Matumizi ya lugha ya picha katika nyimbo za Kinyankole zinazohusu ukimwi

Date

2011

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Utafiti huu umechunguza Matumizi ya Lugha ya Picha katika Nyimbo za Kinyankole. Utafiti ulihusisha nyimbo mbalimbali zinazohusu UKIMWI katika kabila la Wanyankole. Lengo lilikuwa ni kuchunguza mbinu zinazotumiwa na watunzi wa nyimbo hizi katika kuelimisha jamii kuhusu UKIMWI. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Upokezi iliyoasisiwa na Hans-Robert Jauss (1960). Mtafiti alichunguza vipengele na misingi ya nadharia hii ambayo ilisaidia katika uwasilishaji na uchambuzi wa data. Utafiti ulihusisha sehemu za uwandani na maktabani, ambapo data zilizopatikana zilichambuliwa kwa kutumia nadharia ya Upokezi. Maktabani mtafiti alisoma vitabu, na makala mbalimbali ambazo zilisaidia katika upatikanaji wa data muhimu. Uwandani, mtafiti alipata data kutoka kwa watunzi na waimbaji wa nyimbo za UKIMWI. Katika utafiti huu, imeonekana kuwa nyimbo hizi zimetoa mchango mkubwa katika kuwashauri na kuwahamasisha wanajamii kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI. Vilevile utafiti huu umebainisha kuwa suala la unyanyapaa kwa wagonjwa wa UKIMWI lipo na wagojwa hawa wananyanyapaliwa hata na ndugu zao. Ingawa jitihada za kuzuia unyanyapaa zipo na zinasisitizwa. Pia imegundulika kuwa, baadhi ya watu wenye VVU wanawaambukiza wengine kwa makusudi kabisa. Hii ni kutokuwa na elimu ya kutosha. Utafiti huu, unapendekeza jitihada zaidi zitolewe kuhusiana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.

Description

Available in print

Keywords

Nyankole language, Songs, Nyankole, AIDS - Diseases, Uganda

Citation

Perpetua, A (2011) Matumizi ya lugha ya picha katika nyimbo za Kinyankole zinazohusu ukimwi. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx