PhD Theses
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing PhD Theses by Subject "Bantu languages"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Nafasi ya lugha ya kiswahili katika mandhari- lugha ya jiji la Mbeya nchini Tanzania(University of Dar es salaam, 2020) Kawonga, GervasUtafiti huu ulihusu nafasi ya lugha ya Kiswahili katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Lengo kuu lilikuwa kuchunguza nafasi ya lugha ya Kiswahili katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Malengo mahususi yalikuwa matatu: kwanza, kubainisha ruwaza za lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Pili, kudhihirisha nafasi ya lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia ruwaza za lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Tatu, kuwianisha sera ya lugha ya Tanzania na nafasi ya lugha kwenye mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu yenye msingi kwamba katika jamii kuna vipengele vya kimfumo na kiitikadi vinavyosababisha uhusiano usio wa usawa miongoni mwa lugha za jamii mbalimbali. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya upigaji wa picha za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu na mbinu ya usaili. Uchambuzi wa data za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu ulifanyika kwa mbinu ya usomaji wa matini na Programu Tarakilishi ya Takwimu (PTT). Uwasilishaji wa data umefanyika kwa kutumia vielelezo vya majedwali, grafu na picha kwa data za kiidadi za mabango ya makampuni ya mawasiliano ya simu. Nukuu za usaili na ufafanuzi wa kinathari umetumika kwa data za kitaamuli. Matokeo yanaonesha kwamba kuna ruwaza nne za lugha katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Ruwaza zilizobainishwa ni Kiswahili pekee, Kiingereza pekee, Kiswahili-Kiingereza na Kiingereza-Kiswahili. Kiswahili kinajitokeza kwa asilimia 54.5 katika ruwaza ya Kiswahili pekee mbele ya Kiingereza. Kwa kigezo cha ukubwa wa maandishi Kiswahili kinajitokeza cha kwanza kwa asilimia 63 kwa maandishi makubwa zaidi kuliko Kiingereza. Vilevile, kwa kigezo cha idadi ya maneno Kiswahili kinajitokeza katika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 72.23. Kwa hiyo, Kiswahili kinajitokeza katika nafasi ya kwanza kimatumizi katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya nchini Tanzania. Aidha, kuna uwiano baina ya Sera ya Lugha ya Tanzania na nafasi ya matumizi ya lugha katika mandhari-lugha ya Jiji la Mbeya. Hata hivyo, tunapendekeza serikali ifanye mapitio ya sera ya lugha ili kuunda kanuni za matumizi ya lugha katika mandhari-lugha na kuweka urari wa matumizi ya lugha katika mandhari-lugha. Vilevile, tafiti fuatishi zifanyike kwa kuchunguza mabango ya makampuni mahususi tofautitofauti ili kupanua uelewa kuhusu ruwaza za lugha, nafasi ya Kiswahili na uwiano wa nafasi ya matumizi ya lugha na Sera ya lugha ya Tanzania.Item Ukanushi katika vitenzi vva lugha ya kibena: Msingi wa kimofosintaksia(University of Dar es Salaam,, 2012) Mbunda, Irene EdwardUtafiti huu unaliusu utokeuji wa mofimu za ukunnslii kalika vitenzi vya lugha ya Kibena. Data iliyojadiliwa katika utafiti huu imekusanywa kutoka kalika vjjjjj vitatu ambavyo ni Mlwango, llunda na Kichiwa, Vijiji hivi vipo kalika wilaya ya Njombe, mkoani Njoinbe. Data msingi na data fuatizi /imetumika katika utafiti huu. Data msingi ilikusanywa uwandani, wakati data fuati/i ilikusanywa kutoka maktabani. Utafiti huu umegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeonesha suala lililochunguzwa katika utafiti huu pamoja na mipaka yake. Sura ya pili imeonesha msingi wa nadharia ya Umbo Upeo iliyoasisiwa na Prince na Smolensky (1993), Nadharia hii imetumika kama mwongozo wa uchambuzi wa data iliyokusanywa. Vilevile machapisho mbalimbali yanayoelezea juu ya mofimu za ukanushi katika vitenzi vya lugha mbalimbali za Kibantu yameoneshwa katika sura ya pili. Sura ya tatu inaonesha mbinu zilizotumiwa na mtafiti katika kukusanya data ya utafiti ambayo imechambuliwa na kufafanuliwa katika utafiti huu. Mbinu ya ushuhudiaji, hojaji na usaili zimeelezewa kuwa zimetumika katika kukusanya data uwandani. Mbinu ya kusoma na kunukuu imetumika kukusanya data maktabani. Sura ya nne imeonesha uchambuzi wa data ulivyofanyika katika utafiti huu kwa kuzingatia masharti zuizi yanayozuia mofimu za ukanushi kujitokeza katika ruwaza zisizo kubalifu katika lugha ya Kibena. Uzingatiaji wa masharti zuizi hayo unatokana na mwongozo wa nadharia ya Umbo Upeo iliyo na madai ya msingi kuwa maumbo mbalimbali ya lugha hutokana na masharti zuizi yaliyopo. Hivyo mofimu za ukanushi zimebainishwa kujitokeza kulingana na masharti zuizi ya utokeaji wa mofimu hizo katika lugha ya Kibena. Sura ya tano imeonesha matokeo ya utafiti pamoja na mapendekezo ya tafiti fuatishi. Data ya utafiti imebaini kuwepo kwa mofimu nne za ukanushi katika lugha ya Kibena. Mofimu hizo zimeoneshwa kuwa hujitokeza mwanzoni mwa vitenzi vinavyokanushwa. Vilevile data ya utafiti imebaini kuwa lugha ya Kibena haina tabia ya kupachika mofimu za ukanushi zaidi ya moja katika kitenzi kimoja.Item Ulinganishi wa Kiisimu wa “Lugha” za kibantu za Mara Kaskazini(University of Dar es Salaam, 2019) Boniphase, Alphonce MorangoUtafiti huu unahusu "Ulinganishi wa Kiisimu wa "Lugha" za Mara Kaskazini" ili kubaini karna ni lugha zinazojitegemea au ni lahaja tu za lugha moja kuu ya awali. ''Lugha" za Mara Kaskazini zilizolinganishwa ni Kikurya, Kisimbiti, Kikiroobha, Kisweeta, Kikabwa, Kisuba, Kikine na Kikenye. Utafiti huu una malengo mahsusi mawili: kubainisha mfanano na tofauti ya vi gezo vya kiisimu ambavyo ni msamiati wa msingi , mfu mo wa sauti, mfurno wa ngeli , mfumo wa njeo na mfumo wa ukanushi . Lengo la pili ni kuanisha kiwango cha uhusiano kilichopo kinachoweza kubainisha karna ''lu gha" za Mara Kaskazini ni lugha au lahaja. Utafiti urneongozwa na nadharia kuu mbili ambazo ni Nadharia ya Mwachano na Makutano ya Lugha za Kibantu pamoja na nadhariatete ya Ndugu na Nd ugu wa Mbali i liyoasisi wa na M assamba mwaka 2007. Nadharia ya pili ni Isimu Historia-Linganishi i liyoasisi wa na Jones rnwaka 1786. Utafiti huu unategemewa kuwa na umuhi mu kwa wanaisi rnu na wanajami i wal iokuwa wanatatizika kuhusu "lugha" hizi na wale wote wenye kiu ya kutaka kujua namna ya kulinganisha lugha mbalimbali kiisirnu. Aidha, data zautafiti huu zilipatikana uwandani kwa kuhusisha mbinu mbal imbali za utafiti arn bazo nikusikiliza, usaili , hojaji na majad iliano katika majopo. Eneo la utafiti lilihusisha vijiji 14 kutoka katika Wilaya za Tarime, Rorya, Butiama, Musoma Mjini na Musoma Vijijini. Matokeo ya utafiti huu yamedhihi risha kuwa "lugha" zilizolinganishwa si lugha zinazojitegemea, bali ni lahaja zilizotokana na lugha moja ya awali . "Lugha" hizi zimeonesha mfanano wa zaidi ya asilimia sabini (70%). Mfanano huo umezigawa "lugha" hizi katika makundi mawili: kundi la "lugha" za Kikurya, Kisimbiti, Kisweeta, Kikine na Kikenye na kundi la "lugha" za Ki kabwa, Kisuba l na Kikiroobha.Tunapendekeza tafiti zaidi zifanywe katika vipengele kadhaa vya ki isimu ambavyo havikushughulikiwa katika utafiti huu. V ipengel e hivyo, ni kama vile kipengele cha toni. Kipengele hiki kimeonekana kuwa changamani katika "lugha" za Mara Kaskazini, kimeonesha kutofautisha njeo, hivyo kina athari katika matamshi. Suala lingine ni kukosekana kwa "lugha" ya Kishashi, mojawapo ya "lugha" zilizopangwa kuchunguzwa katika utafiti huu lakini haikuwepo kat ika mazingira hal isi kule uwandani na wala wazungumzaji wake, japokuwa eneo la Ushashi lipo.