Usawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya za Kiswahili: mifano kutoka Kiu (1972) na Usiku Utakapokwisha (1990)

Date

2012

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Abstract

Tasnifu hii imetokana na utafiti uliofanywa kwa lengo la kuchunguza usawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya ya Usiku Utakapokwisha na Kiu. Riwaya hizi zilichaguliwa kwa sababu zinakidhi malengo ya utafiti huu. Data zilikusanywa za maktabani na uwandani kutoka katika shule ya sekondari ya Kibasila na Jitegemee katika wilaya ya Temeke. Katika utafiti huu tuliongozwa na nadharia ya uhalisia ambayo hueleza mambo kiualisia na yanavyotendeka katika jamii. Pia tunaelezwa kuwa katika nadharia ya uhalisia mtunzi huwachora wahusika kama walivyo katika jamii. Na katika matokeo yetu tumedhihrisha hili ya kwamba waandishi wote wawili wa riwaya husika wamefanikiwa kuwachora wahusika ambao wanabeba uhalisia wa mambo kama vile kutoa rushwa ya ngono ili kujipatia utajiri. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa, mara nyingine, wanawake hulazimika kutoa rushwa ya ngono ili kujipatia ajira, huku wanaume wakilazimika kutoa fedha. Vilevile matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba katika tendo zima la utoaji rushwa ya ngono mshiriki anaweza asinufaike na rushwa hiyo bali mtu wa pembeni ambaye ni wa kati. Pia wasichana kujiingiza katika rushwa ya ngono ni kutokana na umaskini uliokithiri katika jamii. Mwisho, utafiti huu umetoa mapendekezo ya maeneo yanayohitajiwa kufanyika utafiti zaidi ili kupanua wigo wa marejeleo juu ya rushwa ya ngono na Fasihi kwa ujumla.

Description

Available in print form

Keywords

Swahili literature

Citation

Mattee, S (2012) Usawiri wa rushwa ya ngono katika riwaya za Kiswahili: mifano kutoka Kiu (1972) na Usiku Utakapokwisha (1990), Master dissertation, University of Dar es Salaam. (Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)