Usawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya za Kiswahili: mifano kutoka Kiu (1972) na Usiku Utakapokwisha (1990)

dc.contributor.authorMattee, Spice
dc.date.accessioned2019-08-14T11:31:31Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:40Z
dc.date.available2019-08-14T11:31:31Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:40Z
dc.date.issued2012
dc.descriptionAvailable in print formen_US
dc.description.abstractTasnifu hii imetokana na utafiti uliofanywa kwa lengo la kuchunguza usawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya ya Usiku Utakapokwisha na Kiu. Riwaya hizi zilichaguliwa kwa sababu zinakidhi malengo ya utafiti huu. Data zilikusanywa za maktabani na uwandani kutoka katika shule ya sekondari ya Kibasila na Jitegemee katika wilaya ya Temeke. Katika utafiti huu tuliongozwa na nadharia ya uhalisia ambayo hueleza mambo kiualisia na yanavyotendeka katika jamii. Pia tunaelezwa kuwa katika nadharia ya uhalisia mtunzi huwachora wahusika kama walivyo katika jamii. Na katika matokeo yetu tumedhihrisha hili ya kwamba waandishi wote wawili wa riwaya husika wamefanikiwa kuwachora wahusika ambao wanabeba uhalisia wa mambo kama vile kutoa rushwa ya ngono ili kujipatia utajiri. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa, mara nyingine, wanawake hulazimika kutoa rushwa ya ngono ili kujipatia ajira, huku wanaume wakilazimika kutoa fedha. Vilevile matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba katika tendo zima la utoaji rushwa ya ngono mshiriki anaweza asinufaike na rushwa hiyo bali mtu wa pembeni ambaye ni wa kati. Pia wasichana kujiingiza katika rushwa ya ngono ni kutokana na umaskini uliokithiri katika jamii. Mwisho, utafiti huu umetoa mapendekezo ya maeneo yanayohitajiwa kufanyika utafiti zaidi ili kupanua wigo wa marejeleo juu ya rushwa ya ngono na Fasihi kwa ujumla.en_US
dc.identifier.citationMattee, S (2012) Usawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya za Kiswahili: mifano kutoka Kiu (1972) na Usiku Utakapokwisha (1990), Master dissertation, University of Dar es Salaam. (Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3447
dc.language.isootheren_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.titleUsawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya za Kiswahili: mifano kutoka Kiu (1972) na Usiku Utakapokwisha (1990)en_US
dc.typeThesisen_US

Files