Uainishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya ki-vunjo

No Thumbnail Available
Date
2013
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuainisha ngeli za nomino za lugha ya ki-Vunjo kwa mkabala wa viambishi awali vya nomino, kufafanua muainisho mdogo wa nomino kwa uzingatizi wa kisemantiki na kueleza dhima za viambishi ngeli vya nomino. Utafiti huu umefanyika katika kata ya Mwika, vijiji vya Maring‟a, Uuwo na Kirimeni, wilaya ya Moshi Vijijini mkoa wa Kilimanjaro, nchini Tanzania. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mofolojia Asili (NMA) ili kufanikisha malengo yake. Kazi imegawanyika katika sura nne. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti pamoja na mapitio ya maandiko na mbinu zilizotumika katika utafiti huu. Sura ya pili, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data iliyokusanywa uwandani. Katika uchanganuzi huo ngeli za nomino zimeainishwa kwa kigezo cha kimofolojia kwa kuzingatia mkabala wa viambishi awali vya nomino. Katika sura ya tatu kigezo cha kisemantiki kimetumika ili kufafanua muainisho mdogo wa Ngeli za nomino katika lugha ya ki-Vunjo. Sura ya nne, imeshughulikia matokeo, hitimisho na mapendekezo ya utafiti ambao unaweza kufanywa baadae. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa lugha ya ki-Vunjo ina ngeli za nomino 18. Pia utafiti huu umebainisha kuwa nomino za ki-Vunjo zenye sifa za kisemantiki zinazofanana zimetawanyika katika ngeli tofauti. Vilevile utafiti huu umebainisha kuwa viambishi ngeli vya nomino za ki-Vunjo vina dhima zaidi ya umoja, wingi, ukubwa na udogo. Dhima hizo ni ubaya, uzuri, udhaifu, urefu, wembamba, ufupi, tabia mbaya na tabia nzuri.
Description
Available in print copy
Keywords
bantu, lugha, nomino, kivunjo
Citation
Ndekiro, R.(2013). Uainishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya ki-vunjo. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/search.aspx?formtype=advanced)