Uzingativu wa vipengele vya kifasihi katika kazi za fasihi ya kiswahili zilizotafsiriwa Mifano kutoka Tafsiri ya Julius Caezar ya J.K. Nyerere (1963)

Date

2015

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

University of Dar es Salaam

Abstract

Lengo letu ni kuchunguza vipengele vya kifasihi katika tafsiri ya kazi za fasihi ya Kiswahili ili kuona kama vipengele hivyo vimezingatiwa kama vilivyotumiwa katika matini ya lugha chanzi au havikuzingatiwa. Ili kufanikisha lengo hilo la utafiti, nadharia mbili zilitumika; nadharia ya Hemenitiki na nadharia ya tafsiri ya Ulinganifu. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni watafitiwa kusoma matini, usaili, hojaji na usomaji wa nyaraka maktabani. Vifaa vilivyotumika katika kukusanya data ni karatasi, kalamu, kompyuta, shajara, hojaji na dodoso. Mikabala miwili ilitumika katika uchambuzi wa data; nayo ni mkabala wa kitaamuli na mkabala wa kitakwimu. Kwa ujumla, matokeo ya uchambuzi wa data yalituwezesha kujibu maswali ya utafiti kwani matokeo yalibainisha kuwa vipengele vya kifasihi vilivyozingatiwa kwa kiasi kikubwa na vilivyozingatiwa kwa kiasi kidogo. Sababu za kuzingatiwa kwa viwango tofauti ni tofauti baina ya lugha chanzi na lugha lengwa kimuundo na kitamaduni, tofauti ya mandhari ya kiwakati kati ya kuandikwa matini chanzi na wakati wa kutafsiri, kutokuwa na taaluma ya fasihi na tafsiri kwa mfasiri, hadhira lengwa tofauti kati ya ile ya matini chanzi na ya matini lengwa na mfasiri kutokuwa na lengo maalumu la kutafsiri. Pia athari za kuzingatiwa na kutozingatiwa kwa vipengele hivyo ni kuhafifishwa kwa ujumbe na dhamira pamoja na kupunguza mguso wa hisia uliokuwepo katika matini chanzi. Vilevile ilibainika kuwa mambo ya kuzingatia wakati wa kutafsiri matini za fasihi ili kuhakikisha uzingativu wa vipengele vya fasihi unadumishwa ni mfasiri kuwa na ujuzi wa taaluma ya fasihi na tafsiri na kuepuka athari binafsi za upendeleo wakati wa kutafsiri.

Description

Available in print form, East Africana Collection, Dr. Wilbert Chagula Library, Class mark (THS EAF PL8703.5.T4756)

Keywords

Swahili literature

Citation

Thomas, E. Z. (2015). Uzingativu wa vipengele vya kifasihi katika kazi za fasihi ya kiswahili zilizotafsiriwa Mifano kutoka Tafsiri ya Julius Caezar ya J.K. Nyerere (1963), Master dissertation, Chuo kikuu cha Dar es Salaam.