PhD Theses
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing PhD Theses by Author "Buberwa, Adventina"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mofolojia ya majina ya mahali ya kiswahili na kihaya katika jamii ya wahaya: uzingativu wa masuala ya kiisimujamii(University of Dar es Salaam, 2016) Buberwa, AdventinaBaadhi ya wanaisimu huyatazama majina ya mahali kama maneno yasiyoweza kuchanganuliwa kimofolojia ilhali wengine wakiyatazama kama maneno yaliyojengwa kwa vipashio maalum. Madai haya kinzani ndiyo yaliyoongoza raghba ya mtafiti kufanya utafiti huu unaochunguza mofolojia ya majina ya mahali ya Kiswahili na Kihaya kwa kuzingatia masuala ya kiisimujamii yanayofafanua maumbo hayo. Kwa kutumia mbinu za utafiti zilizoteuliwa, yaani usaili, mijadala katika makundi lengwa na ushuhudiaji, data ya utafiti huu ilikusanywa kutoka katika wilaya za Muleba, Misenyi, Bukoba vijijini na Bukoba Mjini, mkoani Kagera. Vifaa vya kukusanyia data vilivyotumika ni pamoja na kalamu na daftari, kinasasauti, kompyuta pakatwa na kamera. Uchanganuzi wa data kimofolojia umeongozwa na nadharia ya Mofolojia Leksika. Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa kutumia majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika. Uchanganuzi wa vipengele vya kiisimujamii umefanywa kwa kuongozwa na mkabala wa Uchanganuzi Tunduizi Kilongo. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa majina ya mahali yaliyochunguzwa yameundwa ama kwa neno moja pekee au kwa maneno ambatani, yaani neno zaidi ya moja. Utafiti huu umethibitisha kuwa vipo vipashio maalum vinavyounda majina ya mahali na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia. Licha ya majina ya mahali kutokana na masuala mbalimbali ya kiisimujamii, majina hayo hayateuliwi kama yalivyo kama wanaisimu waliotangulia walivyodhani. Mbinu za uundaji wa maneno huhusika katika uundaji wa majina ya mahali. Utafiti huu unapendekeza kuwa utafiti kama huu unaweza kufanywa katika maeneo mengine. Aidha, inapendekezwa kuwa majina ya mahali yanaweza kuchunguzwa kimofolojia, kisemantiki, kiisimujamii au kisintaksia.