Athari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzo

dc.contributor.authorMalindi, Bakita
dc.date.accessioned2019-10-28T11:24:49Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.available2019-10-28T11:24:49Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:42Z
dc.date.issued2014
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8295.4.M34)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu Athari za matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo, uliofanyika katika mkoa wa Mara manispaa ya Musoma katika kata za Mwisenge, Iringo, Mkendo, Nyakato na Kamnyonge. Utafiti huu ulihusisha jumla ya watafitiwa 40 ambapo wanawake walikuwa 20 na wanaume walikuwa 20, vilevile kila kata ilitoa watafitiwa 8. Utafiti huu ulilenga kwanza kubaini matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Pili, kubainisha makundi ya jamii yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa kuzingatia jinsi, umri na kiwango cha elimu. Tatu, kueleza sababu za kutumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo.Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha wazi kuwa kuna baadhi ya matamshi ya Kikwaya yanayotumika katika Kiswahili cha mazungumzo. Matamshi hayo ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo hutokana na matumizi ya mara kwa mara ya lugha ya Kikwaya, kutopata elimu na kutumia lugha mbili au zaidi katika eneo moja. Utafiti huu pia umedhihirisha makundi ya jamii ya watafitiwa yanayotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo. Makundi hayo mtafiti ameyagawa katika sehemu mbili, yaani kuna makundi ya watafitiwa wanaotumia matamshi ya Kikwaya katika Kiswahili cha mazungumzo kwa wingi, na kuna makundi ya watafitiwa wasiotumia sana matamshi ya Kikwaya. Makundi yanayotumia sana matamshi ya Kikwaya ni wazee (72%), wakulima (74%), wasiosoma (72%), wanawake (70%) na wafanyabiashara (60%). Hali kadhalika makundi ya watafitiwa yasiyotumia sana matamshi ya Kikwaya ni vijana (39%),waliosoma shule (48%), wanaume (52%) na wafanyakazi (45%).en_US
dc.identifier.citationMalindi, B (2014) Athari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzo,Master dissertation, University of Dar es Salaam. Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3469
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectMaraen_US
dc.subjectTanzania (Region)en_US
dc.subjectLanguageen_US
dc.subjectBantu languagesen_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectKwaya languageen_US
dc.titleAthari ya matamshi ya kikwaya katika kiswahili cha mazungumzoen_US
dc.typeThesisen_US

Files