Ulinganishi wa lugha za ‘’Runyaċitara’’

Thumbnail Image
Date
2019
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo kikuu cha Dar es Salaam
Abstract
Utafiti, huu ulihusu ulinganishi wa lugha za ‘’Runyaċitara’’ ili kufanunua kama zina uhusiano wa kimnasaba baina yake au la. Malengo mahususi yaliyoshughulikiwa ni kubainisha historia ya lugha hizi, kufanunua kutofautiana na kufanana kulikopo kati ya lugha hizi na tatu ni kutathmini kama hizi ni lugha moja, makundi mawili au kila lugha inajitegemea. Nadharia ya mwanachano na Makutano ya lugha za kibantu na nadhariatete yake ya ndugu na ndugu wa mbali kiisimu ambazo ziliasisiwa na Massamba (2007) zimetumiwa kueleza historia ya lugha hizi pamoja na kutathamini uhusiano wa lugha hizi kwa kuegemea kiwango cha ukaribu kiisimu. Aidha, ya Isimu historian na linganishi ambayo mwasisi wake ni William Jones 1786 imetumiwa kuelezea vipengele vya kiisimu na msamiati wa msingi kisinkroniki na kidikronuki. Mikabala mchanganyiko imetumiwa katika utafiti huu, na maeneo ya utafiti yamehusisha Wilaya za Kabarole, Hoima, Mbarara na Kabale ambazo zimo nchini Uganda. Vilevile, usampulishaji hatua ulitumiwa kuchagua maeneo mahususi na watoa taarifa kimaksudi na pia kwa kutumia usampulishaji tajwa. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, kuptia maandiko, mahojiano, uthibitishaji kauli na usaili. Data hizi zilihusu historia ya wazungumzaji na lugha zaopamoja na taarifa za kiisimu; msamiati wa msingi, mfumo wa sauti na sauti mrejeo, mofolojia, ngeli za nomino na hali na njeo ili kufanunua uhusiano wa lugha hizi. Data zimechanganuliwa kwa kutumia mbinu linganishi, takwimu leksika, maelezo na programu ya ‘linganishi lugha kwa mfumo wa kompyuta’. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo nay a kitakwimu ili kuelezea uhusiano wa lugha za ‘’Runyacitara’’. Matokeo yanaonesha kwamba hizi ni lugha zenye mnasaba ambazo zilitokana na mame- lugha moja. Lugha hiz zinajibainisha katika makundi mawili ya Runyoro na Rutooro na kundi la Runyankore na Ruċiga kutokana na mabadiliko ya lugha na kila kundi ni ndugu ya mbali kwa kundi jingine. Hali ya lugha hizi tunayoiona leo hii inaweza kufafanuliwa kidikroniki kama matokeo yanavyoonesha mabadiliko ya lugha yaliyotokea kiisimu. Kwa upande mwingine, kwa sababu yawazungumzaji kutaka kujibainisha kama watu wa jamii tofauti huwa wanaibuka na miundo mipya ili kujitofautisha na wenzao. Hitimisho ni kwamba lugha hizi zina uhusiano wa kimnasaba kwa kuhusisha mfanano wa 85.39% katika msamiati wa msingi na vipengele vingine vya kiisimu. Matokeo ya uundaji upya yalionesha kwamba maumbo tunayoyaona leo hii ya;itokana na maumbo ya awali. Kwa hivyo, lugha hizi ni kundi moja la lugha lenye makundi ndani mwake ambayo ni lahaja. Matokeo haya yana mchango mkubwa katika kufafanua uhusiano wa lugha za Runyoro, Rutooro, Runyankore na Ruċiga kwa kuegemea historia ya wazungumzaji wake na maendelo ya lugha kiisimu, nadharia, utafiti umethibitisha kwamba hali ya lugha kisinkronia inaweza kufafanuliwa kidikronia na vilevile kuthibitisha kwamba mijongeo ya watu inaweza kusababisha mwanachano na makutano ya lugha. Aidha, matokeo yanachangia katika data za kisiimu za lugha za kibantu na nadharia ya isimu kwa ujumla pamoja na data zilizoko makavazini. Inapendekezwa kuwe na utafiti zaidi juu ya; lugha nyingine zinazoonesha mfanano na hizi; nafasi ya teknolojia katika mwachano na makutano ya lugha; athari ya uhusiano wa lugha hizi katika vipengele vingine vya kijamii na vipengele mahususi vya kiisimu katika lugha hizi. Aidha, kuna haja ya kuwa na usanifishaji wa mfumo rasmi wa ‘’Runyaċitara’’.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.T34A755)
Keywords
Bantu language, Runyacitara ( Nyoro language )
Citation
Asiimwe , C (2019) Ulinganishi wa lugha za ‘’Runyaċitara’’, Tasnifu ya uzamivu,Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam
Collections