Kona ya Kiswahili
Permanent URI for this community
Browse
Browsing Kona ya Kiswahili by Title
Now showing 1 - 20 of 32
Results Per Page
Sort Options
Item AYO: Msichana wa wa Kiafrica(Oxford University Press, 1971) Arnott, KathleenHii ni tafsiri ya kiswahili ya ayo msichana wa kiafrika iliyotafsiriwa na Kathleen Arnott na kuchapishwa na Oxford University Press, LondonItem Baada ya dhiki faraja(Tanzania Publishing House Ltd., 1969) Mushi, J.SMtenda mema hulipwa mema,ndivyo wazee walivyosema.na baada ya dhiki faraja,Tulia shida zinapokuja.Kwani shida nyingi zikiingia ndipo furaha kubwa yakaribiaItem balaa la ukemwenza(Benedictine Publications Ndanda, 1960) Mlele, AminaMasimulizi haya ya kusisimua yameandikwa hasa kwa wanafamilia ambayo kuna mme mmoja na mke zaidi ya mmoja kaitka familia moja jinsi wanavyoishi katika maisha ya kila siku.Item Chakula kiletacho afya(India Kuu press, 1945) Culwick, Arthur Theodore; Ratcliffe, B. J.kitabu hichi kinaelezea jinsi chakula kinavyotumika mwilini kuleta afya na vyakula viletavyo afya katika mwiliItem Diwani ya Lambert(East African literature bureau, 1971) Mnyampala, MathiasMashairi ya diwani ya Lambert yameandikwa na mshairi nguli wa mashairi na kuhaririwa na Mathias MnyampalaItem Dunia ngumu(Tanzania Publishing House, 1969) Chiume, M. W. K.Dunia ngumu ni hadithi inayoelezea kuhusiana na maisha,mambo yote yaliyoelezwa si mambo yaliyotendeka kweli. halikadhalika majina ya watu ,nchi hata kama yanafanana na watu wa nchi husika hawahusiani na watu wa nchi tunazozijua.Hivyo toka zamani hadithi hutufunza mengi ni matumaini yangu watu watakaosoma watajifunza katika hadithi hii.Item Elisi katika nchi ya ajabu(Sheldon Press, 1940) Carroll, LewisElisi katika nchi ya ajabu ni mfululizo wa hadithi mbalimbali , hii ni hadithi inayomuelezea mzungu aliyewapenda watoto na kuwasimulia habari tamu sana za ndoto ikiwemo habari za mtoto yule katika nchi ya ajabu.Item Hadithi kutoka nchi mbalimbali(Oxford University Press, 1971) Zaidi, NoorjehanKitabu hiki kimekusanya hadithi kutoka nchi za Afrika Mashariki, bara Arabu, bara Hindi, Indonensia, China, Japan, Amerika ya Kaskazini, Uingereza, Ujerumani na Urusi. Hadithi hizi zimetafsiriwa na noorjehan Zaidi kwa ajili ya mafunzo ya vijana na wavulana wa Afrika MasharikiItem Hila za mzee kobe na hadithi nyengine(East african publishing house, 1969) Mdoe, Fred JimHila za mzee kobe ni mjumuiko wa hadithi za kikwetu 4, Zenye maudhui mbali mbali ikiwemo; kiwavi fedhuli,Kisa cha gumbo, mfalme na mhunziItem Jero Sikitu(Tanzania Publishing House, 1972) Akwisombe, Jacob B.''Jero si kitu ni hadithi inayoelezea juu ya maisha ya Afisa mmoja wa kilimo ambaye aliamini kwamba ingawaje madaraka yake yalimtaka aishi mjini na kufanya kazi katika makao makuu ya wizara, aliweza kuwa manufaa zaidi kwa wananchi kwa kuhamia katika kijiji kilichokuwa karibu na hapo mjini.Alilazimika kusafiri kila siku kwenda kazin kwake,lakini vile vile aliweza kupata nafasi baada ya saa za kazi na katika siku zake za mapumziko,kuwashauri wanakijiji hicho mambo ya kilimo,ingawa yeye,kama ilivyo kawaida kwa wengi wetu,alikuwa na matatizo yake binafsi yaliyokuwa na nguvu ya kuweza kumwondoa azma yake hiyo katu hakukata tamaa.Item Jua na upepo(East African Publishing House, 1968) Mtindi, AnneJua na upepo ni mkusanyiko wa hadithi mbali mbali zenye maudhui tofauti ikiwemo mke mvivu,Msichana mtundu,Taabu za wanyama na Mistari ya pundamilia. Msomaji utajifunza mengi kuhusiana na hadithi hizi.Item Jua na Upepo na Hadithi nyingine(East African Publishing House, 1968) Matindi, AnneMasimulizi haya ya kusisimua yameandikwa hasa kwa watoto wa madarasa ya kwanza katika shule za Afrika mashariki. Hadithi hizi zilikusanywa na Anne Matindi, zilikua kwa lugha ya kiingereza na kutafsiriwa na Fred Jim Mdoe katika Lugha ya KiswahiliItem Karibuni wageni watukufu(1960) Karama, SaidMashairi haya yakitungwa wakati H.H Sultani wa Unguja alipokua yupita Mombaza kwenda katika mapumziko yake huyo ulaya ya ingereza tarehe 21 jubi 1960. Mtunzi ni Al- Ustada Said Kalama wa Kileleni MombazaItem Kisa cha Hamisi(Kenya Longmans, 1968) Omolo, Leo OderaHamisi alipowasili Kisumu mjini alikuwa kijana maskini hohe hahe,hana nguo wala kazi. Baada ya mda si mrefu mambo yalimgeukia hamisi hivi sasa ni tajiri mkubwa mjini kisumu. Utajiri wa hamisi haukutokana na uhalifu wala dhulma,Bali ni kwa uaminifu mkubwa.Hamisi alionyesha moyo wa uthabiti na uaminifu kwa tajiri yake Shuka alipowavizia na kuwashikisha wezi waliotamani kuiba mali ya tajiri huyo.Je bosi huyo alifanyeje kwa Hamisi karibu usome hadithi hii.Item Koja la lugha(Oxford University Press, 1969) Robert, ShaabanKwa asili shairi hili liliandikwa na Francois Marie Arouet de Voltaire aliyeishi zamani za 1694-1778, Karne mbili na nusu zilizopita. Huyu ni mmoja wa walimu wakuu na mwandishi bora kabisa wa kifaransa.Kwa tafsiri ya kiingeleza iliyofanywa na Joseph McCabe shairi hili lilipangwa kwa beti kumi za mistari 234.Kwa tafsiri ya kiswahili limeandikwa na nguli Shaaban Robert na kupangwa kwa beti 48 za mistari 240,kila ubeti mistari mitano. Usanifu wa shairi hili wapendeza na kufikirisha sana.Item Kufikirika(Mkuki na Nyota, 1967) Robert, ShaabanKUFIKIRIKA ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia,Kaskazini imepakana na Nchi za Anasa,Kusini nchi ya majaribu,Mashariki Bahari ya kufaulu na magharibi safu ya milima ya jitihadi.Ramani ya nchi hiyo ni adimu kupatikana kwasababu nchi yenyewe haiandikiki ila hufikirika kwa mawazo tu.Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo.Wafikirika wengi nao ni wazazi mno, nyumba ina watoto wanane hata kumi na sita si jambo la ajabu.Jumla ya wafikikirika ni sawa na nusu moja ya makabila yote duniani. ina ufalme mkubwa kuliko falme zote za mataifa mengine,Raha inayopatikana katika nchi yakufikirika ni kama kama ile iliyo katka pepo, isipokuwa katika kufikirika kuna maradhi na mauti lakini katika pepo kuna uzima na maisha ya milele.Nchi hiyo ilitawaliwa na nasaba kubwa sana ya wafalme ambao waliungana kwa viungo vyao kama mkufu, lakini mfalme wa mwisho alichelewa kupata mtoto wa kumrithi. kitabu hiki kinasimulia habari ya mfalme huyoItem Kwanza uanze kupanda(1963-05-18) Mwanahewa, R.AItem Lila na fila(Tanzania Longmans, 1966) Kiimbila, J. K.Hadithi hii inathibitisha ukweli wa methali "LILA NA FILA HAVITENGAMANI.INAONYESHA WAZI ukweliwa usemi wa mtaalamu William Shakespeare kwamba "MAOVU WAYATENDAO WANADAMU HUDUMU NAO HATA WAKISHAKUFA" wanadamu mara nyingi huwadhulumu wanadamu wenzao, lakini kwa bahati nzuri mzima nyota ni Mungu,Pengine dhulma yao hushindwa hatimaye Mwenyezimungu huyapindua maisha yao na kuwaonyesha wanadamu ni viumbe duni hata wakijifanya miungu wadogo.Item Maisha yake Doctor Ludwig Krapf misionari wa kwanza wa Ost afrika(Evangelishe Mission, 1913) Wuga, GleissDoctor Ludwig Krapf ni hadithi inayosimulia maisha ya mmisionari wa kwanza wa ost afrika, Zamani mwa miaka ya 1822 kule ulaya katika nchi ya Dachi. Palikua na watu waliovuna ngano na miundu yao. Jua likiwa kali wakaona kiu tena wakachoka.Item Mashairi yangu(T.P.M book departmant, 1967) Zani, Z.M.Skitabu hiki cha mashairi yangu kina jumla ya mashairi 19 ambayo ni, Jana usiku niliota ndoto, Nilipigwa fumbo najibu kwa fumbo,Mwanangu waenda nchi za mbali, wasia wako baba una mambo si haba, mgeni kumpokea kumbe ni kujitongea, mwizi namchukia sana, Paliondokea mzee hakika, Ndugu watano walizaliwa, fumbo jingine la tatu hili, Aoaye mbali na kwao asipodanganya atadanganyika, Maua, Maskini, Tajiri, Duniani nifanyaje nione raha moyoni? Binadamu hatosheki, Vilima vya shimba, Duniani raha ya mtu katika mambo matatu, Msomaji hodari na Kalamu yangu sasa twaachana