Usawiri wa ontolojia ya kiafrika katika ngano za Kiha.
Loading...
Date
2018
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu umejadili vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika vinavyosawiriwa katika ngano za Kiha. Tatizo lililosukuma utafiti huu ni kuwapo kwa makundi mawili yanayojadili Ontolojia ya Kiafrika kwa kujikita katika dini na masuala ya kijamii, kiutamaduni na mahusiano ya kiutawala bila kuhusisha fasihi. Kwa hiyo, utafiti huu ulijikita katika ngano za Waha ili kuona namna zinavyosawiri Ontolojia ya Kiafrika. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza usawiri wa Ontolojia ya Kiafrika katika ngano za Kiha. Malengo mahususi yalikuwa kubainisha vipengele vya Ontolojia ya Kiafrika katika ngano za kiha na kujadili namna Ontolojia ya Kiafrika inavyosawiriwa katika ngano za Kiha. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika. Nadharia ya Ontolojia ya Kiafrika inahusu masuala ya maisha na dhima ya kuwapo kwake. Msisitizo wa nadharia hii ni mahusiano yaliyopo baina ya ulimwengu katika nyuga tatu na walimwengu waliomo katika nyuga hizo. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani na uwandani kuchunguza ngano zilizokusanywa katika vijiji vitano (Janda, Kirungu, Kimara, Kinazi na Munzeze) vya wilaya ya Buhigwe zinavyosawiri Ontolojia ya Kiafrika. Ngano zilikusanywa, kufasiriwa na kuchambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli. Watafitiwa walikuwa ni mchanganyiko wa wanawake na wanaume wa umri tofautitofauti. Wazee wenye ufahamu wa mila na desturi za Waha walihusishwa katika uchambuzi wa ngano zilizohakikiwa. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tumefikia mahitimisho kuwa ngano zinasawiri Ontolojia ya Kiafrika. Vipengele mbalimbali vya Ontolojia ya Kiafrika vimebainishwa katika utafiti huu. Vipengele hivyo ni pamoja na uduara wa maisha, dhana ya kifo, kuwapo kwa Mungu Mkuu, matambiko, imani katika sihiri na uganga, uzazi, ndoa na malezi, miiko, familia pana, mizimu na mapepo, utoaji wa majina, usababishi/sababu ya matukio na dhana ya wakati. Vipengele vingine ni kuwapo kwa nguvu zilizo nje ya mazingira ya kawaida, kuwapo kwa maisha baada ya kufa, roho kuhamia katika kiumbe kingine, umoja na mshikamano na maadili/tabia njema. Utafiti huu umeonesha kwamba ngano zinaweza kubeba ontolojia ya jamii bila kujiegemeza katika dini au masuala ya kijamii kama vile siasa na uchumi. Msuko wa visa na matukio katika ngano umeweza kudhihirisha uontolojia uliomo katika ngano hizo.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8025.T34R36)
Keywords
Bantu languages, Swahili literature, Ngano za kiha
Citation
Raphael, D. (2018). Usawiri wa ontolojia ya kiafrika katika ngano za Kiha. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.