PhD Theses
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing PhD Theses by Author "Mosha, Doroth Felician"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Majukumu ya wahusika kijinsia katika nyimbo za watoto za Kiswahili na uhalisia wake katika malezi ya watoto nchini Tanzania(Chuo kikuu cha Dar es Salaam, 2019) Mosha, Doroth FelicianTasnifu hii ni matokeo ya mada ya utafiti ‘’ Majukumu’’ ya wahusika kijinsia katika nyimbo za watoto za Kiswahili na Uhalisia wake katika Malezi ya watoto nchini Tanzania’’ Tum’echunguza namna watunzi wa nyimbo za watoto walivyowateua wahusika kuwapa majukumu anuwai kwa mujibu wa jinsi zao. Vilevile, tumechambua maoni ya wanajamii (walimu, wanafunzi na wataalamu wa masuala ya jinsia) kuona namna wanavyogawanya majukumu kwa watoto wanapowatia malezi. Lengo ni kufanya ulinganishi ili kuona endapo kuna uhalisia wa majukumu ya kijimsia katika nyimbo za watoto na malezi ya watoto nchini Tanzania. Utafiti uliongozwa na malengo muhususi manne: Mosi, kubainisha wahusika waliojitokeza katika nyimbo za watoto kwa mujibu wa jinsi zao. Pili, kuchambua majukumu ya wahusika hao. Tatu, kujadili moni ya jamii kuhusu majukumu ya kijinsia katika malezi ya watoto na kulinganisha na yale ya nyimbo za watoto kwa watoto na jamii. Data zilizokusanywa kwa njia ya mahojiano, ushuhudiaji na maandiko mbalimbali ziifanikisha malengo tajwa. Data hizi zimewasilishwa na kuchambuliwa kwa njia ya kitaamuli kukiwa pia na matumizi ya uchambuzi wa kitakwimu na majedwali. Utafiti umeongozwa na nadharia za Skima ya kijinsia na uhalisia. Skima ya kijinsia ni nadharia ya mrengo wa jinsia inayoangazia namna mtoto anavyojifunza majukumu yanayomhusu kwa kuhushudia yale yanayofanywa na wanaume na wanawake wakiongozwa na utamaduni wa jamii husika. Nadharia ya uhalisia imezingatia ukweli na uyakinifu wa majukumu ya kijisnisia katika malezi ya watoto kama yalivyosawiriwa katika nyimbo za watoto ili kubaini kufanana na kutofautiana kwake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa: Mosi, wahusika wa kike ni wengi kuliko wahusika wa kiume na wamebebeshwa majukumu mengi. Pili, watunzi wa nyimbo za watoto wamesawiri mgawanyo sawia wa majukumu ya kijinsia ya wahusika. Tatu, maoni ya wanajamii yamebaini kutokuwa na unyoofu wa mgawanyo wa majukumu ya kijinsia katika malezi ya watoto. Hali hii huchangiwa na tofauti za kiutamduni na malezi ya kifamilia, mitazamo na itikadi tofauti, dini, elimu, tofauti za kihistoria na hatua ya maendeleo ilivyofikiwa katika familia au jamii husika. Hivyo, hakuna usahili wa kiuhalisia baina ya majukumu ya wahusika kijinsia katika za watoto na majukumu ya wahusika kijisinsia katika nyimbo za watoto umebainika kuwa na athari chanya na hasi kwa watoto na jamii.