Nafasi ya dhana ya moyo katika kuibua dhamira na hisia za kishairi: uchunguzi wa ushairi wa andenenga
Loading...
Date
2015
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu “ Nafasi ya Dhana ya Moyo Kiatika Kuibua Dhamira na Hisia za Kishairi: Uchunguzi wa Ushairi wa Andenenga. Utafiti ulihusisha mashairi kutoka katika Diwani ya Ustadh Andanenga na Bharii ya Elimu ya Ushairi. Lengo kuu l utafiti huu lilikua ni kuchunguza namna matumizi ya dhana ya moyo katika ushairi wa Andanenga yalivyo chochea uteuzi wa mbinu za kimtindo pamoja na uteuzi wa dhamira na hisia za kishairi. Maandiko na mchapisho mbalimbali yahusianayo na mada ya utafiti yamepitwa kwa kina kwa kuongoza na nadharia za Mwigo, Uhusivu n Mwingiliano Matini. Utafiti umetumia mbinu ya uchambuzi matini katika kukusanya data za msingi na data za ufatizi kutoka maandiko mbalimbali. Uchambuzi wa utafiti huu umefanywa kwa kuongoza na mbinu ya uchambuzi wa kimaelezo, uchambuzi matini na uchambuzi wa kifasihi ulioongoza na nadharia za Mwigo, Uhusivu na Mwingiliano Matini. Matokeo ya utafiti yanaonesha kua Andanenga amefanikiwa kutumia dhana ya moyo kwa kuikamilisha ushikamani wake kifani na kimaudhui. Tumelioma hili kupitia mbinu za kimtindo zilizotumika sanjari na dhana ya moyo pia katika dhamira na hisia tulizozichambua zilizonasibishwa na dhana ya moyo. Mwisho, tumetoa hitimisho kuu la utafiti na kuaiisha nyanja mbalimbali za kiutafiti zinazoweza kuibuliwa katika mashairi teule na ushairi wa Kiswahili kwa
ujumla
Description
Available in print form, Eat Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library,(THS EAF PL8704.G38)
Keywords
Swahili poetry, Swahili language
Citation
Gawaza, M. I.(2015) Nafasi ya dhana ya moyo katika kuibua dhamira na hisia za kishairi: uchunguzi wa ushairi wa andenenga. tasnifu ya MA(kiswahili). Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dar es Salaam.