Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "Bantu languages"
Now showing 1 - 12 of 12
Results Per Page
Sort Options
Item Athari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzo(University of Dar es Salaam, 2014) Malindi, BakitaUtafiti huu unahusu Athari za matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo, uliofanyika katika mkoa wa Mara manispaa ya Musoma katika kata za Mwisenge, Iringo, Mkendo, Nyakato na Kamnyonge. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 40 ambapo wanawake walikuwa 20 na wanaume walikuwa 20, vilevile kila kata ilitoa watafitiwa 8. Utafiti huu ulilenga kwanza kubaini matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Pili, kubainisha makundi ya jamii yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa kuzingatia jinsi, umri na kiwango cha elimu. Tatu, kueleza sababu za kutumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo.Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha wazi kuwa kuna baadhi ya matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Matamshi hayo ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo hutokana na matumizi ya mara kwa mara ya lugha ya Kikwaya, kutopata elimu na kutumia lugha mbili au zaidi katika eneo moja. Utafiti huu pia umedhihirisha makundi ya jamii ya watafitiwa yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo. Makundi hayo mtafiti ameyagawa katika sehemu mbili, yaani kuna makundi ya watafitiwa wanaotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa wingi, na kuna makundi ya watafitiwa wasiotumia sana matamshi ya Kikwaya. Makundi yanayotumia sana matamshi ya Kikwaya ni wazee (72%), wakulima (74%), wasiosoma (72%), wanawake (70%) na wafanyabiashara (60%). Hali kadhalika makundi ya watafitiwa yasiyotumia sana matamshi ya Kikwaya ni vijana (39%),waliosoma shule (48%), wanaume (52%) na wafanyakazi (45%).Item A comparative study of Ruri, Jita and Kwaya languages of the Eastern shores of Lake Nyanza(University of Dar es Salaam, 1977) Massamba, David Phineas BhukandaIn this work a comparative study of Ruri, Jita and Kwaya “languages” of the eastern shores of Lake Nyanza, in Musoma District, has been made. The aim is to try to establish whether these so-called “languages” are really separate languages or are mere dialects of one common (parent) language. The introductory part of the work surveys the existing views as regards to these “languages” and their validity. Section II mainly concerns the methodological approach. Section III is an overview of previous classification of these “language” Vs ‘Dialect’ with a view to shading more light to the work intended. Section V embodies the main body of the work. Under this a comparison of two major items has been made: (a) A set of lexical items (b) A set of grammatical items. The work contains an Appendix at the end. These are samples of tenses.Item Dhamira za nyimbo za harusi za wakerewe na mabadiliko ya jamii(University of Dar es Salaam,, 2012) Mugassa, Anna Helen FaustinTasinifu hii ni matokeo ya utafiti kuhusu Dhamira za Nyimbo za Harusi za Wakerewe na Mabadiliko ya Jamii. Utafiti ulikusudia kuchunguza mabadiliko ya jamii ya Wakerewe jinsi yanavyoakisiwa na dhamira za nyimbo za harusi za Wakerewe. Nyimbo kumi zilizoimbwa kuanzia miaka ya 1970 hadi mwaka 2010 ndizo zilizochungunzwa katika utafiti huu. Nyimbo hizo zimekusanywa kutoka vijiji vya Bukindo na Buzegwe katika wilaya ya Ukerewe.Nyimbo za harusi kumi zilizokusanywa zilichambuliwa ili kuweza kubainisha mabadiliko ya jamii yanavyoakisiwa na dhamira katika jamii ya Wakerewe. Aidha, nadharia ya Sosholojia ilitumika katika uchambuzi wa data. Njia za ushuhudiaji na mahojiano zilisaidia kupata data katika kutimiza lengo la kuchunguza dhamira na mabadiliko ya jamii. Utafiti wetu ulibaini kuwa nyimbo za harusi za Wakerewe huakisi mabadiliko yanayojitokeza katika jamii. Mabadiliko yaliyoakisiwa katika dhamira nyimbo hizo ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuingia kwa ugonjwa wa UKIMWI na kuibuka kwa imani za ushirikina kuhusu maalbino.Mapendekezo ya utafiti huu yalitolewa kwa watafitiwa kufanya tafiti nyingi zaidi katika fani na maudhui kwenye nyimbo za harusi za jamii mbalimbali nchiniItem Dhima ya mhusika bibi katika ngano za kifipa(University of Dar es Salaam, 2016) Waivyala, MargarethUtafiti huu ulihusu Dhima ya mhusika Bibi katika ngano za Kifipa. Malengo mahususi ya utafiti huu ni; kubainisha sifa za mhusika Bibi katika ngano za Kifipa, kueleza dhima za kifani na kimaudhui za mhusika Bibi katika ngano za Kifipa na kuchunguza uhusiano wa usawiri wa mhusika Bibi katika ngano za Kifipa na masuala mbalimbali ya kijamii. Vifaa vilivyotumika katika utafiti huu ni pamoja na kalamu na daftari, kamera ya picha tuli, kompyuta pakatwa, kinyonyi na simu ya mkononi. Mbinu zilizotumika ni; mbinu ya maktabani, mbinu ya uwandani, ushiriki/ushuhudiaji, majadiliano na mahojiano. Pia, data zilipatikana kwa kutumia maswali ya mwongozo wa majadiliano na mahojiano. Data zilichakatwa na kuchambuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Uhasilia na Nadharia ya Semiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa mhusika Bibi katika ngano za Kifipa anasawiriwa kwa mtazamo chanya kutokana na umuhimu wake na sifa zake katika kujenga msingi na imani ya jamii ya Wafipa. Vilevile, tumebaini kuwa pamoja na kuwa Bibi ni mhusika binadamu kinyume cha kazi za fasihi andishi, Bibi hufuata kaida za kingano katika kuwasilisha mambo mbalimbali katika jamii. Katika mtiririko wa ngano hizi za Kifipa, Bibi amesawiriwa katika hali chanya tu akiwa mstari wa mbele katika kutetea mambo mbalimbali katika jamii kama vile upendo wa dhati, utii, uvumulivu, kupinga unyanyasaji katika jamii na mwongozaji wa mbinu mbalimbali za kukabiliana na mambo yanayokwamisha maendeleo ya jamii. Mwisho, utafiti huu umetoa mapendekezo ya maeneo yanayohitajika kufanyiwa utafiti zaidi ili kuinua wigo wa wahusika katika utanzu wa ngano na fasihi simulizi kwa ujumla.Item The locative in Vunjo(University of Dar es Salaam, 1979) Mcha, YohanaThis study is an attempt at characterising the LOCATIVE category in Kivunjo language. The work is in two parts. Part one describes the semantic features associated with the concept of place and examines how these senses are surfaced in the expressions of place in Kivunjo. Place can be conceived of in many different ways depending on how we treat place. The static man and dynamic man view place differently. Many more diversified views would result from the conception of place depending on whether place is static or dynamic. Generally however, any conception of place would reflect the following important features. Place must be considered in terms of the up-down, left-right, back-front near-far, inside-outside opposition. Also important are the static-dynamic relations of place. If the dynamic aspects are taken count of, then place will be considered as a goal, a source or a path of an object. This study considers how Kivunjo reflects some of these semantic distinctions in the locative expressions. The morphological and syntactic modulations of the locative in Kivunjo have a strong bearing towards the Proto-Bantu locative cases. The description reveals that like most other Bantu languages, Kivunjo derives locatives from the Proto-Bantu locative classes 16 and 17. The HA and KU locative markers find reflexes in Kivunjo and their semantic coverage has been retained. MU is not reflexed in Kivunjo to cover the inside locational relations. Locative suffix-NYI which would have logically covered the inside locational relations in the absence of the MU class in Kivunjo assumes much greater semantic coverage than the Proto-Bantu INYI. Furthermore several other forms that bear no morphological resemblances to the Proto Bantu forms are cited in the study. Kivunjo therefore utilizes the HA and KU classes concords, the NYI suffix, bare substantives and other complex constructions in the locative expression. Part two describes the syntactic characteristics of the locative in Kivunjo. It focuses on the two grammatical categories of subject of an object of in sentences where the locatives are involved. It therefore goes about showing that the Locatives can function as subject and object of sentences in Kivunjo. Traditional studies about sentence structure assume that every sentence structure must have a nominal subject. Locatives are not nominals according to these studies. Locatives answer the question “where”. Place constructions would therefore normally function as adverbials of place in sentence structure. Although the same studies would accept “Moshi, the market and similar place names as nominals, they still consider them nominals of the lower order; i.e., they do not refer to entities of the first order (Lyons:1977). In surface sentence structure these place names can function as subjects of sentences, as in: (1a) Moshi is cold. Loc. + COPULA + a (2a). The market has a lot of people. Loc v object According to the theory of immediate constituents, these sentences have locative subjects. They are the left most occurring elements in the sentence structures, and they are also the topics or the Themes of the sentences, and they are also the agreement (singular subject, singular verb) in the sentences in which they occur. But transformational grammarians claim that these sentences can be paraphrased in the following way: 1b. There is coldness in Moshi. 2b. There are a lot of people at the market. According to transformationalists, the strings in 1a. and 2a. are not kernel sentences because of the fact that they could be paraphrased as 1b and 2b. The use of There in both cases to stand for the absent subjects is a further proof that the locatives in 1a and 2a are not subjects of the sentences. The author goes about showing that the grammatical category of subject hood can be occupied by the locative in Kivunjo. Since in Kivunjo, as in any other Bantu languages, all nominals 1 functioning as subjects control all grammatical agreement in the sentences they occur, the feature belonging to the locative class is copied onto any piece it governs, as the subject of the sentence. The object slot in sentence structure is occupied by nominal. Leech (1975) writes on objects saying: a) Like the subject, the object of a clause is a noun phrase; or a nominal clause b) The object usually refers to the person or thing etc., affected by the action of the verb. c) The object normally follows the verb phrase. (page 256). Since the exercise on showing that the locatives can function as subjects of sentences has yield positive results, providing that the locative can function as the object of the sentence is not difficult. The study fulfills the three conditions proposed by Leech above. Section 2:2 focuses on the Locative under major syntactic rules. The rules selected are those that would involve the grammatical categories of subject and object, of sentences. These rules are Passivisation, Topicalization, Relativization, Pronominalization and Tough Movement. According to Keenan (1976) in his Accessibility Hierarchy, the subject and the object of a sentence can easily be relativized, passivized, pronominalized, topicalized and tough moved. The claim is proved positively in this study. This study will be useful in two ways. First it is one of the earliest attempts to describe Kivunjo syntax, a field which is relatively untouched. The findings will provoke the interest of other scholars who might be interested in the field and especially those who might have better ideas on the Kivunjo language. Secondly, the findings might be a contribution to the field of syntactical analyses of languages in an attempt to pinpoint those features in the syntax of world languages that are universal. Methodological note: The work is mainly based on the author’s intuition about her own language backed by wide library research. Views have been drawn from important authors on Bantu languages and other linguists of the world. A few but limited contacts were made with other speakers of Kivunjo especially on the first part of the study. A note on Tone in Kivunjo. In Kivunjo, Tone is phonemic. There are two tones, falling tone and rising tone. In this study, tone will not be marked.Item Maana ya majina ya asili katika jamii ya Kiuru(Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 2013) Azael, RhodasiaUtafiti huu unahusu maana za majina ya asili. Mpaka sasa hakuna utafiti ambao umefanyika kuhusu maana za majina ya asili katika jamii ya Wauru. Kwa hiyo utafiti huu unalenga kuchunguza maana ya majina ya asili katika jamii ya Wauru. Utafiti umejikita katika kubainisha mfumo wa majina ya asili, kuchunguza asili ya majina, maana mahususi ya baadhi ya majina ya jamii ya Wauru, pamoja na umuhimu na mchango wa majina katika utamaduni wa Wauru. Utafiti umefanyika mkoani Kilimanjaro, wilaya ya Moshi vijijini katika vijiji vya Materuni, Mruwia, Kyaseni na Mwasi. Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni pamoja na: usampulishaji, ukusanyaji, uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data ya utafiti ni ya kutoka uwandani ambapo mtafiti alikusanya data kupitia hojaji na dodoso kutoka kwa watafitiwa na kuzifanyia uchanganuzi. Kazi imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza ina utangulizi unaofafanua usuli wa utafiti, tamko la utafiti, malengo ya utafiti, umuhimu wa utafiti, na eneo la utafiti. Sura ya pili inahusika na mapitio ya maandiko na kiunzi cha Nadharia ya Uumbaji iliyotumika kama mhimili wa utafiti huu. Sura ya tatu imehusika na mbinu na njia za utafiti zilizotumika katika kufanikisha utafiti huu. Mbinu zilizotumika ni ya pamoja na kubaini sampuli na kufanya usampulishaji ambapo mtafiti alitumia njia ya mahojiano na hojaji ili kupata taarifa za utafiti huu toka kwa watafitiwa. Sura ya nne, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data kama zilivyopatikana kutoka uwandani. Data zimegawanyika katika sehemu nne: ambapo sehemu ya kwanza imebainisha mfumo wa majina ya asili ya jamii ya Wauru, sehemu ya pili imetoa ufafanunuzi kuhusu asili ya majina ya jamii ya Wauru, sehemu ya tatu imetoa ufafanuzi kuhusu maana mahususi ya baadhi ya majina ya jamii ya Wauru na sehemu ya nne imejadili umuhimu na mchango wa majina katika utamaduni wa Wauru. Sura ya tano imegawanyika katika sehemu tatu; sehemu ya kwanza inaelezea matokeo ya utafiti ambapo utafiti umebaini kuwa majina mengi ya asili yanayotolewa katika jamii ya Wauru, yamekuwa yakipungua siku hadi siku kutokana na kuingia kwa majina ya kigeni. Aidha, utafiti umebaini kuwa majina katika jamii ya Wauru hayatolewi kiholela, bali hutolewa kwa kuzingatia mazingira halisi ya uzaliwaji wa mtoto na matatizo ama faraja alizokuwa nazo mama kipindi au/na baada ya ujauzito. Pia, utafiti umegundua kuwa asili ya majina ya Kiuru hufungamana na mambo makuu nne: mosi tabia, maumbile au muonekano wa mtoto pindi anapozaliwa au wakati wa makuzi, pili matukio mbalimbali ya kijamii, tatu vipindi mbalimbali katika jamii ya Wauru, nne misingi ya imani na desturi za jamii ya Wauru.Item The structure of Kiswahili sentences: a transformational generative approach(University of Dar es Salaam, 1990) Mgullu, Richard SThis study is an attempt to make a precise structural analysis of Kiswahili sentences within the paradigm of Transformational Generative Theory. Chapter one is an introduction to this study. It includes, among other things, a brief account of the origins and development of Kiswahili, the statement of problem, objectives, and hypotheses. It also includes the review of literature, the theoretical framework and the methodology. Chapter two is devoted to the simple sentence in Kiswahili. The simple sentence is discussed by using its immediate constituents; the simple noun-phrase and the simple verb-phrase. The central thesis here is that the structure of a simple sentence depends, to a larger extent on the type of the verb which is used in a particular sentence. We illustrate how intransitive, intensive, monotransitive and ditransitive verbs affect the final structure of the simple sentence. It is finally concluded that a simple sentence must not have any coordination or subordination. Chapter three deals with the compound sentence. A very clear link between the compound and the simple sentence is established. The link is that a compounds sentence is an outcome of the coordination of two or more simple sentences. The transformations which are involved in the coordination of simple sentences are discussed. We conclude this chapter by positing a condition that a compound sentence must not contain any embedded sentence. Chapter four deals with the complex sentence in Kiswahili. It is established that the complex sentence is clearly distinguished from the other types of sentences in view of the fact that the complex sentence - and only the complex sentences - contain embedded sentences which are subordinate to their matrix sentences. The conclusion which is drawn in Chapter Five is that a Transformational model is very useful in any sound discussion on the structure of Kiswahili sentences, when one considers its ability to characterize the intrinsic linguistic competence of the speakers.Item Toni katika nomino za lugha ya ki-konongo(University of Dar es Salaam,, 2012) Mashauri, Michael A.Lugha nyingi za ki-Bantu ni lugha zenye toni (taz. Nurse na Philippson 2003: 8). Pamoja na ukweli huo kubainishwa, na wataalamu mbalimbali kujaribu kuchanganua vipengele vya toni katika lugha za ki-Bantu bado lugha nyingi hazijafanyiwa utafiti wa kutosha na nyingine hazijaandikiwa kabisa. Miongoni mwa lugha ambazo hazijaandikiwa ni lugha ya ki-Konongo. Hivyo basi, utafiti huu unahusu toni katika nomino za lugha hii katika kujaribu kuziba pengo hili. Data zilizotumika katika utafiti huu ni nomino zilizokusanywa uwandani katika kijiji cha Inyonga na Mtakuja tarafa ya Inyonga, Wilayani Mlele, Mkoa wa Katavi. Data zilikusanywa kwa hojaji, mahojiano na kurekodiwa kwa kinasasauti aina ya MP3 IC recorder na kuchambuliwa kwa mbinu ya uchanganuzi wa data kimada. Katika uchanganuzi wa data tumetumia nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru iliyoasisiwa na Goldsmith (1976) ambapo vipengele vya kifonolojia vimewakilishwa katika rusu huru. Utafiti huu umegusia vipengele vya kifonolojia kama vile irabu, konsonanti, silabi na michakato ya kifonolojia inayoathiri toni. Aidha, tumezungumzia vipengele vya kimofolojia vinavyogusa kipengele cha toni kama vile uradidi na mwambatano wa nomino. Imebainika pia lcuwa toni za lugha hii ni tabirifu na huwa na kiinitoni lcinachopachikwa katika kiambishi awali kitangulizi kwa mashina ya nomino yasiyo na kiinitoni; yaani nomino za ngelitoni ya I; katika ngelitoni ya II kinapachikwa katika kiambishi awali kitangulizi na silabi ya mwisho kasoro moja na zile za ngelitoni ya III na IV kiinitoni kinapachikwa katika kiambishi awali kitangulizi na silabi ya mwisho ya shina. Kwa upande wa viambishi ni kiambishi awali kitangulizi na viambishi vya mahali pekee ndivyo vyenye kiinitoni na huwa na tonijuu. Vilevile kuna kanuni kadhaa ambazo zimejibainisha kama vile upachikaji kiinitoni, usambaaji tonijuu ya mwisho, ushukajitoni kihatua, upandaji tonichini, uundaji tonipanda au tonishuka na kanuni za uhusishaji KTM na kiinitoniItem Uainishaji wa ngeli za nomino za kikinga: mtazamo wa kimofolojia na kisemantiki Jimson Nasson Sigimba(University of Dar es Salaam, 2014) Sigimba, Jimson NassonMalengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuziainisha ngeli za nomino za Kikinga kwa mtazamo wa kimofolojia na kisemantiki na kujua idadi yake. Aidha, ufafanuzi wa mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki na dhima zinazojitokeza katika viambishi ngeli vya nomino za Kikinga umeshughulikiwa. Utafiti huu umefanyika katika vijiji vya Ikonda, Iwawa, Tandala na Bulongwa Wilayani Makete ambamo watafitiwa 32 kutoka vijiji hivyo waliteuliwa. Njia za ukusanyaji wa data zilizotumika ni hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Nadharia ya Mofolojia Asilia iliongoza utafiti huu ili kuweza kufafanua dhima mbalimbali zinazojitokeza katika viambishi ngeli vya nomino za Kikinga. Utafiti huu umegawanyika katika sura tano. Sura ya Kwanza inahusu maelezo yahusuyo eneo la utafiti, usuli wa tatizo, mfumo wa sauti za Kikinga, historia ya Wakinga, michakato ya kimofolojia, malengo ya utafiti, maswali na umuhimu wa utafiti na msingi wa nadharia. Katika Sura ya Pili, machapisho mbalimbali yaliyohusu uainishaji wa ngeli katika lugha za Kibantu yamepitiwa ili kuweza kujua namna ya kutafiti mada husika kwa kutumia mbinu za wataalamu waliotangulia. Sura ya Tatu inahusu mbinu za utafiti zilizotumika katika ukusanyaji wa data. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data iliyokusanywa uwandani umefafanuliwa katika Sura ya Nne. Katika sura hii ngeli za nomino za Kikinga zimeainishwa kwa kutumia kigezo cha kimofolojia na kisemantiki. Utafiti huu umebaini pia kuwa ngeli za Kikinga huanza na Irabu Tangulizi (IT) kisha kufuatiwa na Kiambishi Ngeli (Kng) na Shina (Sh). Kiambishi ngeli cha nomino (Kng) ndicho kilichotumika kuainisha ngeli za nomino za Kikinga na sio irabu tangulizi (IT). Sura ya Tano imeelezea matokeo ya utafiti, mapendekezo ya tafiti fuatishi na hitimisho. Utafiti huu umebaini kuwa lugha ya Kikinga ina ngeli za nomino 19 kwa mtazamo wa kimofolojia. Pia, imeonekana kuna mtawanyiko wa nomino za Kikinga katika ngeli tofauti tofauti isipokuwa ngeli inayohusu watu, nomino za mkopo, vitu dhahania, vitu visivyohesabika, zenye dhima ya udogo na mahali zinapoainishwa kimofolojia na kisemantiki. Zaidi ya hayo imebainika kuwa viambishi ngeli vya nomino za Kikinga vinaweza kubeba dhima ya kuonesha umoja, wingi, uzuri, ubaya, udogo na ukubwa.Item Uanishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya Ki-bena.