo na maswali ya utafiti, matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa sifa ya kiwango cha uelekezi wa maumbo asili ya vitenzi ndiyo inayoamua hali ya uwasilishwaji wa nomino kapa, nomino moja hadi nomino mbili za yambwa, ambapo aina za yambwa huwa ni yambwa tendewa na yambwa tendwa. Pili kuna uwezekano wa kuumba maumbo nyambuzi mbalimbali katika Kimatengo na Kiswahili . maumbo hayo nyambuzi yanayoathiri mazingira ya uwasilishwaji wa yambwa na dhima zake kisintaksia na kisemantiki ni utendea, utendesha,utendeshea, utendano, utendeka,utendeano,utendesheano,ujirejea, utendua na utendwa. Hali kadhalika, matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa mazingira ya uwasilishwaji wa yambwa na dhima zake za kisintaksia na kisemantiki yanaamuliwa na aina ya umbo na maana msingi ya kitenzi na maana msingi ya nomino husika ya yambwa. Katika Kimatengo na Kiswahili kuna uwezekano wa kutokea kwa nomino mbili za yambwa, ambazo ni yambwa tendewa na yambwa tendwa. Aidha, matokeo yanaonesha kuwa katika Kimatengo hakuna maumbo tendwa yanayojitokeza kwenye vitenzi katika lugha nyingine za Kibantu kama vile Kiswahili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kuna haja ya kuendelea kukifanyia utafiti zaidi kipengele cha yambwa katika lugha za kibantu ili kubaini umahususi wa kila lugha kuhusu viashiria vya kisintaksia na kisemantiki vya yambwa. Katika kimatengo na Kiswahili kuna haja ya kufanya utafiti kuhusu kipengele cha kiambishi cha yambwa katika maumbo mbalimbali ya vitenzi vyake na kuhusu ukwezwaji unaoonesha umada wa nomino ya yambwa pamoja na kategoria nyingine muhimu katika sentensi za lugha hizo
Description
Available in print form, East Africana collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8876.N234)
Keywords
Swahili language,, Grammar,, comarative and general,, Word formation,, Matengo (African people)
Citation
Nchimbi, F(2020)Utokeaji wa Yambwa na dhima zake katika Kimatengo Na Kiswahili,Doctoral dissertation ,Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Dar es Salaam.
Collections