Masters Dissertations
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Masters Dissertations by Author "Ambrose, Daniel"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Sintaksia ya maswali kaika lugha ya Kiswahili(University of Dar es Salaam, 2016) Ambrose, DanielUtafiti huu ulilenga kuchunguza Sintaksia ya maswali katika lugha ya Miongoni mwa mambo ambayo mtafiti aliyatafiti ni viashiria vya maswali, aina ya maswali. muundo wa maswali na matumizi mengine ya maswali katika lugha ya Kiswahili. Data ilikusanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi na Mtaa wa pasua nchini Tanzania. Data ilikusanywa kwa njia ya hojaji, mahojiano na mijadala katika vikundi lengwa. Data ilichambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya Kiunzi Rasmi cha Sarufi Geuzamaumbo Zalishi iliyoasisiwa na mwanaisimu mashuhuri NoamChomsky. Utafiti huu umegundua kuwa viulizi vinaweza kugawanywa kwa namna kuu mbili, kimuundo na kidhima. Pia utafiti huu ulibaini kuwa muundo wa sentensi ulizi hauhusishi uhamaji wa viambajengo. Pamoja na hayo utafiti huu umegundua kuwa kwa kutumia kigezo cha kidhima sentensi ulizi katika lugha ya Kiswahili zinaweza kugawanywa katika sehemu kuu nne. Zaidi ya yote, tofauti na yalivyo matarajio ya watu wengi, maswali zaidi ya kuhoji juu ya jambo fulani, huweza kuwa na matumizi mengine kama vile kukejeli, kutoa majibu, kupima ufahamu, na kudokeza hisia za mzungumzaji kama vile hasira na huzuni. Mwisho, baada ya kuwasilishwa na kuchambuliwa matokeo ya utafiti, mapendekezo yametolewa juu ya nini kifanyike zaidi kutokana na matokeo hayo