Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Subject "bantu"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item LAHAJA ZA KIHEHE Mtazamo wa kiisimu(University of Dar es Salaam, 2013) Haonga, Ernest daimonUtafiti huu ulilenga kubainisha na kueleza lahaja za Kihehe kwa mtazamo wa kiisimu, Tatizo lililosababisha utafiti huu ni kuwa watafiti mbalimbali wamedokeza tu kuhusu lahaja za Kihehe lakini hawajafanya utafiti wa kina kuhusu suala hilo. Wengi wamezielezea lahaja za Kihehe kutokana na kuwa wamilisi tu wa lugha hiyo. Aidha, watafiti waliotangulia hawakubaliani juu ya lahaja hizo na hivyo tukaona kuna haja ya kufanya utafiti wa kina ili kuzibainisha na kuzieleza. Data zilizotumika katika utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia utafiti wa maktabani na uwandani. Uwandani zilitumika mbinu kama vile majadiliano katika vikundi, hojaji na usaili zilizosaidia kupata data simulizi na andishi. Ukusanyaji, uchambuzi na ufasiri wa data uliongozwa na nadharia ya Mwachano na Makutano wa Kibantu ya Massamba (2007). Data zilichambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo na sio wa kiidadi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kuna lahaja kuu mbili za Kihehe ambazo zinaainishwa kulingana na mahali zinapozungumzwa. Lahaja hizo ni lahaja ya milimani na lahaja ya mabondeni. Lahaja hizo, mbali na kufanana katika vipengele kadhaa vya kiisimu, bado zina tofauti. Tofauti zinajibainisha katika sauti zinazotumiwa, maumbo ya maneno, jinsi sentensi zinavyoundwa na maana za maneno. Ingawa utafiti huu umeshughulikia kwa kina lahaja za Kihehe, tunaona bado kuna haja ya kufanya utafiti mwingine utakaohusisha mitazamo mingine nje ya mitazamo ya kiisimu ili kupata mahitimisho jumuishi. Pia, kwa kuwa Kihehe kilichochunguzwa humu ni cha mkoa wa Iringa tu, kuna haja ya kufanya utafiti utakaojumuisha wasemaji wa lugha hii katika mikoa mingine kama vile Njombe na Mbeya. Aidha, utafiti huu haukushughulikia vipengele vya kiisimu kwa mapana yanayostahili, hivyo kuna haja ya kufanya utafiti mwingine utakaotimiza hilo.Item Uainishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya ki-vunjo(University of Dar es Salaam, 2013) Ndekiro, RuthUtafiti huu ulilenga kuainisha ngeli za nomino za lugha ya ki-Vunjo kwa mkabala wa viambishi awali vya nomino, kufafanua muainisho mdogo wa nomino kwa uzingatizi wa kisemantiki na kueleza dhima za viambishi ngeli vya nomino. Utafiti huu umefanyika katika kata ya Mwika, vijiji vya Maring‟a, Uuwo na Kirimeni, wilaya ya Moshi Vijijini mkoa wa Kilimanjaro, nchini Tanzania. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mofolojia Asili (NMA) ili kufanikisha malengo yake. Kazi imegawanyika katika sura nne. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti pamoja na mapitio ya maandiko na mbinu zilizotumika katika utafiti huu. Sura ya pili, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data iliyokusanywa uwandani. Katika uchanganuzi huo ngeli za nomino zimeainishwa kwa kigezo cha kimofolojia kwa kuzingatia mkabala wa viambishi awali vya nomino. Katika sura ya tatu kigezo cha kisemantiki kimetumika ili kufafanua muainisho mdogo wa Ngeli za nomino katika lugha ya ki-Vunjo. Sura ya nne, imeshughulikia matokeo, hitimisho na mapendekezo ya utafiti ambao unaweza kufanywa baadae. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa lugha ya ki-Vunjo ina ngeli za nomino 18. Pia utafiti huu umebainisha kuwa nomino za ki-Vunjo zenye sifa za kisemantiki zinazofanana zimetawanyika katika ngeli tofauti. Vilevile utafiti huu umebainisha kuwa viambishi ngeli vya nomino za ki-Vunjo vina dhima zaidi ya umoja, wingi, ukubwa na udogo. Dhima hizo ni ubaya, uzuri, udhaifu, urefu, wembamba, ufupi, tabia mbaya na tabia nzuri.