Dhamira za nyimbo za harusi za wakerewe na mabadiliko ya jamii
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasinifu hii ni matokeo ya utafiti kuhusu Dhamira za Nyimbo za Harusi za Wakerewe na Mabadiliko ya Jamii. Utafiti ulikusudia kuchunguza mabadiliko ya jamii ya Wakerewe jinsi yanavyoakisiwa na dhamira za nyimbo za harusi za Wakerewe. Nyimbo kumi zilizoimbwa kuanzia miaka ya 1970 hadi mwaka 2010 ndizo zilizochungunzwa katika utafiti huu. Nyimbo hizo zimekusanywa kutoka vijiji vya Bukindo na Buzegwe katika wilaya ya Ukerewe.Nyimbo za harusi kumi zilizokusanywa zilichambuliwa ili kuweza kubainisha mabadiliko ya jamii yanavyoakisiwa na dhamira katika jamii ya Wakerewe. Aidha, nadharia ya Sosholojia ilitumika katika uchambuzi wa data. Njia za ushuhudiaji na mahojiano zilisaidia kupata data katika kutimiza lengo la kuchunguza dhamira na mabadiliko ya jamii. Utafiti wetu ulibaini kuwa nyimbo za harusi za Wakerewe huakisi mabadiliko yanayojitokeza katika jamii. Mabadiliko yaliyoakisiwa katika dhamira nyimbo hizo ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuingia kwa ugonjwa wa UKIMWI na kuibuka kwa imani za ushirikina kuhusu maalbino.Mapendekezo ya utafiti huu yalitolewa kwa watafitiwa kufanya tafiti nyingi zaidi katika fani na maudhui kwenye nyimbo za harusi za jamii mbalimbali nchini