Mnyambuliko wa vitenzi katika lugh ya Kijita
Date
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Suala la Mnyambuliko na michakato ya kimofofonolojia limewavutia wataalamu wingi. Hata hivyo, hakuna utafiti mujarabu ambao umefanyika katika lugha ya Kijita. Utafiti huu umechunguza minyambuliko ya vitenzi katika lugha ya Kijita na kubainisha vipashiol, michakato na kanuni zinazoukilia ruwaza ya mnyambuliko katika lugha hiyo. Kwa ujumla, Nadharia ya Isimu fafanuzi pamoja na kiunzi Rasmi cha Fonolojia Zalishi ndizo zimeongoza majadala na uchnganuzi wa data hii. Sura ya tano imeshughlikia matokeo, hitimisho, na mapendekezo ya tafiti fuatishi. Matokeo ya utafiti yamebainisha minyambuliko mitano na kwamba, lugh ya Kijita ina vipashio, michakato na kanuni zinazoukilia utokeaji wake. Aidha michakato ya kimofofonolojia imebainishwa na kuelezwa kwa mujibu wa Kiunzi Rasmi cha Fonolojia Zalishi na pale ilipolazimu kanuni zimefafanuliwa na kurasimishwa kwa kuzingatia iktisadi na uwazi wa kanuni.