Ulinganishi wa methali za Kiswahili na za Kichina

No Thumbnail Available
Date
2010
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Methali ni kazi mojawapo ya fasihi simulizi ambayo inatumia maneno machache, kimafumbo au kwa kupigia mifano ili kuelezea maadili na uzoefu wa shughuli mbalimbali ambazo zinaitambulisha jamii fulani. Kazi hii inachunguza na kulinganisha muundo, tamathali za semi, taswira na dhamira za methali za Kiswahili na za Kichina. Methali za Kiswahili na za Kichina zinatofautiana kimuundo na zinatumia tamathali za semi kwa kiwango tofauti, tena zinatumia taswira zinazofahamika na jamii yenyewe. Hali kadhalika, methali za Kiswahili na za Kichina zinafanana kwa kiasi kikubwa kimaudhui. Methali hizo huwafundisha watu jinsi wanavyotakiwa kuwa na tabia nzuri, kuishi vizuri na watu na kushughulikia mambo ya ulimwenguni. Vipengele vyote vya kifani na kimaudhui vinathibitisha sifa za methali. Kutokana na ulinganishi wa methali, inadhihirika kwamba sifa za kijamii na kiutamaduni baina ya Waswahili na ya Wachina zinafanana. Watu wa jamii hizo wanaweza kuelewana kwa urahisi itikadi na amali zao.
Description
Kinapatikana katika mfumo wa kuprintiwa
Keywords
Methali, Kiswahili, Kichina
Citation
Lei, Z (2010) Ulinganishi wa methali za Kiswahili na za Kichina. Uzamili wa Fasihi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kinapatikana tovuti ya http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx?