Ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na Nje ya darasa katika ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili ikiwa lugha ya pili katika jamii ya Wairaki.
Loading...
Date
2019
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Abstract
Suala la mazingira ya ujifunzaji lugha ya pili (kuanzia sasa Lg2) limewavuta wataalamu mbalimbali. Hata hivyo hakuna utafiti uliofanyika kuhusu ulinganishi wa msamiati katika mazingira ya darasani na nje ya darasa katika kumwezesha mjifunzaji kumudu lugha ya Kiswahili katika jamii ya Wairaki. Hivyo, utafiti huu umechunguza ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na nje ya Darasa katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 katika jamii ya Wairaki. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vitatu vya Gilala, Maran na Kilimatembo katika kata ya Rhotia, Wilayani Karatu, Mkoani Arusha, Tanzania. utafiti ulikuwa na malengo matatu, kubainisha mazingira ya darasani na nje ya darsas yanayodhihirika katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya Wairaki, kuchungua dhima za mazingira ya darasani na nje ya darasa katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii Wairaki na kulinganisha dhima za mazingira ya darasani na nje ya darasa katika ujifunzaji msamiati wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya wairaki. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia njia kuu mbili, hojaji na usaili. Aidha, utafiti wa data uliongozwa na nadharia ya Utamaduni-Jamii. Matokeo ya utafiti ni kuwa mazingira ya nje ya darasa yanayodhihirika katika ujifunzaji wa msamiati wa Kiswahili ni pamoja na mabango yaliyopo barabarani na madukani, mabanda ya video. Mazingira ya darasani yamehusisha: vitabu na matini mbalimbali, kamusi za Kiswahili. Vilevile, imebainika kuwa mazingira ya nje ya darasa yana dhima za kujenga kumbukumbu na kujiamini, kuchochea udadisi. Nayo mazingira ya darasani yana dhima za kujenga uelewa, kutoa motisha kwa mjifunzaji lugha . pia utafiti umebaini kuwa mazigira ya darasani na nyumbani yana dhima kubwa katika ujifunzaji wa Lg2 lakini kwa kiwango tofautitofauti. Hata hivyo, mazingira ya darasani yanaonekana kuwa ni faafu Zaidi katika ujifunzaji wa misamiati wa Kiswahili kwa wanafunzi wa Kiiraki kuliko mazingira ya nje ya darasa. Hii ni kutokana na matumizi makubwa ya Kiswahili katika jamii hiyo. Utafiti huu unapendekeza kufayika kwa tafiti za kina katka ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa kuchunguza tofauti za ujifunzaji wa Kiswahili ikiwa Lg2 kwa wanafunzi wa jamii ya Kibantu na ule wa jamii ambazo si za kibantu katika vipengele vya fonolojia, mofolojia na sintaksia za lugha husika.
Description
Available in print form, East Africana collection, Dr. Wilbert Chagula Library, class mark (THS EAF PL8701.T34.G46)
Keywords
Classroom environment, Swahili language, Second language acquisition, Vocabularies, Study and learning, Iraq(African people)
Citation
Ginni, V. F(2019) Ulinganishi wa dhima za mazingira ya Darasani na Nje ya darasa katika ujifunzaji wa Msamiati wa Kiswahili ikiwa lugha ya pili katika jamii ya Wairaki.Tasinifu ya Shahada ya Udhamiri ,Chuo Kikuu cha Dar es salaam,Dar es salaam.