Ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na Nje ya darasa katika ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili ikiwa lugha ya pili katika jamii ya Wairaki.

dc.contributor.authorGinni, Veronica Felix
dc.date.accessioned2021-11-16T11:50:41Z
dc.date.available2021-11-16T11:50:41Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8701.T34.G46)en_US
dc.description.abstractSuala la mazingira ya ujifunzaji lugha ya pili (kuanzia sasa Lg2) limewavuta wataalamu mbalimbali. Hata hivyo hakuna utafiti uliofanyika kuhusu ulinganishi wa msamiati katika mazingira ya darasani na nje ya darasa katika kumwezesha mjifunzaji kumudu lugha ya Kiswahili katika jamii ya Wairaki. Hivyo, utafiti huu umechunguza ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na nje ya Darasa katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 katika jamii ya Wairaki. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vitatu vya Gilala, Maran na Kilimatembo katika kata ya Rhotia, Wilayani Karatu, Mkoani Arusha, Tanzania. utafiti ulikuwa na malengo matatu, kubainisha mazingira ya darasani na nje ya darsas yanayodhihirika katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya Wairaki, kuchungua dhima za mazingira ya darasani na nje ya darasa katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii Wairaki na kulinganisha dhima za mazingira ya darasani na nje ya darasa katika ujifunzaji msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya wairaki. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia kuu mbili, hojaji na usaili. Aidha, utafiti wa data uliongozwa na nadharia ya Utamaduni-Jamii. Matokeo ya utafiti ni kuwa mazingira ya nje ya darasa yanayodhihirika katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ni pamoja na mabango yaliyopo barabarani na madukani, mabanda ya video. Mazingira ya darasani yamehusisha: vitabu na matini mbalimbali, kamusi za Kiswahili. Vilevile, imebainika kuwa mazingira ya nje ya darasa yana dhima za kujenga kumbukumbu na kujiamini, kuchochea udadisi. Nayo mazingira ya darasani yana dhima za kujenga uelewa, kutoa motisha kwa mjifunzaji lugha . pia utafiti umebaini kuwa mazigira ya darasani na nyumbani yana dhima kubwa katika ujifunzaji wa Lg2 lakini kwa kiwango tofautitofauti. Hata hivyo, mazingira ya darasani yanaonekana kuwa ni faafu Zaidi katika ujifunzaji wa misamiati wa Kiswahili kwa wanafunzi wa Kiiraki kuliko mazingira ya nje ya darasa. Hii ni kutokana na matumizi makubwa ya Kiswahili katika jamii hiyo. Utafiti huu unapendekeza kufayika kwa tafiti za kina katka ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa kuchunguza tofauti za ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya Kibantu na ule wa jamii ambazo si za kibantu katika vipengele vya fonolojia, mofolojia na sintaksia za lugha husika.en_US
dc.identifier.citationGinni, V. F(2019) Ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na Nje ya darasa katika ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili ikiwa lugha ya pili katika jamii ya Wairaki.Tasinifu ya Shahada ya Udhamiri ,Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Dar es salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/16472
dc.language.isoenen_US
dc.publisherChuo Kikuu cha Dar es salaamen_US
dc.subjectClassroom environmenten_US
dc.subjectSwahili languageen_US
dc.subjectSecond language acquisitionen_US
dc.subjectVocabulariesen_US
dc.subjectStudy and learningen_US
dc.subjectIraq(African people)en_US
dc.titleUlinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na Nje ya darasa katika ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili ikiwa lugha ya pili katika jamii ya Wairaki.en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Veronica Felix Ginai.pdf
Size:
977.39 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: