Dhima ya mhusika bibi katika ngano za kifipa

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulihusu Dhima ya mhusika Bibi katika ngano za Kifipa. Malengo mahususi ya utafiti huu ni; kubainisha sifa za mhusika Bibi katika ngano za Kifipa, kueleza dhima za kifani na kimaudhui za mhusika Bibi katika ngano za Kifipa na kuchunguza uhusiano wa usawiri wa mhusika Bibi katika ngano za Kifipa na masuala mbalimbali ya kijamii. Vifaa vilivyotumika katika utafiti huu ni pamoja na kalamu na daftari, kamera ya picha tuli, kompyuta pakatwa, kinyonyi na simu ya mkononi. Mbinu zilizotumika ni; mbinu ya maktabani, mbinu ya uwandani, ushiriki/ushuhudiaji, majadiliano na mahojiano. Pia, data zilipatikana kwa kutumia maswali ya mwongozo wa majadiliano na mahojiano. Data zilichakatwa na kuchambuliwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Uhasilia na Nadharia ya Semiotiki. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa mhusika Bibi katika ngano za Kifipa anasawiriwa kwa mtazamo chanya kutokana na umuhimu wake na sifa zake katika kujenga msingi na imani ya jamii ya Wafipa. Vilevile, tumebaini kuwa pamoja na kuwa Bibi ni mhusika binadamu kinyume cha kazi za fasihi andishi, Bibi hufuata kaida za kingano katika kuwasilisha mambo mbalimbali katika jamii. Katika mtiririko wa ngano hizi za Kifipa, Bibi amesawiriwa katika hali chanya tu akiwa mstari wa mbele katika kutetea mambo mbalimbali katika jamii kama vile upendo wa dhati, utii, uvumulivu, kupinga unyanyasaji katika jamii na mwongozaji wa mbinu mbalimbali za kukabiliana na mambo yanayokwamisha maendeleo ya jamii. Mwisho, utafiti huu umetoa mapendekezo ya maeneo yanayohitajika kufanyiwa utafiti zaidi ili kuinua wigo wa wahusika katika utanzu wa ngano na fasihi simulizi kwa ujumla.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF RA777.3.U33W34)
Keywords
Bantu languages, Fipa language, Literature
Citation
Waivyala, M. (2016) Dhima ya mhusika bibi katika ngano za kifipa, Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam