Mfuatano wa mofimu nyambulishi katika vitenzi vya Kikinga

dc.contributor.authorGawasike, Arnold
dc.date.accessioned2019-06-28T08:11:05Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:36Z
dc.date.available2019-06-28T08:11:05Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:36Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in printen_US
dc.description.abstractSuala la unyambulishaji na mfuatano wa mofimu nyambulishi limewavuta wataalamu wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanyika katika lugha ya Kikinga. Kwa hiyo utafiti huu ulikuwa jaribio la kuchunguza unyambulishaji wa vitenzi katika lugha hii na kubainisha kanuni za mfuatano wa mofimu nyambulishi hizo. Aidha, utafiti umechunguza unyambulishi wa aina tano. Utafiti umefanyika katika kata za: Mbalatse, Ipepo na Ukwama, wilaya ya Makete mkoa wa Iringa, Tanzania. Ili kufanikisha kazi hii, Kanuni Tazamishi (KAT) iliongoza utafiti huu, yaani unyambulishaji wa vitenzi kimofolojia unaakisi unyambulishaji wa vitenzi kisintaksia. Mbinu za utafiti zilihusu: usampulishaji, ukusanyaji, uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Data ya utafiti ni ya kutoka uwandani ambapo vitenzi viliteuliwa na kuwekwa katika kategoria mbili; vitenzi visoukomo katika kundi moja na vitenzi vya silabi moja katika kundi jingine. Kazi imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza, imeeleza kiini cha utafiti na utaratibu uliozingatiwa katika kufanikisha utafiti. Sura ya pili, imeshughulikia mapitio ya maandiko kuhusiana na unyambulishaji na mfuatano wa mofimu katika lugha. Mapitio haya yamebainisha kuwa minyambuliko na mifuatano ya mofimu katika lugha ipo. Sura ya tatu, imehusu mbinu za utafiti ambapo populesheni, sampuli, usampulishaji pamoja na njia tatu za ukusanyaji data zilibainishwa. Sura ya nne, imeshughulikia uchanganuzi na uwasilishaji wa data. Kwa ujumla data, iliyopatikana imechanganuliwa kwa njia ya maelezo na kanuni. Kanuni Tazamishi ya Baker (1985) ndiyo iliyoongozo mjadala na uchanganuzi wa data hii. Sura ya tano imeshughulikia matokeo, hitimisho, na tafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yamebainisha minyambuliko mitano na kwamba, lugha ya Kikinga inapangilia mofimu nyambulishi zake kwa mujibu wa Kanuni Tazamishi inayodai unyambulishaji kimofolojia huakisi unyambulishaji sintaksia. Aidha, kanuni ya uukiliwaji iliyoundwa ina tenda kazi pia, katika mfuatano wa mofimu nyambulishi katika lugha ya Kikinga, yaani mofimu moja ikitangulia ina kawaida ya kuukilia mofimu ambazo zinaweza kuifuata na ama kutoifuata yenyewe.en_US
dc.identifier.citationGawasike, A (2011) Mfuatano wa mofimu nyambulishi katika vitenzi vya Kikinga. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspxen_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3404
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectKinga languageen_US
dc.subjectBantu languageen_US
dc.subjectMorphemicsen_US
dc.subjectTanzaniaen_US
dc.titleMfuatano wa mofimu nyambulishi katika vitenzi vya Kikingaen_US
dc.typeThesisen_US

Files