Usimulizi katika riwaya ya kusadikika (1951).

Date

2016

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza usimulizi katika riwaya ya Kusadikika (1951). Malengo mahususi yalikuwa matatu ambayo ni pamoja na kubainisha vipengele vya usimulizi jinsi vinavyojibainisha katika riwaya ya Kusadikika, kuchambua utokezaji wa msimulizi kwa kuzingatia dhima zake wakati wa usimulizi, kujadili namna ambavyo vipengele vya usimulizi vinavyoweza kuibua maana ya kazi ya riwaya. Nadharia ya Naratolojia ndiyo iliyotumika katika uchambuzi wa data ya tasinifu hii. Mbinu za ukusanyaji wa data zilifanyikia maktabani kwa kusoma maandiko na machapisho mbalimbali yanayohusu mada husika. Kwa ujumla, riwaya za Shaaban Robert zimefanyiwa uchambuzi na wataalamu mbalimbali, ingawa kwa kiasi kikubwa wataalamu hao wamejikita zaidi katika fani na maudhui. Pamoja na kuzua mijadala kutokana na uchambuzi, riwaya hizo hazijafanyiwa uchambuzi wa kutosha kwa kuzingatia sifa zake za kiusimulizi. Hivyo, kwa kutumia Nadharia ya Naratolojia, tasinifu hii inachunguza suala la usimulizi kwa kuzingatia vipengele vyake. Hoja ya msingi ya tasinifu hii ni kuwa usimulizi na dhima za msimulizi ni vipengele vinavyosaidia kubaini maudhui na malengo ya kazi inayohusika. Hivyo, katika tasinifu hii vipengele mbalimbali vya usimulizi pamoja na dhima za msimulizi vimebainishwa na kufafanuliwa. Zaidi ya kubainishwa kwa mambo hayo, pia kumetolewa hitimisho la tasinifu na mapendekezo ya maeneo yanayohitaji kutafitiwa kwa tafiti zitakazofuata.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.H46)

Keywords

Swahili literature

Citation

Henry, J. (2016). Usimulizi katika riwaya ya kusadikika (1951). Tasnifu ya Uzamili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.