Dhima ya visasili katika riwaya ya Kiswahili: uchambuzi wa Nagona, Mzingile na Ziraili na Zirani
Loading...
Date
2016
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
University of Dar es Salaam
Abstract
Utafiti huu unahusu “Dhima ya Visasili katika Riwaya ya Kiswahili: Uchambuzi wa Nagona (1990), Mzingile (1991) na Ziraili na Zirani (1999).” Tulifanya utafiti ili kuhakiki madai ya baadhi ya wataalamu wa fasihi wanaoona kuwa uandishi wa Kezilahabi unarudisha nyuma maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Tulichokifanya ni kujadili dhima ya visasili katika riwaya tatu tulizoziteua ili kuona kama madai hayo yana ukweli. Utafiti huu, kwa hiyo, umechunguza dhima ya visasili ambayo ni matini simulizi, ndani ya riwaya ambayo ni matini andishi. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha visasili katika riwaya teule; kujadili dhima ya kimaudhui ya visasili katika riwaya teule na kujadili dhima ya kifani ya visasili katika riwaya teule. Utafiti huu ni wa maktabani na uwandani. Ili kufikia malengo ya utafiti huu mbinu za aina mbili zilitumika kukusanya data. Mbinu ya mahojiano ilitumika kukusanya data za uwandani wakati, kwa upande wa utafiti wa maktabani, mbinu ya kusoma matini ilitumika. Data zilizokusanywa zimewasilishwa kwa njia ya maelezo na Nadharia za Mwingilianomatini na Uhemenitiki ndizo zimetumika katika uchambuzi wa data. Utafiti umebaini kwamba riwaya teule zimesheheni visasili ambavyo vina dhima za kimaudhui na kifani. Dhima hizo ni kubwa na nyingi kiasi cha kuwa na athari chanya katika utanzu wa riwaya na hivyo kuchangia katika maendeleo ya riwaya ya Kiswahili na siyo kuyarudisha nyuma.
Description
Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.M3254)
Keywords
Swahili literature, History and criticism
Citation
Mbijima, R. (2016) Dhima ya visasili katika riwaya ya Kiswahili: uchambuzi wa Nagona, Mzingile na Ziraili na Zirani, Tasnifu ya uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam