Sintaksia ya maswali kaika lugha ya Kiswahili

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu ulilenga kuchunguza Sintaksia ya maswali katika lugha ya Miongoni mwa mambo ambayo mtafiti aliyatafiti ni viashiria vya maswali, aina ya maswali. muundo wa maswali na matumizi mengine ya maswali katika lugha ya Kiswahili. Data ilikusanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi na Mtaa wa pasua nchini Tanzania. Data ilikusanywa kwa njia ya hojaji, mahojiano na mijadala katika vikundi lengwa. Data ilichambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya Kiunzi Rasmi cha Sarufi Geuzamaumbo Zalishi iliyoasisiwa na mwanaisimu mashuhuri NoamChomsky. Utafiti huu umegundua kuwa viulizi vinaweza kugawanywa kwa namna kuu mbili, kimuundo na kidhima. Pia utafiti huu ulibaini kuwa muundo wa sentensi ulizi hauhusishi uhamaji wa viambajengo. Pamoja na hayo utafiti huu umegundua kuwa kwa kutumia kigezo cha kidhima sentensi ulizi katika lugha ya Kiswahili zinaweza kugawanywa katika sehemu kuu nne. Zaidi ya yote, tofauti na yalivyo matarajio ya watu wengi, maswali zaidi ya kuhoji juu ya jambo fulani, huweza kuwa na matumizi mengine kama vile kukejeli, kutoa majibu, kupima ufahamu, na kudokeza hisia za mzungumzaji kama vile hasira na huzuni. Mwisho, baada ya kuwasilishwa na kuchambuliwa matokeo ya utafiti, mapendekezo yametolewa juu ya nini kifanyike zaidi kutokana na matokeo hayo

Description

Available in print form, EAF collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark ( THS EAF PL8702.A52 )

Keywords

Swahili language, Syntax

Citation

Ambrose, D ( 2016 ) Sintaksia ya maswali kaika lugha ya Kiswahili , Masters dissertation, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.