Usimulizi katika riwaya ya kusadikika (1951).

dc.contributor.authorHenry, Jane
dc.date.accessioned2020-02-03T12:44:51Z
dc.date.available2020-02-03T12:44:51Z
dc.date.issued2016
dc.descriptionAvailable in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.H46)en_US
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza usimulizi katika riwaya ya Kusadikika (1951). Malengo mahususi yalikuwa matatu ambayo ni pamoja na kubainisha vipengele vya usimulizi jinsi vinavyojibainisha katika riwaya ya Kusadikika, kuchambua utokezaji wa msimulizi kwa kuzingatia dhima zake wakati wa usimulizi, kujadili namna ambavyo vipengele vya usimulizi vinavyoweza kuibua maana ya kazi ya riwaya. Nadharia ya Naratolojia ndiyo iliyotumika katika uchambuzi wa data ya tasinifu hii. Mbinu za ukusanyaji wa data zilifanyikia maktabani kwa kusoma maandiko na machapisho mbalimbali yanayohusu mada husika. Kwa ujumla, riwaya za Shaaban Robert zimefanyiwa uchambuzi na wataalamu mbalimbali, ingawa kwa kiasi kikubwa wataalamu hao wamejikita zaidi katika fani na maudhui. Pamoja na kuzua mijadala kutokana na uchambuzi, riwaya hizo hazijafanyiwa uchambuzi wa kutosha kwa kuzingatia sifa zake za kiusimulizi. Hivyo, kwa kutumia Nadharia ya Naratolojia, tasinifu hii inachunguza suala la usimulizi kwa kuzingatia vipengele vyake. Hoja ya msingi ya tasinifu hii ni kuwa usimulizi na dhima za msimulizi ni vipengele vinavyosaidia kubaini maudhui na malengo ya kazi inayohusika. Hivyo, katika tasinifu hii vipengele mbalimbali vya usimulizi pamoja na dhima za msimulizi vimebainishwa na kufafanuliwa. Zaidi ya kubainishwa kwa mambo hayo, pia kumetolewa hitimisho la tasinifu na mapendekezo ya maeneo yanayohitaji kutafitiwa kwa tafiti zitakazofuata.en_US
dc.identifier.citationHenry, J. (2016). Usimulizi katika riwaya ya kusadikika (1951). Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.en_US
dc.identifier.urihttp://41.86.178.5:8080/xmlui/handle/123456789/6888
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.titleUsimulizi katika riwaya ya kusadikika (1951).en_US
dc.typeThesisen_US

Files

Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Henry 2016.pdf
Size:
83.78 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: