Usawiri wa wahusika walemavu katika fasihi ya kiswahili

dc.contributor.authorMukama, Shukuru
dc.date.accessioned2019-07-11T11:00:52Z
dc.date.accessioned2020-01-07T16:26:38Z
dc.date.available2019-07-11T11:00:52Z
dc.date.available2020-01-07T16:26:38Z
dc.date.issued2011
dc.descriptionAvailable in print formen_US
dc.description.abstractUtafiti huu, umechunguza jinsi Wahusika wenye ulemavu walivyosawiriwa katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu ulihusisha riwaya za Njozi Iliyopotea, Takadini na Nisamehe. Kwa kutumia nadharia ya Udenguzi, iliyoasisiwa na Derrida (1976), mtafiti alichunguza vipengele na misingi muhimu ya nadharia hii ambayo ilisaidia katika uchambuzi na uwasilishaji wa data husika. Utafiti ulihusisha sehemu za uwandani na maktabani ambapo data zilizopatikana zilichambuliwa kwa kutumia nadharia hiyo ya udenguzi. Maoni ya walemavu yalilinganishwa na jinsi waandishi walivyowatumia wahusika wenye ulemavu katika kazi za fasihi. Katika utafiti huu imeonekana kuwa, watu wenye ulemavu wanapata taabu katika jamii. Hii inatokana na ulemavu walionao. Kwa kuwa waandishi wa kazi za fasihi wanaandika yale yaliyomo katika jamii, ni wazi kuwa yale wanayoyaandika katika kazi za kifasihi hayana tofauti na yale yaliyomo katika jamii. Vilevile imebainika katika utafiti huu kuwa, watu wenye ulemavu hawakuwa na welewa wowote kuhusiana na jinsi wanavyotumika katika kazi za kifasihi, utafiti huu umewafungua macho na umewapa welewa na kuwapa mwanga wa nini kinaendelea katika fasihi ya Kiswahili. Imependekezwa katika utafiti huu kuwa, uchunguzi zaidi kuhusu watu wenye ulemavu unahitajika. Hasa walemavu wa aina nyingine na katika kazi nyingine za kifasihi kama vile tamthiliya na ushairi.en_US
dc.identifier.citationMukama, S.(2011) Usawiri wa wahusika walemavu katika fasihi ya kiswahili. Master dissertation, University of Dar es Salaam. Available at (http://41.86.178.3/internetserver3.1.2/detail.aspx)en_US
dc.identifier.urihttp://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/3427
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Dar es Salaamen_US
dc.subjectSwahili literatureen_US
dc.subjectRiwaya ya Nisameheen_US
dc.subjectRiwaya ya Takadinien_US
dc.subjectRiwaya ya Njozi iliyopoteaen_US
dc.titleUsawiri wa wahusika walemavu katika fasihi ya kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US

Files