(University of Dar es Salaam, 2011) Mwendamseke, Faraja JaphetUtafiti huu unahusu uainishaji wa ngeli za nomino za lahaja ya Ki-Mwasamu ya lugha ya Ki-bena inayozungumzwa kusini magharibi mwa Tanzania katika wilaya ya njombe mkoani Iringa. Jumla ya watafitiwa 29 kutoka kata ya Imalinyi, lgima na Mdandu ndio waliohusika. uteuzi wao ulikuwa wa kinasibu. Taarifa zimekusanywa kwa watafitiwa kwa njia ya hojaji, mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti huu ulikuwa na malengo yafuatayo: kubainisha ngeli za Ki-Bena na idadi yake, kuchunguza mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki katika ngeli zilizoundwa kwa msingi wa kimofolojia na kufafanua dhima mbalimbali zinazojitokeza katika viambishi ngeli vya nomino. lli kutimiza malengo haya mikabala mitatu ya kinadharia imetumika ambayo ni: mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino, mkabala wa Viambishi vya Upatanisho wa Kisarufi na mkabala wa Kisemantiki. Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino umetumika kubainisha viambishi ngeli vya nomino katika misingi ya umoja na wings. Aidha mkabala wa Viambishi vya Upatanisho wa Kisarutl umetuinika pia kutokana na nomlno zmgine kutokuwa na viambishi dhahiri vya urnojzt na wingi. Katika uchunguzi wetu tumebaini kuna ngeli za Ki-Bona 18. Mkabala wa Kisemantiki umetumika kuchunguza mtawanyiko wa nomino zenye asili moja kisemantiki katika ngeli za msingi wa kimofolojia. Imebainika mtawanyiko wa nomino katika lugha ya Ki-bena upo katika nomino za viungo vya mwili, matunda, na wanyama. Mtawanyiko kama huu haupo katika nomino zinazohusu binadamu. Hivyo inatofautiana sana na lugha kami vile Kiswahili. Pia utafiti huu umebaini katika- lugha ya Ki-Bena, viambishi ngeli vya nomino vina dhima kama vile umoja/wingi, ukubwa/udogo na uzuri/ubaya. Dhima zote hizi huweza kujitokeza katika kiambishi kwa wakati mmoja na kusababisha utata. Pia kuna upekee unaojitokcza katika dhitna ya uzuri na ubaya ambapo dhima ya ubaya hutumika kwa binadamu na viumbe wanaufungwa na binadamu tu, lakini dhima ya uzuri ni kwa wote.Item Ulinganishi wa kiisimu wa lugha ya Samatengo na ya Kindendeule(University of Dar es Salaam, 2013) Kawonga, GervasMadai kwamba lugha ya Samatengo na ya Kindendeule zinafanana yamekuwapo kwa muda mrefu miongoni mwa wanaisimu, wachunguzi na wazungumzaji wa Samatengo na Kindendeule. Utafiti huu ulihusu Ulinganishi wa Kiisimu wa Lugha ya Samatengo na ya Kindendeule. Tatizo la utafiti lilikuwa ni kutafuta data za kiisimu kutoka uwandani ili kuhakiki madai kwamba lugha ya Samatengo na ya Kindendeule zinafanana. Lengo kuu lilikuwa kuonesha ni kwa kiwango gani Samatengo na Kindendeule zinafanana kiisimu ili kufahamu hadhi ya kila moja katika muktadha wa uhususiano wake. Kulikuwa na malengo mahususi matatu. Moja, kuweka vigezo vya kubainisha msingi wa kufanana kwa Samatengo na Kindendeule. Pili, kueleza mwelekeo unaotokana na kufanana kwa vigezo vilivyowekwa. Tatu, kuthibitisha kama hizi ni lugha mbili tofauti au ni lahaja za lugha moja. Data kwa ajili ya utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia tatu ambazo ni maandishi maktabani, hojaji na majadiliano ya vikundilengwa. Mbinu za uchambuzi wa data zilizotumika ni mbinu ya takwimuleksika, mbinu linganishi, na mbinu ya maelezo, ambazo zilikuwa zikikamilishana. Matokeo kwa jumla yamesaidia kujibu maswali ya utafiti na kufikia malengo yaliyowekwa. Lengo la kwanza na swali la kwanza lilihusu vigezo vya kubainisha kufanana kwa Samatengo na Kindendeule. Vigezo viwili vilitumika ambavyo ni msamiati wa msingi na ukubaliano wa sauti. Lengo la pili na swali la pili lilihusu mwelekeo unaotokana na kiwango cha kufanana kwa vigezo vilivyowekwa; imewekwa wazi kwamba mwelekeo ni wa uhusiano wa karibu zaidi kiasi cha kuhitimisha kuwa ni lahaja za lugha moja ya azali. Lengo la tatu na swali la tatu lilihusu kuthibitisha kama hizo ni lugha mbili au ni lahaja za lugha moja. Imethibitishwa kwa vigezo vya kiisimu kuwa Samatengo na Kindendeule ni lahaja za lugha moja. Utafiti unaonesha kwamba Samatengo na Kindendeule zinafanana kwenye kigezo cha msamiati wa msingi kwa 87%. Pia zinafanana katika kigezo cha fonimu za konsonanti kwa asilimia 75% na katika kigezo cha fonimu za irabu kwa 100%. Fasili ya viwango hivyo vya asilimia za kufanana ni kwamba Samatengo na Kindendeule ni lahaja za lugha moja ya azali. Inapendekezwa kwanza, kwa kuwa utafiti huu ulihusu ulinganishi wa Samatengo na Kindendeule, ufanyike utafiti mwingine katika kulinganisha lugha nyingine zinazodaiwa kufanana ili kuweka wazi kiwango cha uhusiano kilichopo baina ya lugha hizo kwa ajili ya kupanua maarifa ya isimu. Pili, inapendekezwa ufanyike utafiti mwingine utakaosaidia kubaini lugha azali kwayo Samatengo na Kindendeule zilitokana nayo. Tatu, utafiti huu ulilinganisha vipengele viwili vya kiisimu yaani msamiati wa msingi na ukubaliano wa sauti. Hivyo ufanyike utafiti mwingine kwa kutumia vigezo vya sintaksia, mofololojia na semantiki ili kubaini kiwango cha kufanana baina ya Samatengo na Kindendeule katika vipengele hivyo. Nne, ufanyike pia utafiti mwingine ili kubaini athari za kihistoria na kiisimujamii katika lahaja za Samatengo na Kindendeule.Item Usawiri wa ontolojia ya kiafrika katika ngano za Kiha.(University of Dar es Salaam, 2018) Raphael, DeogratiasUtafiti huu umejadili vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika vinavyosawiriwa katika ngano za Kiha. Tatizo lililosukuma utafiti huu ni kuwapo kwa makundi mawili yanayojadili Ontolojia ya Kiafrika kwa kujikita katika dini na masuala ya kijamii, kiutamaduni na mahusiano ya kiutawala bila kuhusisha fasihi. Kwa hiyo, utafiti huu ulijikita katika ngano za Waha ili kuona namna zinavyosawiri Ontolojia ya Kiafrika. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza usawiri wa Ontolojia ya Kiafrika katika ngano za Kiha. Malengo mahususi yalikuwa kubainisha vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika katika ngano za kiha na kujadili namna Ontolojia ya Kiafrika inavyosawiriwa katika ngano za Kiha. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika inahusu masuala ya maisha na dhima ya kuwapo kwake. Msisitizo wa nadharia hii ni mahusiano yaliyopo baina ya ulimwengu katika nyuga tatu na walimwengu waliomo katika nyuga hizo. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani na uwandani kuchunguza ngano zilizokusanywa katika vijiji vitano (Janda, Kirungu, Kimara, Kinazi na Munzeze) vya wilaya ya Buhigwe zinavyosawiri Ontolojia ya Kiafrika. Ngano zilikusanywa, kufasiriwa na kuchambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli. Watafitiwa walikuwa ni mchanganyiko wa wanawake na wanaume wa umri tofautitofauti. Wazee wenye ufahamu wa mila na desturi za Waha walihusishwa katika uchambuzi wa ngano zilizohakikiwa. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa ngano zinasawiri Ontolojia ya Kiafrika. Vipengele mbalimbali vya Ontolojia ya Kiafrika vimebainishwa katika utafiti huu. Vipengele hivyo ni pamoja na uduara wa maisha, dhana ya kifo, kuwapo kwa Mungu Mkuu, matambiko, imani katika sihiri na uganga, uzazi, ndoa na malezi, miiko, familia pana, mizimu na mapepo, utoaji wa majina, usababishi/sababu ya matukio na dhana ya wakati. Vipengele vingine ni kuwapo kwa nguvu zilizo nje ya mazingira ya kawaida, kuwapo kwa maisha baada ya kufa, roho kuhamia katika kiumbe kingine, umoja na mshikamano na maadili/tabia njema. Utafiti huu umeonesha kwamba ngano zinaweza kubeba ontolojia ya jamii bila kujiegemeza katika dini au masuala ya kijamii kama vile siasa na uchumi. Msuko wa visa na matukio katika ngano umeweza kudhihirisha uontolojia uliomo katika ngano hizo.