Hadithi za wahenga

Permanent URI for this collection

Browse

Recent Submissions

Now showing 1 - 20 of 20
  • Item
    Mashaka hospitalini
    (East African Literature Bureau, 1971) Institute of Adult Education University of Dar es Salaam
    Mfululizo wa vitabu vya Juhudi ni matokeo ya Juhudi ya Chuo cha Elimu ya watu wazima,Chuo kikuu,Dar es Salaam.Katika Shabaha ya kuelimisha watu wazima ili kumvuta mtu mzima vimeandikwa kwa muundo wa hadithi,mazungumzo na majadiliano na mambo yanayowahusu watu wazima.
  • Item
    Lila na fila
    (Tanzania Longmans, 1966) Kiimbila, J. K.
    Hadithi hii inathibitisha ukweli wa methali "LILA NA FILA HAVITENGAMANI.INAONYESHA WAZI ukweliwa usemi wa mtaalamu William Shakespeare kwamba "MAOVU WAYATENDAO WANADAMU HUDUMU NAO HATA WAKISHAKUFA" wanadamu mara nyingi huwadhulumu wanadamu wenzao, lakini kwa bahati nzuri mzima nyota ni Mungu,Pengine dhulma yao hushindwa hatimaye Mwenyezimungu huyapindua maisha yao na kuwaonyesha wanadamu ni viumbe duni hata wakijifanya miungu wadogo.
  • Item
    Kisa cha Hamisi
    (Kenya Longmans, 1968) Omolo, Leo Odera
    Hamisi alipowasili Kisumu mjini alikuwa kijana maskini hohe hahe,hana nguo wala kazi. Baada ya mda si mrefu mambo yalimgeukia hamisi hivi sasa ni tajiri mkubwa mjini kisumu. Utajiri wa hamisi haukutokana na uhalifu wala dhulma,Bali ni kwa uaminifu mkubwa.Hamisi alionyesha moyo wa uthabiti na uaminifu kwa tajiri yake Shuka alipowavizia na kuwashikisha wezi waliotamani kuiba mali ya tajiri huyo.Je bosi huyo alifanyeje kwa Hamisi karibu usome hadithi hii.
  • Item
    Jua na upepo
    (East African Publishing House, 1968) Mtindi, Anne
    Jua na upepo ni mkusanyiko wa hadithi mbali mbali zenye maudhui tofauti ikiwemo mke mvivu,Msichana mtundu,Taabu za wanyama na Mistari ya pundamilia. Msomaji utajifunza mengi kuhusiana na hadithi hizi.
  • Item
    Dunia ngumu
    (Tanzania Publishing House, 1969) Chiume, M. W. K.
    Dunia ngumu ni hadithi inayoelezea kuhusiana na maisha,mambo yote yaliyoelezwa si mambo yaliyotendeka kweli. halikadhalika majina ya watu ,nchi hata kama yanafanana na watu wa nchi husika hawahusiani na watu wa nchi tunazozijua.Hivyo toka zamani hadithi hutufunza mengi ni matumaini yangu watu watakaosoma watajifunza katika hadithi hii.
  • Item
    Baada ya dhiki faraja
    (Tanzania Publishing House Ltd., 1969) Mushi, J.S
    Mtenda mema hulipwa mema,ndivyo wazee walivyosema.na baada ya dhiki faraja,Tulia shida zinapokuja.Kwani shida nyingi zikiingia ndipo furaha kubwa yakaribia
  • Item
    Mwasi
    (Heinemann, 1972) Zaidi, N
    Kijiji cha pachanga kilikuwa kimelogwa na madhehebu ya watu walioamini pepo. hili ilifanyika kwa kuiabudu miungu ya mito na ardhi.Miungu hii iliaminiwa kuongoza maisha ulimwenguni na sudi za maisha ya wanadamu.Hata ajabu za maumbile zilisababishwa na miungu.Mzee matata ndiye aliyekuwa mjumbe baina ya miungu na wanadamu.Mtu mzima huyu aliyekuwa amenenepa na aliyeogopwa na kuheshimiwa na watu wote.Mzee matata alisifika mno kwani ilisadikiwa alikuwa na uwezo wa kuzianzisha nguvu za miungu-nguvu ambazo ziliweza kuyaumbua,kuyaangamiza au kuyaneemesha maisha kwa kunuiza maneno machache
  • Item
    Sivyo ilivyo
    (Zanzibar publishers, 1970) Makungu, Hamidi Vuai
    Siku moja katika siku saba zinazojirudia zizo kwa zizo katika maisha yetu,Shungi baada ya kufikiri hali ya udhaifu wa maisha yake hasa kwa vile hakusoma na bahati yake ya kukosa kazi, kila alikotoka maofisini,viwandani hata kwa matajiri,aliamua kwenda kuangalia hali yake kwa mganga ili afanyiwe maarifa ya kazi.Shungi kadharauliwa na kila mtu pengine hata na Bi Nali mke wa rafiki yake,yawezekana hata na mzee Finya anamdharau shungi, Dharau ni nini? Kule kumuonea huruma mtu nayo ni dharau, unamdharau kwasababu kwasababu hawezi kujimudu.
  • Item
    Peke yangu mjini
    (Central Tanganyika Press, 1972) Mandao, Martha
    Ni hadithi inayomuangazia Ani (msichana) alikuwa katika jiji kubwa la Dar es salaam kuanza kazi kwa mara ya kwanza katika maisha yake. Mbali kutoka katika maisha yake ya kijijini,Mbali na wazazi wake,Jamaa zake,Walimu wake na sasa yupo mjini mahali ambapo anaona kila kitu ni tofauti kubwa.Mara tu alipofika alikuwa na matazamio makubwa juu ya maisha katika jiji lile kubwa akitazamia kuwa msichana wa kupata kila kitu kwa hali ya juu zaidi na kuona vitu vipya ambavyo katika kijiji chake hangeweza kuvipata.
  • Item
    Mfalme na majitu
    (East African Publishing House, 1972) Omolo, Leo Odera
    Ni hadithi za kikwetu zenye mkusanyiko wa masimulizi mbalimbali ikiwemo hadithi :- mfalme na waganga, njaa na maafa,shujaa na majitu,binti malidadi na waganga na maafa
  • Item
    Maisha yake Doctor Ludwig Krapf misionari wa kwanza wa Ost afrika
    (Evangelishe Mission, 1913) Wuga, Gleiss
    Doctor Ludwig Krapf ni hadithi inayosimulia maisha ya mmisionari wa kwanza wa ost afrika, Zamani mwa miaka ya 1822 kule ulaya katika nchi ya Dachi. Palikua na watu waliovuna ngano na miundu yao. Jua likiwa kali wakaona kiu tena wakachoka.
  • Item
    Kufikirika
    (Mkuki na Nyota, 1967) Robert, Shaaban
    KUFIKIRIKA ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia,Kaskazini imepakana na Nchi za Anasa,Kusini nchi ya majaribu,Mashariki Bahari ya kufaulu na magharibi safu ya milima ya jitihadi.Ramani ya nchi hiyo ni adimu kupatikana kwasababu nchi yenyewe haiandikiki ila hufikirika kwa mawazo tu.Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo.Wafikirika wengi nao ni wazazi mno, nyumba ina watoto wanane hata kumi na sita si jambo la ajabu.Jumla ya wafikikirika ni sawa na nusu moja ya makabila yote duniani. ina ufalme mkubwa kuliko falme zote za mataifa mengine,Raha inayopatikana katika nchi yakufikirika ni kama kama ile iliyo katka pepo, isipokuwa katika kufikirika kuna maradhi na mauti lakini katika pepo kuna uzima na maisha ya milele.Nchi hiyo ilitawaliwa na nasaba kubwa sana ya wafalme ambao waliungana kwa viungo vyao kama mkufu, lakini mfalme wa mwisho alichelewa kupata mtoto wa kumrithi. kitabu hiki kinasimulia habari ya mfalme huyo
  • Item
    Jero Sikitu
    (Tanzania Publishing House, 1972) Akwisombe, Jacob B.
    ''Jero si kitu ni hadithi inayoelezea juu ya maisha ya Afisa mmoja wa kilimo ambaye aliamini kwamba ingawaje madaraka yake yalimtaka aishi mjini na kufanya kazi katika makao makuu ya wizara, aliweza kuwa manufaa zaidi kwa wananchi kwa kuhamia katika kijiji kilichokuwa karibu na hapo mjini.Alilazimika kusafiri kila siku kwenda kazin kwake,lakini vile vile aliweza kupata nafasi baada ya saa za kazi na katika siku zake za mapumziko,kuwashauri wanakijiji hicho mambo ya kilimo,ingawa yeye,kama ilivyo kawaida kwa wengi wetu,alikuwa na matatizo yake binafsi yaliyokuwa na nguvu ya kuweza kumwondoa azma yake hiyo katu hakukata tamaa.
  • Item
    Mawaidha ya Wamuchuthe
    (East African Publishing House, 1969) Michuki, David N.
    Kwa vile lugha ya kiswahili ilivyoenea siku hizi na kutumiwa na Waafrika wasiofundishwa lugha hiyo na mama zao, si ajabu tukiona Waafrika wakiachana na kanuni zilizopo za utungaji wa mashairi na kutunga wanavyotaka wenyewe. Hii ni moja ya dalili ya maendeleo ya kisasa. Bila shaka wale waliozoea kuandika mashairi hawatapendezwa na kanuni mpya. Ubora wa mashairi ya asili ya kiswahili ni katika kuandika walivyoandika washairi waliotangulia, kusiwepo na mabadiliko hata kidogo. Lakini hakuna maendeleo bila mabadiliko.Kitabu hiki kilichofasiriwa na bwana Michuki kinafaa sana kusomwa katika shule nyingi iwezekanavyo kwasbabu ya mtindo wake utawashawishi watoto wetu kujua zaidi juu ya historia na hekima za babu zetu.Sina shaka kusema kuwa watu wazima pia watapendezwa hali kadhalika.
  • Item
    Hila za mzee kobe na hadithi nyengine
    (East african publishing house, 1969) Mdoe, Fred Jim
    Hila za mzee kobe ni mjumuiko wa hadithi za kikwetu 4, Zenye maudhui mbali mbali ikiwemo; kiwavi fedhuli,Kisa cha gumbo, mfalme na mhunzi
  • Item
    Chakula kiletacho afya
    (India Kuu press, 1945) Culwick, Arthur Theodore; Ratcliffe, B. J.
    kitabu hichi kinaelezea jinsi chakula kinavyotumika mwilini kuleta afya na vyakula viletavyo afya katika mwili
  • Item
    balaa la ukemwenza
    (Benedictine Publications Ndanda, 1960) Mlele, Amina
    Masimulizi haya ya kusisimua yameandikwa hasa kwa wanafamilia ambayo kuna mme mmoja na mke zaidi ya mmoja kaitka familia moja jinsi wanavyoishi katika maisha ya kila siku.
  • Item
    Hadithi kutoka nchi mbalimbali
    (Oxford University Press, 1971) Zaidi, Noorjehan
    Kitabu hiki kimekusanya hadithi kutoka nchi za Afrika Mashariki, bara Arabu, bara Hindi, Indonensia, China, Japan, Amerika ya Kaskazini, Uingereza, Ujerumani na Urusi. Hadithi hizi zimetafsiriwa na noorjehan Zaidi kwa ajili ya mafunzo ya vijana na wavulana wa Afrika Mashariki
  • Item
    Jua na Upepo na Hadithi nyingine
    (East African Publishing House, 1968) Matindi, Anne
    Masimulizi haya ya kusisimua yameandikwa hasa kwa watoto wa madarasa ya kwanza katika shule za Afrika mashariki. Hadithi hizi zilikusanywa na Anne Matindi, zilikua kwa lugha ya kiingereza na kutafsiriwa na Fred Jim Mdoe katika Lugha ya Kiswahili
  • Item
    AYO: Msichana wa wa Kiafrica
    (Oxford University Press, 1971) Arnott, Kathleen
    Hii ni tafsiri ya kiswahili ya ayo msichana wa kiafrika iliyotafsiriwa na Kathleen Arnott na kuchapishwa na Oxford University Press, London