Dhima ya visasili katika riwaya ya Kiswahili: uchambuzi wa Nagona, Mzingile na Ziraili na Zirani

dc.contributor.authorMbijima, Rose
dc.date.accessioned2020-04-16T12:16:29Z
dc.date.available2020-04-16T12:16:29Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.M3254)en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu “Dhima ya Visasili katika Riwaya ya Kiswahili: Uchambuzi wa Nagona (1990), Mzingile (1991) na Ziraili na Zirani (1999).” Tulifanya utafiti ili kuhakiki madai ya baadhi ya wataalamu wa fasihi wanaoona kuwa uandishi wa Kezilahabi unarudisha nyuma maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Tulichokifanya ni kujadili dhima ya visasili katika riwaya tatu tulizoziteua ili kuona kama madai hayo yana ukweli. Utafiti huu, kwa hiyo, umechunguza dhima ya visasili ambayo ni matini simulizi, ndani ya riwaya ambayo ni matini andishi. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha visasili katika riwaya teule; kujadili dhima ya kimaudhui ya visasili katika riwaya teule na kujadili dhima ya kifani ya visasili katika riwaya teule. Utafiti huu ni wa maktabani na uwandani. Ili kufikia malengo ya utafiti huu mbinu za aina mbili zilitumika kukusanya data. Mbinu ya mahojiano ilitumika kukusanya data za uwandani wakati, kwa upande wa utafiti wa maktabani, mbinu ya kusoma matini ilitumika. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo na Nadharia za Mwingilianomatini na Uhemenitiki ndizo zimetumika katika uchambuzi wa data. Utafiti umebaini kwamba riwaya teule zimesheheni visasili ambavyo vina dhima za kimaudhui na kifani. Dhima hizo ni kubwa na nyingi kiasi cha kuwa na athari chanya katika utanzu wa riwaya na hivyo kuchangia katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili na siyo kuyarudisha nyuma.en_US
dc.identifier.citationMbijima, R. (2016) Dhima ya visasili katika riwaya ya Kiswahili: uchambuzi wa Nagona, Mzingile na Ziraili na Zirani, Tasnifu ya uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaamen_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/9523
dc.language.isoswen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectHistory and criticismen_US
dc.titleDhima ya visasili katika riwaya ya Kiswahili: uchambuzi wa Nagona, Mzingile na Ziraili na Ziranien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mbijima, Rose.pdf
Size:
138.37 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description:
Collections