PhD Theses
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing PhD Theses by Subject "A case of Dar es Salaam and Kigoma region"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Practices of teachers‟ participation in secondary school governance in Tanzania: a case of Dar es salaam and Kigoma regions(University of Dar es Salaam, 2018) Lulamye, Steward NgagardUtafiti huu ulijikita juu ya ushiriki wa walimu katika utawala wa shule kivitendo nchini Tanzania. Kwa ujumla utafiti umeangazia michakato na mikakati inayotumika katika kukuza ushiriki huo kwa kulinganisha kati ya shule za mijini na vijijini katika mikoa ya Dar es Salaam na Kigoma. Mahsusi zaidi utafiti ulijikita katika mambo manne ambayo ni uelewa na maarifa ya walimu juu ya mikakati na michakato ambayo inatumika kukuza ushiriki katika utawala wa shule kama ilivyobainishwa katika Sera za Elimu na za shule; mienendo na mitazamo ya walimu wa shule za sekondari katika ushiriki wa utawala wa shule; mikakati na michakato mbalimbali inavyotumika katika kukuza ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule kwa mwalimu mmojammoja, kama kikundi cha walimu na mwalimu katika ngazi ya shule na pia utafiti uliangazia changamoto chanya zinazoathiri ushiriki dhabiti wa walimu katika utawala wa shule. Katika utafiti huu mpango wa uchunguzi na uchambuzi ulitumika katika kuchunguza mambo mbalimbali. Utafiti huu umetumia njia zisizo za kimahesabu na zile za kimahesabu. Katika kupata sampuli za utafiti zilitumika njia zifuatazo, njia rahisi ya kubahatisha (simple random), njia tabaka (stratified sampling) na sampuli makusudi (purposive sumpling) ambazo zilitumika kuwapata washiriki 281 wa utafiti ambao walikuwa ni walimu, watawala wa shule, wanafunzi, wazazi, wajumbe wa bodi za shule, wahadhili toka Shule kuu ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSE), Taasisi zisizo za serikali ambazo ni Haki Elimu na Twaweza Pamoja na Maofisa wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoka kitengo cha mipango na sera. Taarifa za utafiti zilikusanywa kwa kutumia maswali ya hojaji( questionnaires ), maswali elekezi ya usaili,(interview guide questions) kundi mahsusi la mjadala (Focus group discussions), uchunguzi wa asili (naturalistic observations) na njia zingine za kusoma majarida kupata taarifa kama vile vitabu, sera, machapisho na vipepelushi mbalimbali.Kwa ujumla, utafiti ulibainisha kuwa washiriki wengi katika maeneo yote mawili ya utafiti wameweza kuchambua mikakati na michakato inayo tumia katika kukuza ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Mahususi, zaidi matokeo ya utafiti yameonesha kuwa walimu wengi walikuwa na uelewa na maarifa ya kutosha juu ya mikakati na michakato inayotumika katika kukuza ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Kuweka malengo na madhumuni pamoja na kuandaa mipango ya mafanikio ya kitaaluma ilikuwa ni mikakati mikuu iliyobainishwa, wakati kipimo cha uwajibikaji wa walimu, uimarishaji wa kuwajibika na mamlaka waliyonayo ilikuwa ni Michakato mikuu iliyobainishwa katika mkoa wa Dar es salaam na Kigoma ambapo utafiti ulifanyika. Matokeo yalibainisha zaidi kuwa kulikuwa na mwenendo na mtazamo chanya wa walimu juu ya ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Kadhalika, matokeo yameonesha kuwa washiriki wengi wa utafiti huu katika maeneo yote mawili ya utafiti wamebainisha na kupembua mikakati, michakato na shughuli kama kufundisha na kujifunzia ambayo inatumika kuimarisha ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Vilevile, changamoto za mwalimu mmoja mmoja pamoja na za Utawala wa shule ilibainishwa kuwa ni changamoto kuu zinazokabili ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Pia unyumbulifu wa Maendeleo ya kitaalama ya walimu, Kamati maalum za shule, na Utawala wa shule unaokubali mabadiliko ni mikakati iliyo pendekezwa kukuza ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Hivyo basi utafiti huu unachangia taaluma mpya katika Nyanja ya Utawala wa shule hasa katika michakato, mikakati na changamoto za ushiriki wa walimu katika utawala wa shule kwa mwalimu mmoja mmoja, kama kundi la walimu, na walimu katika ngazi ya shule.Kwa hiyo hitimisho la jumla ni kwamba, washiriki wa utafiti walio wengi walichambua mikakati na michakato ya ushiriki wa walimu katika Utawala wa shule. Utafiti unapendekeza kuwa, kila mdau anapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo, ili kurahisisha uendeshaji mzuri wa shule za sekondari. Kwa mfano wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapaswa kubuni njia nzuri ya kusambaza kwa wadau sera ya elimu na pia kutoa mafunzo yahusuyo sera hiyo katika shule. Mwisho utafiti ulipendekeza maeneo mengine ya kufanyia utafiti juu ya ushiriki wa walimu katika utawala wa shule katika mikoa mingine, utafiti juu ya sera mpya ya elimu na vile vile kufanya utafiti kuangalia ni jinsi gani ushiriki wa walimu katika utawala wa shule unaweza kuhamasisha wanafunzi kuwa na utayali wa kusoma kwa bidii na hatimaye kuongeza ubora wa elimu nchini Tanzania.