Usawiri wa wahusika wanawake katika ngano za kinyiramba
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza usawiri wa wa ngano za husika wanawake katika Kinyiramba. Lengo hili limeweza kufanikiwa kutokana na kukamilika kwa malengo mahususi yaliyohusu kuchunguza dhamira mbalimbali za usawiri wa rnwanamke katika ngano, kubainisha na kuchambua usawiri wa wahusika wanawake katika ngano hizo. Maandiko na machapisho mbalimbali juu ya ngano na nafasi ya mwanamke yamepitiwa kwa kutumia nadharia. Uhalisa. Utafiti umetumia mbinu ya uchambuzi matinikatika kukusanya data za msingi za utafiti pamoja na data za upili kutoka maandiko mbalimbali. Uchambuzi wa data umeongozwa na mbinu ya uchambuzi wa kifasihi. Matokeo ya utafitiyanaonesha kwamba, wahusika wanawake wamesawiriwa kwa mtazamo hasi katika ngano hizi kuliko ule chanya. Aidha uchunguzi umegundua kwamba ngano hizi zimeyazungumzia masuala mbalimbali yanayowakandamiza wanawake katika jamii ikiwepo mfumo dume. Miongoni mwa masuala hayo ni uhuru wa mwanamke ambao hujengwa na dhamira nyingine kama vile ulezi, uzalishaji mall, uvurnilivu, ushujaa, umalaya, uchawi, rnwenye wive, chombo cha starehe na kadhalika. Utafiti umegundua kwamba hit imetokana na mfumo wa jamii unavyomtazama mwanamke. Mwisho limetolewa hitimisho kuu la utafiti, lililoainisha nyanja mbalimbali za kiutafiti zinazoweza kuibuliwa katika wahusika wengine katika kazi za fasihi simulizi hususani ngano.